Sikukuu ya Shamu El -Nasiim

Misingi ya Sikukuu ya Shamu El -Nasiim inarejea Misri ya kifirauni. Wakati ambapo mafarao waliisheherekea  sikukuu hiyo tokea mwaka 270 K.k.  Na  ilikuwa ikiitwa "SHAMUS"  nalo ni neno la kihiroghlifia linamaanisha kuyarejesha maisha  kwani walikuwa wakiamini kwamba zama za mwanzo za uumbaji wa ulimwengu zilianzia siku hiyo.  Na baadaye  limeongezwa neno  Nasiim kwa kulizingatia kuwa ni mwanzo wa majira ya vuli na hali ya hewa ya wastani. 

 

 Sherehe hiyo ilihamishwa kwa mayahudi ambao waliitia "Sikukuu ya Mapumziko" na waliizingatia kuwa ni mwisho wa mwaka wa kihibru . Wakati ambapo siku hiyo ilienda sambamba na kutoka kwao Misri katika zama ya Nabii Mussa. Na baadaye sherehe hiyo ilihamishwa kwa  wakristo wa Misri ambao waliitia "Sikukuu ya Kufufuliwa kwa Yesu". Na hayo kuashiria itikadi zao kuhusu kusulubiwa kwa Yesu na kutoka kwake kaburini .

 Tangu wakati huo siku hiyo ikawa sikukuu rasmi katika mataifa mbalimbali ya kiarabu. VileVile sikukuu ya Shamu Nasiim ni maarufu kwa jina la "NEROZ" nalo ni neno  la kiajemi lililoingizwa kwenye lugha ya kiarabu  na linamaanisha "siku mpya".  Sikukuu hiyo ni moja ya sikukuu za waajemi na siku ya kwanza ya mwaka wa kiajemi. Sikukuu hiyo inaendelea kwa muda wa siku tano.

 Inaaminiwa kuwa "Jemshid  ambaye ni mmoja wa wafalme wa kiajemi  kuwa ni wa kwanza kuisherehekea sikukuu hiyo. 

Na miongoni mwa muonekano ya sherehe hiyo ni kuzuru matembeleo ya kimaumbile, mashamba na bustani  kwa ajili ya  mapokezi  ya kuchomoza  kwa  jua na kuitumia siku ya sherehe kutoka  kuchomoza kwake mpaka kuchwa kwake.  Na wanaleta pamoja nao  vyakula, vinywaji, vifaa vya michezo na burudani  na vyombo vya muziki. VileVile wasichana wanajipanga kwa mapambo ya  duara yaliyotengenezwa kwa maua ya  majira ya vuli na khasa maua ya Yasmini.  

Aidhaa watoto wanalibeba tawi la mtende lililorembwa kwa maua na rangi. Huwa na mazingira ya sherehe zilizojaa uchezaji wa ngoma kwa vikundi juu ya mirindimo ya muziki na nyimbo za sikukuu ya Shamu Nasiim zikiongezea na kufanyika  mechi na sherehe za maigizo. Na sherehe hiyo inaendelea mpaka kuchomoza kwa jua siku inayofuatia.

VileVile  kufanyika sherehe za mapokezi na kupongezana  nyumbani. Au kusherehekea matembeleo na mitaa au kufanyika sherehe za burudani na makongamano ya kienyeji.

Kuna vyakula mbalimbali vinavyoliwa na wanaoisherehekea sikukuu ya Shamu Nasiim  kama vile, mayai yaliyopakwa rangi, samaki waliotiwa chumvi na kukaushwa kwa moshi, vitunguu, majani na chachu ya kijani. Sababu ya kula mayai inarejea katika itikadi ya mafarao kuwa ni alama ya maisha. VileVile fikra ya kuyatia rangi mayai na kuyachora mapambo inarejea katika itikadi yao kwamba njia hiyo itahakikisha matamanio yao na ndoto zao.  

Comments