Mji wa Ras Sidr uko katika upande wa mashariki kwa ghuba ya Suez
katika kaskazini na
kusini mwa eneo la Oyoun Musa, na eneo hilo ni mahali mbalimbali pa kiutalii
kwa utalii wa mazingira(Alcotorizm)na huko unaweza kufanya mazoezi ya Tanga,
kuogelea, kupiga mbizi na safari au
mapumziko ya afya na kujua mahali pa kihistoria na kiutamaduni.
Mji huo
ni wa kwanza katika Sinai kusini kutoka upande wa mashariki, na uko mbali na
mfereji wa Suez karibu na kilomita 60
.mji wa Ras Sidr uko katika ghuba ya Suez, na una ukubwa wa kilomita 6750 za
mraba, na kuna katika mji ule mabonde mengi yenye rutuba kama bonde la Sidr.
Inawezekana
kufikia eneo la Ras Sidr kwa bahari,ardhi na hewa,ambapo kwamba mji huo uko
mbali na mji wa Kairo kilomita 200 kwa ardhi
kupitia handaki ya shahidi Ahmed Hamdy na kwa bahari kupitia bandari za Suez
kama Al-Adabiya, Al-Arish na Al-Tor. Uwanja wa ndege wa kimataifa tayari
umeanzishwa katika eneo hili, na hapo kuna viwanja vitatu vya ndege vya kimataifa
vinasaidia eneo la Ras Sidr,navyo ni
Kairo, Al-Arish na Sharm El-Sheikh.
Mji wa Ras Sidr una maeneo mbalimbali ya
kiutalii kama fukwe zake nzuri kwa urefu wa kilomita 95 na hewa yake nzuri hadi milima ya Serpal au
mlima wa farao unaotoa nafasi kwa
wapenzi wa kutazama ndege, na pale kuna mbuzi wa mlima na ngamia wanaoweza
kutembea katika milima na mabonde.
Na kutoka
mambo muhimu zaidi ya eneo la kiutalii ni mapumziko yake ya afya ya kikibriti
yaliyogunduliwa na Mafarao tangu miaka
5000 na mapumziko yale ni vyoo na macho
ya kawaida ya kibiriti yalifika joto lake hadi 75. Kuna pia mabonde yanayovutia
wapenzi wa safari za jangwa na kuwinda kama bonde la Al-Gherendel, la Tiba na
bonde la Taraki,na mabonde yale yalijazwa,
na mimea, miti ya ajabu na ndege za kware. Mji wa Ras Sidr una vikundi
vitatu vya wabedui ni Oyoun Musa ,bonde la Gherendel na Abu Essaouira, na huko
kuweza kujua mahusika ya kikabila na sanaa za kibedui kama kazi za mikono
zilizopambwa na turquoise ya Sinai, nguo zilizoshonwa na sanaa za muziki za
bedui.
Mji wa
Sinai ukizingatiwa mkutano wa tamaduni, ustaarabu wa kale na ujumbe wa mbinguni
tangu enzi ya Mafarao, nabii Musa, Mkiristo, wagiriki na warumi, na kutoka
mahali mazuri hapo ni Oyoun Musa, choo cha farao na bonde la maktab.
Vijiji
vya kiutalii vilizidi katika mji wa Sinai katika miaka ya mwisho ili kufurahia
fukwe zake nzuri katika maji ya ghuba ya
Suez,na hewa yake nzuri mnamo mwaka mzima,pamoja na utalii wa burudani katika
fukwe za Ras Sidr ,ambapo kuna baadhi ya mahali pa kihistoria ndani yake kama:
Maandishi
ya pango:
maandishi
ya pango yalikuwa makale zaidi kuliko maeneo ya utalii wa kitamaduni yote
katika Sinai, na maandishi haya yanazingatia kujali kwa wamisri kwa madini na
kutuma safari hadi maeneo haya katika bonde la Sidr katika mashariki ya ghuba
ya Suez, lakini baadhi ya maandishi ya pango yaliharibika. Jina la pango
linaitwa sehemu ya bonde la Qunia,ambapo kuna hapo mlima ambao una turquoise
ambayo zilitokwa na wamisri wakale, na bado kuna katika eneo hili mabaki ya
mapango ya wafanyakazi kwenye moja ya majengo yenye urefu, inawezekana
kufuatilia kuta zake lakini maandishi muhimu yaliyokuwepo hapo, hayakuwepo
tena, ambapo kutuma baadhi ya maandishi
haya hadi makumbusho ya Misri mjini Kairo au yaliharibika katika majaribu ya
kutafutia turquoise katika mwanzo wa Karne ya kisasa.
Ngome wa
Al-Gondi:
Ngome hii
iko katika mlima wa kichwa cha Al-Gondi iliofika hadi urefu wa futi 2150 juu ya bahari, na uliongezeka futi 500 juu ya mto mpana juu ya pande zote,
na mlima huu una sura ajabu na mahali pazuri pa sura ya kawaida unaweza kuuona
kwa macho yake kutoka kilomita mbali, na anayesimama juu yake anagundua mbali
zaidi kutoka umbali huu. Kujenga ngome hii kunahusisha na matokeo ya kihistoria
ambapo Salah El-Din na ndugu yake mfalme Al-Adel wameanza kujenga ngome hii
katika mwaka 1183, na wamemaliza katika 1187.
Utaratibu
wa Ngome :
Ngome ya Salah Al-Din iko juu ya mlima wa
El-Gondi, na ngome hii ina sura ya mstatili ilielekea katika pande mbili
kaskazini kwa mashariki na kusini kwa magharibi, na upande wa kusini ulimaliza
kwa sura ya bunduki, mkono wa mgome ni Kati ya
mita 150 hadi 200 kama urefu na upana wake ni mia mita na ukuta nje wa
ngome ni mita mbili, lakini pande zake zilijengwa na nguzo ngumu. Ngome hii
inajumisha ndani yake vyumba vidogo kwa
wanajeshi, na kujenga majengo mengi kwa
vitu mbalimbali kama shimo la upana( mita 50-60 ) kina chake ni mita tano chini
ya ardhi na lilikuwa kama duka la vyakula, na pia msikiti bila paa, na ukuta wake
wa mashariki una kibla kina uaandishi maridadi wa Basmala na paa ya msikiti ni
mita 6-12, kuna pia bomba la maji lilichorwa katika mlima ambapo kuna ndani
yake tanki ya vipimo vya mita 5,5-6-10,
na bado kuta zake ni nzuri na ina mashimo mawili kwa kuingia na kutoka maji.
Comments