Wengi hukielezea kama lango la Misri kuelekea Afrika, na Watafiti na wahusika wa uwanja wa kiafrika wanakielezea kama "Mwelekeo na Nyumba ya Waafrika wanaohangaika Elimu na Utamaduni kwa utaifa au hata itikadi zao",
Mwaka huu kinaingia mwaka wake wa tatu baada
ya sabini, kilianzishwa mnamo 1947 ,
kinatengwa na kitivo mama kwa karibu
miaka 39, wakati ambapo Chuo Kikuu cha
Kairo kilianzishwa mnamo 1908 . Kwa sasa ni Kitivo cha Mafunzo ya Kiafrika ya
juu - zamani Chuo cha tafiti na Mafunzo ya kiafrika.
Asili ya Kitivo cha Masomo ya Juu ya Kiafrika ilianzia mwaka
1947 , ambapo kilianzishwa chini ya jina la Taasisi ya Mafunzo ya Sudan, ambayo
wakati huo ilihusishwa na Kitivo cha Sanaa, Chuo Kikuu cha Kairo na kilijumuisha
idara mbili tu: Historia na Jiografia. Mnamo 1954 jina la taasisi hiyo
lilibadilika kuwa Taasisi ya tafiti za Kiafrika, basi jina hilo lilibadilika
tena mnamo 1970 na kutolewa kwa Uamuzi wa Jamhuri kwa kuanzisha Taasisi ya
tafiti na Mafunzo ya Afrika, ambapo idara nne mpya ziliongezwa nazo ni: Siasa,
Uchumi, lugha za Kiafrika, Rasilimali asili na Elimu ya Binadamu.
Mnamo Desemba 3, 2018, Waziri Mkuu alitoa uamuzi wa
kubadilisha Chuo cha tafiti na Mafunzo ya Kiafrika na kuwa Kitivo cha
Masomo ya Juu ya kiafrika, na hii ilikuwa
sanjari na matayarisho ya Misri kuchukua Urais wa Umoja wa Afrika na imani ya uongozi wa kisiasa
uliowakilishwa na Rais Mheshimiwa, Abd
El-Fatah El-Sisi wa umuhimu wa jumba hili la zamani la Kiafrika katika
kuboresha na kuimarisha mahusiano ya Misri na Afrika kupitia Elimu, sayansi na
nguvu laini.
Kuna takwimu na dalili zinazothibitisha msimamo wa upainia
kwa jumba la kipekee la Kiafrika.Tukumbuke kutoka kwake kwamba maelfu ya
wanafunzi kutoka Misri na nchi mbali mbali za Kiafrika wamehitimu kutoka kwake,
na miongoni mwao walioshikilia nafasi za juu za uongozi katika nchi zao baada
ya kubeba bango la maarifa kutoka Misri. Kwa mfano, idadi ya wanafunzi
waliojiunga na Kitivo mwaka huu ni takriban 617 tu katika mipango ya masomo
(Diploma maalum - Uzamili - Uzamivu), kwa kuongeza wanafunzi 100 waliojiunga na
diploma za kiufundi, na 593 wameshapata digrii za Uzamili na Uzamivu katika
nyanja tofauti mnamo miaka mitatu iliyopita.
Kitivo hiki ni pamoja na maktaba kubwa ya kipekee iliyo
maalum katika mambo yote ya Kiafrika ambayo ina maelfu ya marejeleo, vitabu,
nakala na mamia ya Tafiti za Uzamili na Uzamivu , wakati ambapo maktaba hiyo
inajumuisha nadharia 1267 za Uzamili na
nadharia 771 za Uzamivu, ikimaanisha kuwa ina nadharia za kisayansi 2038,
pamoja na upitishaji wa nakala 134 za Kiarabu na nakala za kigeni za 117 , na
vitabu na marejeleo takriban 20338 katika taaluma zote na nadharia na kutumika
kwa sayansi ya masomo ya Kiafrika. Kitivo hiki pia kinajumuisha kikundi cha
maprofesa wakubwa na wataalamu katika masuala anuwai ya Kiafrika, maprofesa
hawa wanawasilisha masomo yao na utafiti wa kisayansi ili kuhudumia masuala ya
Kiafrika na kutoa masuluhisho kwa shida zinazozikabili nchi na watu wa bara
hilo. Ikiwa tutafuatilia uzalishaji wa kisayansi wa wanachuoni wa Kitivo wakati
wa miaka mitano iliyopita tu 2015-2020, tutapata kuwa idadi ya utafiti
iliyochapishwa kimataifa na ndani katika mambo anuwai ya Kiafrika
yalifikia tafiti 700 za kimataifa na
ndani.
Kwa kuongezea, Kitivo hicho ni pamoja na mamia ya wanafunzi
waafrika, sawa iwe wanasoma katika idara mbali mbali za Kitivo hicho katika
Diploma, Uzamili, na Uzamivu au
wanafunzi waliosajiliwa na Ofisi ya Masuala ya Wanafunzi waafrika katika Chuo
Kikuu cha Kairo na Chama cha Mawasiliano cha Wanafunzi wa Kiafrika wanaoshiriki katika shughuli zote za Afrika
na vikao vilivyoandaliwa na Kitivo hicho.
Kitivo cha Masomo ya
Kiafrika pia kina jukumu muhimu katika kuelimisha na kuhimiza jamii ya kienyeji
na ya Kiafrika juu ya masuala yote ya
Kiafrika Katika suala hili, Kitivo kilipanga shughuli za bure za masomo na
semina kama (Afrika ni Binadamu na Mahali 1) na (Afrika ni Binadamu , Mahali na
Changamoto 2) na kozi zingine za mafunzo zilizopangwa na ofisi ya utunzaji wa
masuala ya Wanafunzi waafrika, Chuo Kikuu cha Kairo, Kituo cha Habari na
Mashauriano ya Afrika, au Programu ya Kuijenga uwezo na Mafunzo ya Afrika.
Kitivo hicho pia kilifanya shughuli nyingi za kimataifa na
za mitaa, Mipango, mikutano na semina zilizolenga kutafakari shida na masuala
ya Kiafrika na kutoa maoni na
masuluhisho kwao .. Kitivo hiki pia kilipanga mradi wa viongozi 1,000 wa
Kiafrika, ambao uliwasilishwa kwa zaidi ya wanafunzi 5,000 kutoka nchi 35 za
Kiafrika na walipata mafunzo kwa mwaka mzima na wataalam na maprofesa kutoka
Kitivo katika taaluma zote. Kwa kuzingatia mgogoro wa kisasa wa Corona, Kitivo
kilipanga Semina kadhaa za kimataifa za kufahamu maendeleo haya.kiliandaa
semina juu ya virusi vya Corona na athari zake za kiuchumi, lugha ya hotuba ya
vyombo vya habari vya Kiafrika na athari zake katika kuunda maoni ya umma na
kuongeza uhamasishaji wa pamoja kwa kuzingatia janga la Corona.
Kitivo cha Masomo ya Kiafrika - hakika - ni
dirisha la Misri barani Afrika, lango lake kuu kwa bara lake la Afrika,
na kiunga kinachounganisha Misri na ndugu zake wa kiafrika.
Comments