Thoma aliyependwa na mamilioni ya wananchi katika kipindi cha miaka hamsini ya kazi bora na mafanikio.
Alijulikana kwa sababu ya sauti yake nzuri na historia yake iliyojaa na changamoto kadhaa.Alipania kuchapa kazi hadi mwisho wa umri wake.Amewapa wananchi fani nzuri kabisa.Nyimbo zake zimeitaka nyara mioyo ya waarabu wore mnamo miaka mengi.
Kwa ukweli ingawa Om Kalthom aliaga dunia miaka 40 iliyopita ila fani yake bado ipo.Nyimbo zake zipo akilini mwa mamilioni ya wasikilizaji wake hadi leo.Fani yake kama taa iliyoangaza maisha yetu.
Maisha ya Om Kalthom kwa ufupi.
Jina lake halisi no Fatuma Ebrahim El_Sayed El_Biltaji . Alikuwa na majina ya utani kadhaa kama vile Thoma,Jumuia ya mataifa ya kiarabu,kizeze cha mataifa ya kiarabu,sayari ya mashiriki ya kati na fanani wa umma.
Om Kalthom alizingatiwa kuwa ni moja ya waimbaji mashuhuri wa karne 20 . Alianza maisha yake ya fani utotoni mwake.Alipata umaarufu nchini Misri na nchi za kiarabu.
Alizaliwa tarehe 31 Disemba mwaka 1898 katika kijiji kidogo karibu ya El_Mansoura kinachoitwa Tamay El_Zaharia mkoa wa El_Dakahlaya.Hakuna mtu yeyote anaamini kwamba msichana huyu wa familia masikini aliyeishi katika kijiji bila ya shule hata moja atakuwa mashuhuri sana.Lakini alipata umaarufu utotoni mwake kiasi kwamba baba yake alifanya urafiki na sheikh zakaria Ahmed na Sheikh Aboila Mohamed waliokuja mtaani El_Senbaliwen ili kuandaa sherehe kadhaa mwezi wa Ramadan Mtukufu.Hawa walimshawishi baba ya Om Kalthom kuhama kairo na binti yake.Hii ilikuwa hatua ya kwanza katika maisha yake ya kifani.Wakati huu aliimba katika sherehe ya kuadhamisha kumbukumbu ya El_Esra na El_Marag Katika jumba la "Azz El_Din Yakin" na malipo yake alikuwa pete ya dhahabu na paundi tatu kutoka kwa bibi wa jumba.
Mwaka 1921 Om Kalthom alirejea mara tena mjini kairo ili kuimba na timu ya babake.Alipata fursa ya sauti yake inasikika mjini Kairo na sauti yake ilipata kupendwa na sheikh Ali Mahmoud, sheikh Ali El_Kasabgi na hasa sheikh Aboellah Mohamed alikuwa mwalimu wake na alimsihi kuimba katika nyanja nyingine baadala ya nyimbo za kidini.
Mwaka 1923 Om Kalthom alianza kuimba katika majumba ya wakuu wa Kairo.Baadaye alianza kupata umaarufu zaidi na alishindana na mabingwa wa uimbaji wa wakati huu kama Naima El_Masrry,Monira El_Mahdia,Fatuma Series na Fathia Ahmed.
Mwaka 1924 sheikh Aboellah alimsindikiza Om Kalthom hadi mshairi Ahmed El_Romi aliyechukua jukumu LA l kumfundisha Om Kalthom lugha na ushairi.
Om Kalthom alishiriki katika filamu kwa mara ya kwanza mwaka 1936 kwa anwani ya Widad alikuwa mhusika mkuu na aliimba ndani yake.Baadaye alishiriki Katika filamu tano nyingine. Filamu ya mwisho ilikuwa Fatuma mwaka 1947.Filamu hizo ni Ayda mwaka 1942,Nashid El_Amal mwaka 1937,Salama mwaka 1945 na Dananir mwaka 1947.
Om Kalthom alipata tuzo kadhaa katika maisha yake ya kifani kutoka nchi nyingine kama Lebanon,Misri,Jardan , Iraq,Moroco,Tunisia,Libya,Sudan na Pakistan.
Tarehe 3 mwezi wa Februari mwaka 1975 Thoma aliaga dunia alikuwa na umri Wa miaka 73 baada ya miaka kadhaa ya ugonjwa.Wafuasi wake na mataifa ya kiarabu walifanya mazishi makubwa . Thoma aliacha urithi wa kifani kwa fani ya Misri na ya Kiarabu.
Matembeleo ya Om Kalthom katika mataifa ya kiarabu barani Afrika
Historia itaendelea kuwa ithibati ya mafanikio ya bingwa la uimbaji Om Kalthom.
Kwa ukweli bibi Huyu alikuwa kama mti mwenye matawi mengi . kiasi kwamba aliweza kuwaunganisha waarabu wote.Alikuwa anaipenda sana Misri.Kiasi kwamba alitumia Uimbaji kama nguvu laini Kupita uimbaji aliweza kusanya pesa kwa ajili jeshi ya Misri inunue silaha baada ya vita mwaka 1967.
Mfuatiliaji wa historia ya Om Kalthom hufahamu kwamba maisha yake yameisaidia Misri kwa hali na Mali katika vipindi vyote vya kihistoria kwani alikuwa na uzito wa kisanaa. Maisha yake hakuwa uimbaji tu kwa ukweli alikuwa balozi wa fani ya kiarabu na ya kiafrika .Alifanya matembeleo kadhaa ya uimbaji katika mataifa ya kiarabu kama Sudan,Tunisia,Libya na Morocco ili kusanya pesa kwa ajili ya kuisaidia jeshi ya Misri baada ya vita mwaka 1967.Matembeleo haya ya kihistoria bado ipo katika kumbukumbu ya kiarabu na ya Kiafrika.
Comments