Sophie Sarwat

Ni mmoja wa waanzilishi wa spoti ya wanawake nchini Misri naye alikuwa na fadhili ya kuingiza mchezo wa kuogelea kwa Sikadiani huko Misri mwanzoni mwa miaka ya sitini.

 Sophie Sarwat ameshiriki katika zaidi ya raundi ishrini za kimataifa ili kuonesha mchango wa wasichana wa Misri katika spoti hiyo na kambi za mazoezi zilizofanywa nyumbani mwake kutoka pesa yake mfukoni, hadi Misri imepata nafasi maalumu katika spoti hiyo, ambapo zaidi ya wachezaji elfu kutoka klabu tofauti nane Wameshiriki kwenye mchezo ule katika pande zote za Jamhuri.

 

   Safia Sarwat anayejulikana na jina la "Sophie Sarwat ", amezaliwa tarehe 16, mwezi wa Juli, 1934 mjini Kairo na amejifunza katika shule ya Sant Clear, kisha amejiuna na chuo kikuu cha Marekani ambapo amehetimu kutoka kwake mnamo 1966.

 

   Sophie Sarwat ni mmoja wa waanzilishai wa spoti ya wanawake huko Misri, aliyepata michuano ya kwanza ya kuogelea wakati alikuwa na umri 14, mchuano wa Tenisi, pia ameshiriki pamoja na Esmaiel Al-Shafeay katika kushinda kwa michuano ya wawili tofauti  wa tenisi, vilevile yeye alikuwa mchezaji hodari aliyecheza michezo mingi kama Boga, Shish, mpira wa mkono, mpira wa kikapu na alipata medali nyingi. Baada ya uhitimu wake Sofi amefanya kama mwalimu wa historia na kocha wa kuogelea, na alianzisha timu ya "Bale ya kuogelea" ya kimisri ya kwanza na timu yake imefika michuano ya Afrika na imeshiriki kwenye olimpiki ikiwakilisha Misri, naye alikuwa na mchango mkubwa katika kazi kuu ya kijamii. Sophie, kulingana na Wikipidia, ameigiza kwenye filamu nyingi kama "Kati ya El Atlal ", "mwenye shilingi"( mwenye pesa ndogo), "wasichana na majira ya joto", Safari kuelekea Mwezi na "Mlango wa Chuma".

 

  Mnamo  kipindi cha Tisini, Sophie ameanzisha karatasi ya spoti ya kwanza katika gazeti la "Al-Ahram weekly" na alikuwa mhariri kwenye gazeti hilo. Naye ameaga dunia katika Septemba 2009.

Comments