Mashabiki wa Chesi wanaadhimisha Siku ya kimataifa ya Chesi, mwafaka na Julai 20, kama tarehe hii ilipitishwa kama siku ya ulimwengu ya mchezo kulingana na uamuzi wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Mnamo Desemba 12, 2019. kupitishwa kwa tarehe hii kulikuja kufuatia mpango wa Shirikisho la Kimataifa la Chesi, ambalo linaadhimisha siku hii tangu 1966, ambapo inalingana na tarehe ya kuanzishwa kwa Shirikisho huko Paris mnamo 1924.
Katika hafla hii, Shirikisho la Kimataifa la Chesi mwaka huu lilialika wapenzi na wachezaji wote wa mchezo huo waliotajwa kama "Mchezo wa Wafalme", kwa kumfundisha mtu mmoja sheria za mchezo huo ili kuongeza idadi ya mashabiki. Licha ya kutokuwa na uwezo wa wanahistoria kukubali kusuluhisha mzozo wa nchi ya asili ya Chesi zaidi ya miaka 1500 iliyopita, nadharia zinaonyesha kwamba kumbukumbu ya Chesi ni kati ya India na Uchina, wakati wengine hurejelea kwa wamisri wa zamani, na ushahidi wao kwa hii ni ugunduzi wa moja ya "Chessboard" ndani ya kaburi la Tut Ankh Amoun. Misemo ya kihistoria inaonyesha kwamba "Chesi" imekuwa ikichezwa tangu enzi la Mfalme "Ramses III".
Kwenye maadhimisho ya Siku ya Chesi ya kimisri mwaka huo, Dokta Hisham El-Gendy, Mkuu wa Shirikisho la Mchezo la Misri, alialika vilabu vyote, taaluma, vituo vya vijana, makocha na waandaaji walioshirikiana na Shirikisho la Chesi la Misri, kufundisha angalau mtu mmoja kulingana na matakwa ya Shirikisho la Kimataifa, na kusajili tukio hilo kupitia video au picha, na kutangaza hayo ndani ya siku hiyo .
El Gendy alisema kuwa Shirikisho la Kimataifa la Chesi lililazimishwa kuahirisha Olimpiki - ambayo hufanyika daima baada ya kupita miaka miwili - hadi mwaka ujao, wakati ambapo itakavyofanyika nchini Urusi mwezi ujao. Shirikisho la Misri litashiriki katika mashindano ya majaribio ya Michezo ya Olimpiki "Mkondoni" kesho kutwa, Jumatano, na ushiriki wa nchi 190. Mchezaji Mmisri, Bassem Samir, ndiye anayeshika nafasi ya kwanza katika kiwango cha Waarabu na Afrika, mmoja wa wachezaji muhimu sana kushiriki kwenye mashindano haya, na alionyesha furaha yake kwa ushiriki huo, na akasisitiza kwamba kama mchezaji anayependa mchezo huo, atasherehekea Siku ya Chesi Duniani kupitia Mtandao na uchambuzi au matangazo ya moja ya michezo yake muhimu kando na ushiriki wa binti yake, mwenye miaka miwili, na kumfundisha sheria za Chesi. Shirikisho la Chesi la Kimisri limeandaa mashindano 13 "mkondoni" mnamo kipindi cha miezi mitatu iliyopita, mashindano 8 kwa timu za vijana, na mashindano mengine 5 kwa wasichana, kwa ushiriki wa wachezaji wa kiume na kike zaidi ya 450.
Comments