Loubna Mostafa anahakikisha nafasi ya nne ya michuano ya dunia ya kuogelea kwa Paralympics

 Loubna Mostafa, mchezaji wa klabu ya Zamalek na timu ya kitaifa ya kuogelea kwa Paralympics kwa watu wenye mahitaji maalum ameweza kushinda nafasi ya nne ya mashindano ya michuano ya dunia ya watu wenye mahitaji maalum yanayofanyika nchini Australia.

 

Mchezaji huyo ameshinda nafasi ya nne katika mbio ya mita 200 ya nyuma, kwa muda wa 3.58.18 katika michuano inayoendelea mpaka siku ya  21, mwezi huu wa Oktoba.

 

Loubna Mostafa ni mchezaji wa pekee anayeshiriki katika michuano baada ya kufuzu kwake katika awamu tatu ya fainali, wakati huo akishinda medali ya kidhahabu ya mashindano hayo, atapata tiketi ya kufikia Paralympics za Tokyo 2020.

 

Inatajwa kuwa Loubna Mostafa amehakikisha zaidi ya medali 170 mbalimbali katika michuano tofauti za kuogelea kwa Paralympics anayezishiriki.

Comments