Mwanasyansi mmisri wa anga alipata vyeo vingi huko Marekani kulingana na uhodari wake wa kisyansni , cheo cha muhimu zaidi ni Meneja wa kituo cha utafiti wa agna
Alifanya kazi katika wakala ya NASA kwa kusaidia katika mipango ya uchunguzi wa kijiolojia kwa
mwezi , kama kuchagua mahali pa kushuka
kwa majumbe ya APOLO na kuwafundisha wanaanga wachugue aina zinazofaa kutoka
udongo wa mwezi na kuziletea ardhini ili kuchambua na kuchunguza .
Uzazi na Malezi
Alizaliwa mwaka
1938 , familia yake yenye kiwango cha kawaida katika kijiji cha Tokh EL Aklam mojawapo vijiji vya Seblawin
mkoani Dakahlia .
vyeti vya kielimu
Alipata shahada
ya kwanza ( kemia na Jolojia ) mnamo mwaka 1958 .
Alipata uzamili
katika elimu ya Jiolojia mwaka 1961 kutoka kwa chuo cha Mineralogy Missouri , huko
Marekani.
Alipata uanachama
wa fahari katika chama kimoja cha vyama muhimu ( SIGMA XI ) kwa kutambuliwa kwa
juhudi zake katika nadharia ya Uzamili .
Alipewa cheti cha
Uzamivu mwaka 1964 na alishughulika katika teknolojia ya kiuchumi .
Nafasi alizozipata
Dokta Farouk El-Baz alikuwa meneja wa tafiti za anga katika Boaten , Marekani , na kabla hivyo
alikuwa naibu wa Rais kwa elimu na teknolojia katika shirika la AITEC la vifaa
vya kupiga picha mjini Linkgston , Masachostess .
tangu mwaka 1973
hadi alijiunga na shirika la AITEC mwaka 1982 , Dokta Farouk El Baz alianzisha
na kuongoza kituo cha masomo ya ardhi na sayari katika makumbusho ya kitaifa kwa
hewa na anga katika chuo cha Smethunien , Washington mji mkuu wa Marekani .
alikuwa mshauri
wa kisayansi kwa Rais EL SADAT katikati ya 1978 _ 1981 .
Tangu mwaka 1967 hadi mwaka 1972 , EL Baz
alifanya kazi katika maabara ya BELL , Washington kama msimamizi wa mipango ya
kuchunguza mwezi na kugundua sakafu ya mwezi . na kupitia miaka hii , alishiriki
katika kuthamini mpango wa shirika la ndege kwa anga " NASA " kwa
safari za kitropiki kuelekea mwezi , pamoja na uanachama wake katika vikundi
vya kisayansi vya kufadhili ili kuandaa majukumu ya safari za APOLLO kwenye
sakafu ya mwezi .
Alikuwa katibu wa
kamati ya kuchagua mahali pa meli za APOLLO zinaposhuka kwenye sakafu ya mwezi
.
Alikuwa mkuu wa
timu ya kufundisha wanaanga katika sayansi kwa ujumla na kupiga picha kwa mwezi
hasa .
Alikuwa rais wa
tafiti za majaribio ya binafsi kwa usimamizi wa Ardhi kutoka anga ya nje na kupiga
picha na hiyo katika miradi wa usafiri wa anga ya nje iliyoshirikishwa na APOLLO _ SWAEZR mnamo mwaka 1975
Dokta El Baz
alifundisha sayansi ya jiolojia katika vyuo vikuu vya Asyouti hapa Misri tangu
mwaka 1958 hadi 1960 , vya Mizuri huko
Marekani tangu mwaka 1963 hadi 1964 na Hedleberg huko Ujerumani tangu mwaka
1964 hadi 1965 .
Mnamo mwaka 1966
alifanya kazi ya kugundua mafuta yapo
Khalig El Arabi katika sehemu ya uchimbaji katika kampeni y BAN AMERICAN na
hivyo kabla ya kujiunga na kampeni ya BELL mwaka 1967 .
Mnamo mwaka 1973
alikuwa mkuu wa uchunguzi wa uangalifu wa anga na upigaji picha kwenye mradi wa
Apollo _ soyuz ambao ulifanya misheni ya kwanza ya kimarekani - Kisovieti huko
Tmoz 1975 .
Mwaka 1986
alijiunga chuo kikuu cha Bosten , katika kituo cha kuhisi kwa umbali kwa kutumia teknolojia ya anga ya
nje katika nyanja za jiolojia na jiografia , nidhamu hii iliboreshwa ili
kugundua baadhi za athari za kimisri .
Dokta El-Baz
aliteuliwa kama mwanachama au mjumbe au mkuu wa karibu vituo , mabaraza na
kamati 40 , kama kuteuliwa kama mjumbe wa chuo cha sayansi cha ulimwengu wa tatu TWAS mwaka 1985 , na alikuwa katika baraza lake la ushauri
mwaka 1997 , na mbunge wa baraza la sayansi na teknolojia ya anga ya nje , na
mkuu wa taasisi ya kuhifadhi athari za kimisri , mshiriki katika kituo cha
fizikia ya kimasomo cha kimataifa katika UNESCO , mjumbe wa chuo cha sayansi
cha kiafrika , rafiki ya chuo cha sayansi cha kiislamu huko Pakistan ,
mwanachama mwanzishi katika chuo cha kiarabu kwa sayansi huko Lebnan, na Mkuu
wa Jumuia ya kiarabu kwa tafiti za jangwa.
Maandishi yake muhimu zaidi
Dokta El-Baz
aliandika vitabu 12 , Apollo iko juu ya
mwezi , Jangwa na nchi kavu , vita vya Ghuba na Mazingira , Atlasi ya picha za Sputniki kwa kuwait , na
alishiriki katika baraza la ushauri kwa nyanja nyingi za kisayansi na kimataifa
. Aliandika makala kadha , na mahojiano mengi yalifanyika kuhusu wasifu wake
yanayofikia mahojiano arubaini , kama " Nyota za kimisri ziko angani " " kutoka piramidi
kuelekea mwezi " , " mvulana mkulima yupo juu ya mwezi " , na
kadhalika .
Karatasi za
kisayansi za Dokta El Baz zilizosambazwa ni karibu na 540, ikiwa alifanya peke
yake au kwa ushirikiano na wengine , na alisimamiza shahada kadhaa za Uzamivu .
Tuzo
Alipata tuzo ya
ENMWARI kwa uanzishi wa kitabia kwa ngazi ya kimataifa mnamo 2018 .
Dokta El-Baz
alipata karibu na tuzo 32 nazo ni kama :
Tuzo ya Mafanikio
ya APOLLO , medali bora kwa Sayansi .
Tuzo ya
kufundisha timu ya kazi ya NASA , tuzo ya timu ya sayansi ya mwezi .
Tuzo ya timu ya
kazi katika mpango wa APOLLO ya kimarekani ya Kisovieti.
Tuzo Meriet ya
ngazi ya kwanza kutoka kwa Rais Anwar El Sadat .
Tuzo ya mlango wa
kidhahabu kutoka kwa chuo cha kimataifa huko Bosten, Mwana bora kutoka mkoa wa
Dakahlia , na shule yake ya kimsingi ilipewa jina lake , na yeye alishiriki
katika baraza la waaminifu wa kamati ya jiolojia huko Marekani , kituo cha kimisri kwa masomo ya kiuchumi na baraza la
mahusiano ya kimisri na kimarekani .
Jumuia ya
jiolojia huko Marekani ilianzisha tuzo ya kila mwaka kwa jina lake iliyoitwa
" tuzo ya Farouk El Baz Kwa tafiti za jangwa " .
Mnamo kumi na
moja mwezi wa Septemba 2019 Shirika la anga ya nje ya kimarekani
"NASA" iliitia sayari ndogo jina la Farouk El Baz , sayari ambayo
ilifunguliwa hivi karibuni kwa thamani ya misaada yake muhimu ya kisayansi .
Dokta Farouk ,
alitembelea Mashariki na Magharibi , na alitoa mihadhara katika vituo vingi vya kiutafiti na vyuo vikuu , alipenda safari za kugundua ,
akakusanya sampuli za mawe tangu utoto wake .
Comments