Daktari. Tedros Adhanum Gebriesos

(Mkurugenzi wa Shirika la Afya Ulimwenguni)

Yeye ni mtafiti mtaalam wa sekta ya Afya na mwanadiplomasia mwenye uzoefu mkubwa,Daktari Tedros amezaliwa mnamo 1965 katika jiji la Asmara huko Eritrea,naye alipata shahada ya kwanza katika Sayansi "Biolojia" kutoka Chuo Kikuu cha Asmara, Eritrea mnamo 1986, kisha akapata shahada ya Uzamili katika Sayansi za Kinga kutoka magonjwa ya kuambukiza Kutoka Chuo Kikuu cha London mnamo 1992, na alipata shahada ya Uzamivu katika Falsafa katika sekta ya Afya ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Nottingham cha kiingereza mnamo 2000.


Naye ndiye mkurugenzi mkuu wa kwanza anayechaguliwa na Jumuia ya Afya Ulimwenguni kutoka miongoni mwa wagombea kadhaa, na yeye ndiye mtu wa kwanza kutoka mkoa wa Afrika wa taasisi hiyo anayeshikilia nafasi ya mkurugenzi wa masuala ya kiufundi na kiutawala katika shirika.

Alichaguliwa na Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afya Duniani kama "Mkurugenzi Mkuu wa Shirika" kwa muda wa miaka mitano wakati wa Mkutano wa Jumuia ya Afya Duniani Na sabaini mnamo Mei 2017, na alichukua madaraka mnamo Julai 1, 2017.

Daktari Tedros aliwahi kuwa "Rais wa Baraza la Ushirikiano wa kumalizika Malaria" mnamo kipindi cha (2007-2009), na alishirikiana katika utawala wa "Ushirikiano kwa ajili ya Afya ya mama, wachanga na watoto" mnamo (2005-2009), kisha alichaguliwa kama Rais wa Baraza la Mfuko wa Dunia kwa Kupambana UKIMWI, kifua kikuu na ugonjwa wa Malaria mnamo (2009-2011) pia alichukua madaraka ya kuwa Rais wa Bodi ya Uratibu wa Programu kwa kipindi cha Umoja wa Mataifa cha pamoja juu ya UKIMWI mnamo (2009-2010), na kabla ya kuchaguliwa kama Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi - alikuwa Waziri wa Afya huko Ethiopia mnamo kipindi cha (2005 - 2012), na pia akashikilia nafasi ya Waziri wa Mambo ya nje wa Ethiopia mnamo kipindi cha (2012 – 2016).

Daktari Tedros ana michango kadhaa ya kisayansi na vitendo, ambapo amechapisha makala nyingi katika majarida mashuhuri ya kisayansi, na ameongoza juhudi kamili za kurekebisha mfumo wa afya nchini mwake wakati ambapo alikuwa Waziri wa Afya, ambapo alifanya kazi ya kuboresha huduma za afya kwa mamilioni ya watu, na alipokuwa Waziri wa Mambo ya nje, Aliongoza juhudi za kujadili Mpango wa kazi kwa Adis Ababa ambapo ndani yake nchi 193 zilijitolea kutoa fedha zinazohitajika kwa kufikia malengo ya Maendeleo endelevu.

Daktari Tedros amepokea tuzo na vyeti kwa kutambuliwa kwa shughuli zake kutoka ulimwenguni kote. Pia mnamo mwaka wa 2016, alipewa nishani iliyopambwa na bendera ya Serbia, na mnamo 2011 alipewa tuzo ya Jimy na Rosalynn Carter kwa masuala ya binadamu kwa kutathmini michango yake katika uwanja wa afya ya umma.

Comments