Jiwe la msingi la mji wa zewail kwa sayansi na teknolojia limewekwa mnamo 1 Januari 2000 katika eneo la EL Sheikh Zayd mjini 6 Oktoba .
sherehe ya kuwekewa jiwe la msingi
lilihudhuriwa na Dokta Ahmed Zewail pamoja na waziri mkuu wa zamani sana Dokta Atef Abed , na mawaziri kadhaa mwiongoni mwa ni Ahmed Nazif , aliyeongoza wizara baada ye.
Baada ya
vikwazo vingi wakati wa kuanzisha kwake , mapinduzi ya 25 Januari mwaka wa 2011
yalifanyika kuenezea roho mpya kwa mradi , serikali ya kimisri ilimwuliza Dokta Ahmed Zewail aanzishe baraza
kuu la ushauri na kuzindua upya mpango katika mahali pake pa asili .
mnamo 11 Mei
, 2011 baraza la mawaziri lilitoa uamuzi wa kuanzisha mradi wa kitaifa kwa Ustawi
wa kisayansi , waliuita mradi huo Mji wa Ahmed Zewail kwa Sayansi na teknolojia.
Mji
ulifunguzwa rasmi mnamo 1 Novemba , 2011
kwenye majengo mawili kutoka majengo ya serikali ya kimisri mjini EL Sheikh
Zayd .
sura ya
kisheria ya mji ilikamilika baada ya kutoa kanuni ya 161 mnamo 20 Desemba ,
2012 inayoainisha malengo na vipengele vya mji huo , pamoja na misingi ya kifedha
na kiidara .
mnamo
tisa Aprili, 2014 , Rais wa Msri wa zamani , Adly Mansour , alitoa uamuzi wa jamhuri
namba (115) kwa kuhususisha ekari 198 ili kujenga makao makuu ya mji wa Zewail
katika eneo la Hadayk Oktoba mjini mwa 6 Oktoba .
Rais wa Jamhuri ya Misri ya Kiarabu, Abd El fatah El Sisi , aliliagiza Shirika la
Uhandisi la kijeshi kufanya kazi ya kujenga na kuanzisha mahali mpya kwa mji .
Sasa hivi
chuo kikuu cha sayansi na teknolojia vilevile vyuo vya utafiti mjini mwa Zewail
vinafanya kwa uwezo wao kamili katika mahali pa mji huko El Sheikh Zayed , kwa
njia inavyosambamba na uamuzi wa Waziri
mkuu wa zamani , mhandisi Ebrahim Mehleb , namba (832) , na hiyo mpaka shughuli
za kujenga zitimize . pamoja na hayo , makao makuu ya kiidara ya mjii _ yaliyopo
Eneo la garden city , Kairo, sasa hivi pia yanafanya kazi.
Baada ya
mapinduzi ya 25 Januari na shukrani kwa
nguvu ya utashi wa kitaifa , Misri inaweza kuboresha teknolojia za kitaifa kwa
kiwango cha ulimwengu na kuinua uzalishaji wa kitaifa mnamo kipindi kifupi.
Katika
enzi hii wakati ambapo elimu inapanuka kwa kiasi kikubwa , hatuna la kufanya ila chaguo moja kukuza
mwamko katika nyanja za elimu na utafiti wa kisayansi , kwani ujuzi ni mwanga
ambao utawekwa kwenye maisha yetu ili kutuongoza , kwa hivyo ni muhimu sana kuhakikisha maendeleo na
kuburudisha . mji unapaswa uwe uhamisishaji unaochochea awamu ya mpito kushika
mstari wa mbele wa sayansi za kisasa , ikiwa ipo leo ama kile kinachotrajiwa
wakati ujao .
Karne ya
ishirini ilishuhudia mapinduzi katika sayansi na teknolojia yaliyobadilisha
ulimwengu. Ugunduzi huo na uvumbuzi zilikuja kama matokeo ya kuunda msingi
mkubwa katika utafiti na msingi wa kisayansi, na pia kupitia kazi ngumu ya
wanasayansi katika mazingira mazuri ya kuvutia akili za kipekee.
Kuna
mifano kadhaa nayo ni kama. Laser na Transistor zilikuwa matokeo ya utafiti wa
kimsingi uliokua katika mchanga unaolishwa na udadisi wa kisayansi, na sasa zinashiriki
katika soko la kimataifa la zaidi ya dola trilioni.
Mnamo karne ya ishirini na moja, kumekuwa na
mafanikio ya hali ya juu vile vile, lakini katika viwango vipya, miongoni mwao
kile kiliangazia tena maana ya wakati na umbali.
Katika enzi
ya teknolojia ya habari, uvumbuzi usio
na mipaka, na Genomes, tunaweza sasa kuwasiliana na sayari zingine mnamo
dakika, kudhibiti jambo kwa kiwango cha nanometers na femtoseconds, na hata
kugawanya au kupindua Jeni.
Kuanzia
na ulimwengu mdogo zaidi (sayansi na teknolojia ya Nano), na kupitia sayansi ya
ulimwengu kubwa zaidi , na kwa ulimwengu mgumu (sayansi za maisha), ni kawaida kuibuka
uvumbuzi mpya na jamii zenye msingi wa maarifa zina sehemu kubwa ya uzalishaji
na maendeleo.
Ni hakika
kwamba kile uvumbuzi mpya wa wanasayansi watafanya mnamo karne ya ishirini na
moja na zaidi itakuwa na athari endelevu kwa maisha ya watu katika nyanja
nyingi, hasa zile zinazohusiana na afya na habari (mawasiliano na kompyuta),
nishati na mazingira.
Kwa
kuongezea, kwa kuzingatia umuhimu wa uzalishaji katika kiwango cha kimataifa
cha kuunganisha rasilimali za watu, wateja
na teknolojia, haiwezekani kwa nchi yoyote kuwa na athari halisi kwenye uchumi
wa dunia bila msingi madhubuti wa kisayansi.
Katika
miongo kadhaa ijayo, tutakuwa na changamoto
zaidi, kuanzia kutafutia njia mbadala ya nishati na kufikia kutosheleza kwa
lishe, na kuishia na maendeleo yanayotarajiwa katika akili ya bandia (mashine hodari
zinazowaza) na maswali yaliyotolewa juu ya aina za Jeni au silika.
Sayansi hudumu kuwa msingi ambao tunapima
faida na hatari, na ufunguo unaotupa nafasi mpya za maendeleo. Kwa hivyo, mji
wa Zewail lazima ufanyie kazi kupitia wahitimu wake, vifaa na uwezo tofauti
kutoa nafasi zile.
Pembetatu
ya Misingi
Mpango
mkubwa wa kitaifa kama huo ili kufanikiwa, kuna vyanzo vitatu vya msingi,
kila kimoja kinawakilisha msingi wa mpango.
Upande wa
kwanza wa pembetatu unafafanua mtazamo wa
Chuo. Na Mtazamo huo uiundwa mnamo 1999,
na kisha uliboreshwa kwa lengo la kujenga muundo wa sayansi na teknolojia inayokua
katika kiwango cha ubora wa ulimwengu, wakati huo huo ikihifadhi upekee wake wa
kushughulikia shida ambazo ni muhimu sana kwa eneo hilo.
Upande wa
pili wa pembetatu ni uundaji wa umbo la kisheria. Ilikuwa lazima kwa Baraza la
Mawaziri kutoa maamuzi hayo mawili muhimu ili kubaini hali ya kisheria ya mpango
huo na kuupatia mji kitambulisho chake kama mradi wa kitaifa, pia ilipaswa
kupata msaada wa Baraza Kuu la kijeshi. Sheria Namba 161 ya Mji wa Zewail
iliruhusu jiji kuwa shirika huru, lisilopata faida, na kuliwezesha kuchukua faida
kamili ya maamuzi haya mawili kwa faida ya nchi.
Umbo la
mji
Mji wa
Zewail unaundwa na miundo mitano iliyoshikamana, lakini licha ya ushikamano
wake ila kila moja ina mchango tofauti:
Chuo
Kikuu: kwa elimu ya juu.
Vituo vya
utafiti bora: katika nyanja za utafiti na maendeleo.
Piramidi
ya Teknolojia: kuhamisha teknolojia kwa soko la kimataifa.
Chuo:
Kuandaa wanafunzi wenye vipaji katika awamu
ya kabla ya chuo kikuu.
Kituo cha
Mafunzo ya kimikakati: kwa miradi mikubwa ya kitaifa, kutathmini faida na
hatari husika.
Miundo
hiyo mitano imepangwa kuingiliana kwa njia thabiti, na kusababisha aina bora za
ushirikiano na kufanikiwa kwa faida kubwa zaidi katika ngazi zote za kisayansi
na kifedha. Muundo huo unawapa wanafunzi na watafiti mazingira bora kwao
kujifunza na kuchangia kuunda msingi mpya wa maarifa.
Licha ya
hayo, mji - pamoja na eneo lake kuu
katika mji wa Sheikh Zayed Kairo - haupaswi kuwa kisiwa kilichowekwa mbali kwa ubora wa kisayansi. lakini, unapaswa
kuratibu na kushirikiana na vyuo vikuu na vituo vya utafiti vya kitaifa pamoja
na vile vilivyo katika nchi zingine.
Mji unashirikiana
na taasisi nyingi za utafiti na Mashirika ya utafiti yaliyoko huko pande zote nchini Misri ili kukuza
Uzalishaji wa kitaifa.
Maendeleo
ya eneo jipya
Mnamo
tisa Aprili , 2014, Rais wa zamani wa Misri, Adly Mansour, alitoa Uamuzi wa Jamhuri namba (115) kuhusisha ekari 198 za kujenga makao makuu mapya ya mji
wa Zewail katika eneo la Hadaek Oktoba huko 6 Oktoba.
Rais Abd
El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, ameiagiza Mamlaka ya
Uhandisi wa Vikosi vya jeshi kujenga eneo
jipya la mji huo na kuufungua mnamo
kipindi cha mwaka mmoja.
Sasa hivi
chuo kikuu cha sayansi na teknolojia vilevile vyuo vya utafiti mjini mwa Zewail
vinafanya kwa uwezo wao kamili katika mahali pa mji huko El Sheikh Zayed , kwa
njia inavyosambamba na uamuzi wa Waziri
mkuu wa zamani , mhandisi Ebrahim Mehleb , namba (832) , na hiyo mpaka shughuli
za kujenga zitimize . pamoja na hayo , makao makuu ya kiidara ya mjii _ yaliyopo
Eneo la garden city , Kairo, sasa hivi pia yanafanya kazi.
Na timu
ya wasanifu mashuhuri - chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Mkuu wa
Halmashauri Kuu ya Ushauri - ilifanya
kazi ili eneo hilo linafanikisha maoni
ya mji na ujumbe wake ndani ya muundo unaounganisha sehemu tano za mji. Eneo jipya
la jiji lina sifa ya maendeleo ya kiufundi na kujali mazingira.
Jiji
litatoa huduma na rasilimali muhimu kwa wanafunzi na wanachuoni kupitia vifaa vya kisasa na vya hali ya juu, litakaloimarisha
sura ya Jiji la Zewail kama moja ya taasisi za
kwanza za masomo.
Eneo jipya
litaonyesha pia dhamira ya jiji la kushiriki kikamilifu sayansi ya karne ya 21,
kuinua teknolojia za kitaifa kwa kiwango cha kimataifa, na kuongeza uzalishaji
wa kitaifa. Ubunifu wa Eneo jipya unachanganya mila ya Misri na ya usanifu.
Katika mazingira haya mapya, mfumo wa elimu utajengwa juu ya ujuzi, fikra za
ubunifu, na ushiriki wa watu wote wa jamii ili kuchangia katika kujenga jamii
inayotegemea maarifa.
Eneo lina
mahali panapotumiwa kutoa mwingiliano kati ya wanafunzi, wanachuoni, na jamii. Eneo
jipya limeundwa kupata maonyesho , na
shughuli zingine nyingi. pia katika Eneo
jipya kuna makao ya wanafunzi na wanachuoni yakiundwa kwa kiwango cha juu zaidi, pamoja na
vifaa vya teknolojia ya habari vya kipekee, vifaa tofauti vya masikio na macho,
na vifaa vya ufundi kupitia mitandao isiyo na waya na darasa hodari .
Kituo cha
Mafunzo ya kimikakati
Katika
Mji wa Zewail kituo kimoja cha mafunzo ya kimikakati kitajengwa kwa miradi
mikubwa ya maendeleo na kwa kutathmini hatari za kitaifa na hivyo kama sehemu ya huduma ya kitaifa inayotolewa kwa Mji. Timu
ya wataalam wa ndani na nje watashirikiana katika kuangalia kila kesi kutoa
uchambuzi wa kisayansi kwa kiwango cha juu.
Huduma zitakazotolewa
na kituo hiki ni pamoja na kufanya
tafiti katika elimu nchini Misri, kuondoa
hali ya kutojua kusoma na kuandika, kuanzisha mitandao wa usafirishaji
wa reli katika pande zote nchini Misri, kuboresha sehemu za jangwa, mustakabali ya maji na
vyanzo vya nishati.
Hatari zinazozikabili
nchi na eneo ni nyingi, kwa hivyo inapaswa kufanyika tafiti zinalenga - kwa mfano, kati ya mambo mengine -
kupata nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani, kuzuia athari za majanga ya
nyuklia, mlipuko wa virusi, uhaba wa
maji, kuharibu El Delta, n.k.
Ripoti
hizo zitatayarishwa kwa njia huru na wazi, na kuzipatikana kwa watengenezaji
sera kupitia mikataba ya makubaliano.
Comments