Patrice lumumba Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
yeye ni miongoni mwa wale ambao walioacha athari kubwa katika historia ya sasa ya Afrika, kwani yeye alijitolea maisha yake katika mapambano ya kuwakomboa watu wa Kongo katika harakati za kugombea uhuru kutoka utawala wa kikoloni pamoja na juhudi zake zilizofanyika katika kuanzisha wazo la Umoja wa Mataifa ya Kiafrika na kwa mantika hii alishiriki katika mkutano wa Umoja wa Mataifa ya Kiafrika uliofanyika mjini Accra nchini Ghana mwaka 1958 na alikutana na hayati Kwame Nkrumah.
Na inaelezwa kwamba mkutano huo ulizungumzia kwa kina wazo la Umoja wa Kiafrika katika ufahamu wa Kikongo na uhusiano wake mzuri na viongozi wengine wa kiafrika kama vile Jamal Abdul-Nasir, Ahmad Siku Toure na Kwame Nkrumah. Na mapambano ya Lumumba katika harakati za kugombea uhuru kwa Kongo toka kwa utawala wa kikoloni unaandikwa kwa maji ya dhahabu katika kurasa za historia ya sasa ya Afrika na pia uvutiaji wake ulienea katika nchi yake na nchi za nje na kuenea bara zima la Afrika. Lakini kwa sababu ya uwepo wake katika maeneo yote ya mapambano yenye lengo la uhuru wa nchi yake ulimfanya kukamatwa mara kwa mara na kuwekwa gerezani.
Na kanuni ambazo zilipambanua mapambano yake katika kufanikisha uhuru zilikuwa na sifa ya amani, zisizo na vurugu zenye ujasiri na nguvu ili kufanikisha haki ya kijamii na alikataa uwepo wa ukuloni na uporaji wa mali za nchi za Kiafrika na aliashiria kwamba “vita ambavyo tunavipata kutoka tawala za kikoloni chini visingizio dhaifu na kwa madai ya kupiga vita ukomunisti vinaficha makusudio ya kweli yasiyotangazwa kwani tawala hizo za kikoloni hazina huruma ila kwa wafuasi wao kutoka viongozi wa kiafrika ambao wamewasaliti watu wao. Na hawaleti kwa nchi zetu za Afrika ila uporaji wa mali zetu kwa kula njama na viongozi hao mafisadi”.
Na Patric Lumumba aliuliwa kwa amri ya Wakoloni tarehe 17 Januari mwaka 1971 akiwa na umri wa miaka 53, lakini amebaki kuwa ni kiongozi imara katika historia ya sasa ya Afrika kwa kutambua mapambano yake na misimamo yake ya heshima.
Comments