Balozi wa Misri na Afrika katika kamati ya kiolimpiki ya kimataifa
Aya Madany anazingatiwa Balozi wa spoti ya kimisri katika matukio ya kimataifa na kamati ya kiolimpiki , ambapo yeye ni mwanachama wa kamati ya wachezaji katika kamati ya kiolimpiki ya kimataifa kisha alikuwa mkuu wake pamoja na kuchaguliwa kwake miongoni mwa kamati iliyoundwa na olimpiki ya kimataifa kwa ajili ya usimamizi katika ndondi katika olimpiki ya Tokyo 2021 inayoundwa kutoka wanachama wanne na miongoni mwao ni Aya Madany.
Aya Madany amezaliwa katika siku ya 20 mwezi wa Novemba, 1988 , na alianza njia yake ya kimichezo katika mchezo wa El khomasi ya kisasa , alishinda mashindano ya dunia ya vijana katika miaka ya 2006 ,2008 na alishiriki katika olimpiki ya Athena na alikuwa mchezaji mdogo kabisa katika kamati ya Misri ya olimpiki na alipata jina la mchezaji mmisri wa kwanza wa mchezo wa Elkhomasi ya kisasa aliyefikia olimpiki katika historia ya michezo ya olimpiki
Aya Madany amechaguliwa kama mwakilishi wa bara la Afrika katika kamati za Shirikisho la kimataifa la Elkhomasi ya kisasa ili kuweka mpango na kupitisha mageuzi yanayohitajika ili kuendeleza mchezo huu juu ya kiwango cha duru za olimpiki za watu wazima na za vijana.
Na Madany aliongeza kuwa alihakikisha mashindano ya kimataifa ambayo aghalabu yanamteua kwa baadhi ya kazi muhimu za usimamizi na kazi muhimu kabisa ni uteuzi wake kwa kamati ya kiolimpiki ya kimisri kwa uongozi wa Mhandisi Hesham Hatab , kwa sababu ya imani yake kwake hasa baada ya mafanikio yake ya uwakilishi wenye heshima Kwa Misri.
Na Madany aliongeza kwamba yeye baada ya mwaka mmoja aliweza kuingia katika kamati ya mambo ya wachezaji kisha akawa mkuu wa kamati hiyo , akiashiria kuwa alifanikiwa kuwa mwanachama wa bodi ya wakurugenzi ya shirikisho la kimataifa la Elkhomasi ya kisasa kisha mwanachama wa bodi ya wakurugenzi ya klabu ya jua hadi aliheshimiwa kutoka Rais Abd El Fatah El-Sisi mnamo mwaka wa 2017.
Comments