Ni ndiye rais wa muda mrefu zaidi kuongoza Al-Ahly kwa muda wa miaka 18
Jaafar Wali Pasha “rais wa klabu ya Al-Ahly” aliyechukua madaraka yake mwaka 1924, ni rais wa muda mrefu zaidi katika utawala wa ngome nyekundu, ambapo ameendelea kuongoza klabu hiyo kwa miaka 18,nao ni muda mrefu zaidi kwa rais yeyote katika historia ya klabu mpaka sasa, akiwashinda marais wengi wa ngome nyekundu kama vile Saleh Selim, Hassan Hamdi, Abdul Mohsen Murtagi na Abdul Saleh Al-Wahsh.
Mwaka wa 1922
ulishuhudia tukio muhimu katika historia ya klabu ya Al-Ahly, ambapo Mahmoud
Mokhtar (au kama anavyojulikana na wote “Mokhtar El Tetsh”,alijiunga na timu,
na alicheza mechi ya kwanza dhidi ya timu ya Anga ya kiingereza kwenye kombe la
sultalni Hussein, Alifunga bao la ushindi katika mechi hiyo iliyomalizika 2-1
kwa Al-Ahly, na Mukhtar El Tetsh baadaye
akawa moja ya hadithi za klabu.
Na mwaka 1922, umeme uliingia klabu ya Al-Ahly kwa mara ya
kwanza, na huo ulikuwa mmoja wa miradi mikubwa ya Klabu, ambapo klabu ilikuwa
na taa na gesi kutoka kuanzishwa hadi kuletwa kwa umeme, na umeme uligharimu
paundi 52, na wanachama wa klabu walisherehekea kwa hilo sherehe kubwa.
Mnamo 1923, Al-Ahly,
ikiongozwa na El-Tetsh, iliingia kwenye michuano ya kwanza katika hazina ya
klabu, iliposhinda Kombe la Sultani Hussein,ikiipiga Zamalek “iliyokuwa
mtawala wakati huo”, halafu iliongeza
majina sita mengine kutoka michuano
hiyo, ikawa mmiliki wa rekodi katika idadi ya ushindi mpaka toleo la mwisho
mwaka 1938.
Mnamo Aprili 1923,timu ilipata kombe kwa mara ya kwanza kwa
kuishinda timu ya Dragons, iliyokuwa na washiriki wa Jeshi la Uingereza, , na
Al-Ahly ilishinda mechi hiyo 1-2 kwa mabao ya Ahmed Mukhtar na Khalil Hosni,
baadaye sherehe za kihistoria ambazo
hazikuwahi kushuhudiwa huko Misri hapo awali zilizinduliwa, na maandamano maarufu yalifanyika kutoka uwanja
wa mechi huko Abbasia hadi makao makuu ya klabu ya Al-Ahly kwenye eneo la Al jazira.
Comments