Historia ya zamani sana na Hazina kubwa ya kazi inayoendelea tangu miaka 60
Kabla ya miaka 60 ,
ilipokuwa matangazo ya kwanza ya televisheni ya kimisri , kusherehekea
kumbukumbu ya nane kwa maandamano ya 23 Julai , saa moja jioni, Julai 21 , 1960
Runinga ya kimisri ambayo hubeba jina la " televisheni ya kiarabu "
ilizindua aya za Quran tukufu ,kisha kuonekana kwa Rais marehemu Gamal Abd El
Nasser wakati wa ufunguzi wa baraza la umma na hotuba aliyeitoa mnamo siku hiyo
na wimbo wa kitaifa ( Nchi yangu kubwa ) .
Matangazo yalifunguliwa kwa mara yake ya kwanza kwa muda wa
masaa matano tu , yalihitimishwa kwa kusoma kwa Quran tukufu baadaye ya redio
ya habari , mwanzoni televisheni ilikuwa kujumuisha kipindi kimoja ,
kilichokuwa kuendelea masaa sita kila siku , kisha masaa yaliongezeka hadi
masaa kumi na tatu kila siku baada ya kuanzisha kipindi kingine cha runinga
mnamo tarehe 21 Julai, 1961 , na imetumiwa kipindi cha tatu mnamo Oktoba 1962
na wastani ya masaa ya matangazo kwenye vipindi vitatu ilikuwa kati ya masaa 25_30 kila siku .
Mwanzo wa kufikiria
Uanzishaji mnamo mwaka wa 1960 haukuwa kwa ghafla , basi
uamuzi huo ulichukuliwa katikati ya miaka ya
hamsini , ila hali za kisiasa na uchokozi wa nchi tatu mwaka 1956 zilisababisha
kuchelewesha kazi ya kuanzisha hadi mwaka 1959 , wakati ambapo Misri ilisaini
mkataba pamoja na shirika la redio la
Marekani"RCA" ili kuongeza mtandao wa runinga ndani ya nchi , uundaji
wa jengo la redio na televisheni ulimaliza mnamo 1960 katika makao makuu yake
ya kisasa katikati ya Kairo huko kornesh El Nile .
Mwaka 1951 ulikuwa jaribio la kwanza la televisheni nichni
Misri , ambapo kampuni ya kiufaransa ya utengenezaji wa redio na televisheni
ilifanya jaribio la kwanza la matangazo ya televisheni huko Kairo , ili kupiga
picha za sherehe zilizofanyika kwa hafla ya harusi ya Mfalme Farouk , kampuni
ilipanga sherehe ya ndani ilihudhuriwa na wanachama ambao wana bahati ya kuweka
vyombo vya upokeaji katika klabu zao .
Mnamo 1954 , Salah
Salem waziri wa mwongozo wa kitaifa wakati huo , alimwambia Rais Gamal Abd El
Nasser jambo la kuanzisha jengo jipya la redio na kituo cha runinga juu ya
mlima wa Mokatam na kilifanyika kwa kweli , na mnamo 1959 uanzishaji wa jengo
la runinga ulianza katika mahali ambapo
lilijengwa hivi sasa , ili kuzindua matangazo yake mwaka 1960 , studio za runinga zilikuwa kuandaliwa na
majaribio ya kwanza katika jukwaa la jumba la Abdin . Mnamo Agosti 13, 1970 amri mpya ya shirikisho la redio na
televisheni ya kimisri (ERTU) iliundwa , na sekta nne zikiundwa : sekta ya
redio , sekta ya runinga , sekta ya uhandisi , sekta ya kufadhili , na kila
sekta ina Rais , na baada ya vita vya 1973
matangazo ya runinga na vifaa vya utangazaji yamebadilishwa , na kuwa
yenye rangi chini ya mpangilio wa "SECAM " , na matangazo ya kimisri
ya runinga yamebadilishwa kutoka kwa mpangilio wa SECAM kuwa BAL mnamo 1992 .
Kuwepo vipindi kadhaa
Mnamo 1973 runinga ya kimisri ilianza opereseheni kubwa
zaidi ili kuboresha vyombo vya matangazo , na mnamo 1978 vipindi viwili vya
kwanza na vya pili viliunganishwa na eneo la Kanah , wakati ambapo kuanzisha
kituo cha runinga kwa vipindi hivyo viwili katika Suez na Ismaalia na Port Saïd
, Mnamo 1988 ilianza matangazo ya runinga kwa kipindi cha tatu kinachotolewa
kwa kanda ya Kairo kubwa , mnamo mwaka huohuo kipindi cha nne kilizinduliwa kwa
kanda ya Kanah "Mfereji wa Suez" .
Mnamo 1990 matangazo ya runinga ya kipindi cha tano kinachowekwa kwa Aleskandaria
yalianza , na mnamo 1994 ilizinduliwa ishara ya matangazo ya majaribio kwa
kituo cha sita kwa katikati ya Delta na makao makuu yake huko Tanta , kinachotolewa
kwa Gharbia , Dakahlia , Monifia , Kafr El Sheikh na Domyat , Mnamo 1994
matangazo ya kipindi cha saba kilianza na makao makuu yake huko Minya na hushughulikia mikoa ya kaskazini
ya Misri ya juu kama Bannysuif , Minya , Fayum na Asyout .
Mnamo 1996 ili kuwa kufunguliwa kituo cha nane na makao
makuu yake ni Aswan na hutolewa kwa ajili ya mikoa ya kusini ya Misri kama
Souhag , Qena , Aswan na Luxor .
Matangazo ya Sputniki
Wakati vituo vya Sputniki na sekta ya Nile kwa vituo maalum
huanza matangazo yake mnamo 1990 , wakati ambapo kipindi cha kimisri cha kwanza
kilikuwa kituo cha satellite cha kiarabu cha serikali cha kwanza kutolewa mnamo
1990 , kituo cha Nile cha kimataifa kilianza mnamo 1994 .
Kituo cha kimisri cha Sputniki cha pili kilianza kama kituo
cha kwanza cha kiarabu kilichokuwa na msimbo na kuingia vyombo vya habari
vinavyolipwa mnamo 1996 , kisha kuonekana kwa sekta ya Nile Kwa vituo maalum
inayojumuisha vituo kadha vya michezo, habari , utamaduni , habari tofauti,
mtoto na vipindi vya mafunzo , baadaye
hujumuisha sinema , vichekesho na burudani ( moja kwa moja ) , na cha mwisho
kituo cha Maspero Zamani kilichokaribishwa sana kwa ubora wake katika
uwasilishaji wa mada za kumbukumbu vya zamani kutoka vipindi , mifululizo na
filamu zenye historia .
Shirika la vyombo vya habari la kitaifa
Maspero ina vipindi vinane vya kitaifa , na vingine kwenye Sputniki , vingine vya redio , pia ina tovuti nyingi
za vyombo vya habari na sekta za kiidara ni tovuti ya vituo vya runinga ya
kimisri , runinga ya Nile , runinga ya Mahrosa , kituo cha habari za Misri ,
sekta ya redio, sekta ya uchumi , sekta ya usalama , na sekta ya uaminifu , na
idadi ya wafanyikazi wake ni wafanyikazi elfu 34 ,pia inafuatiliwa na kampuni
tano nazo ni " Nile sat " , jengo
la uzalishaji wa habari , kampuni na Shirika la Sot El Kahera , kampuni ya CNE
na kampuni ya redio ya Nile iliyoboreshwa .
Mawaziri kumi na tisa walipata nafasi ya waziri wa wizara ya
vyombo vya habari tangu kuanzisha shirikisho la redio na televisheni ,
waziri wa kwanza alikuwa Mohemed Abd El
Kader Hatem , lakini waziri wa mwisho ni Doria Sharf Eldin , wakati ambapo wizara ya vyombo vya habari na
shirikisho la redio na televisheni zimefutwa kulingana na sheria ,namba 92 kwa
mwaka wa 2016 kwa utaratibu wa taasisi kwa vyombo vya habari , na badala ya hivyo shirika la vyombo vya habari
la kitaifa lilikuja linaloongozwa sasa na Hessin Zien .
Vituo vya Idhaa kuu
Maspero inajumuisha karibu na vituo 14 vikuu vya redio navyo ni : redio
ya programu kuu 1934 , redio ya sauti ya Al Arab 1953 , redio ya mashariki ya
kati 1964 , idhaa ya programu ya
kiutamaduni _ programu ya pili hapo awali 1957 , redio ya vijana na michezo 1975
, redio ya muziki , redio ya programu ya Ulaya , redio ya Quran tukufu na redio
ya nyimbo za kimisri _ ya maalum hapo awali 2000 .
Vilevile inajumuisha
redio ya habari na muziki 2000 , redio ya kielimu , redio zilizoelekezwa ,
redio za kikanda , redio ya Misri _ inayofuata sekta ya habari sasa hivi ,
pamoja na vituo vinne vyenye ushirikiano kwa kiasi _ vinavyofuata tovuti za
redio ya Nile navyo ni Mega FM , redio HITS , NAGHAM FM na redio ya umma .
Marais wa shirikisho la redio na televisheni
Marais kumi na wawili wakipata nafasi ya urais wa shirikisho
la redio na televisheni hadi lilipoondoa na kuanzisha shirika la vyombo vya
habari la kitaifa na liliongozwa na Hessin Zien mnamo Oktoba uliopita , nao ni:
1_ Fathy El Bayomi
2_ Amin Basioni
3_ Hassan Hamed
4_ Osama El Sheikh
5_ Samy Abd El Aziz
6_ Tarek El Mahdy
7_ Tharwat Meky
8_ Shokry Abu Emera
9_ Esmael El Sheshtawy
10_ Shokry Abu Emera
11_ Esaam El Amir
12_ Safaa Hegazy
13_ Hessin Zien
Comments