Mfungaji wa kwanza wa Mafarao kwenye Kombe la Dunia
Nyota wa zamani wa klabu ya Al-Masry, moja wa vipaji vya mpira visivyosahaulika katika historia ya mpira wa Misri.
Abdelrahman Fawzy alizaliwa mnamo Agosti 11,1911, akaanza
kucheza mpira mtaani na barabarani mwa Port Said hadi alijiunga na shule ya
sadaka ya kiislamu, wakati wa masomo yake katika shule ya msingi alifanikwa
kuunda timu inayoitwa Timu ya Nile, na timu hiyo ilikutana na timu kadhaa za
shule za sekondari, kupitia timu hiyo alifanikwa kuunda klabu maarufu inayoitwa
Nile pia, na ada ya usajili katika klabu hiyo ilikuwa 0.05 L.E .
Na baada ya muda
Rasilimali za kifedha za klabu ziliongezka, na mechi zake ndani na nje
ziliongezeka, Abd El Rahman Fawzy alipata umaarufu wake na kuvutia maafisa wa
klabu ya Al-Masry, kwa hivyo alimjumuisha katika safu ya timu ya pili mnamo 1927.
Mshambuliaji mkuu wa kikosi cha kwanza cha Al-Masry hakuwepo
wakati mmoja wa mechi zake dhidi ya timu ya kigeni, kwa hivyo Abd El Rahman
Fawzi aliitwa, aliyefainikwa kuthibitisha kuwepo kwake kufunga mabao mawili
yaliyothibitisha miguu yake katika safu ya kikosi cha kwanza.
Mwishoni mwa miaka ishirini, alijiunga na shule ya Al-Saidia
ya sekondari huko Kairo. Alivuta umakini wa
wote wakati wa mechi za timu ya shule, kuteuliwa na Mustafa Kamel
Mansour, kipa wa Al-Ahly, kujiunga na safu zake, na hakika alicheza pamoja na
Al-Ahly kwa mwaka mzima.
Mwanzoni mwa miaka ya 1930, Abd El Rahman Fawzy aliitikia
mwito wa Hassan Fahmy Bek Refaat , Gavana wa mkoa wa Canal, kurudia safu ya Al-Masry na alirudi na wenzake kadhaa
waliohamia kwa llabu kadhaa za Kairo na Aleskandaria.
Abd El-Rahman Fawzi na wenzake kwenye klabu ya Al-Masry
walishinda michuano ya kwanza katika historia ya klabu ya Al-Masry kwa
kuhakikisha michuano ya Kombe la Sultan Hussein mnamo 1933 kwa kuishinda
Olimpiki kwa mabao mawili kwa bao moja, na mambo haya yalirudishwa mwaka
uliofuata wakati Al-Masry ilifanikiwa kushinda michuano hiyo kwa kufunga mabao
manne dhidi ya klabu ya Al-Ahly
iliyofunga mabao mawili.
Nyota wa timu ya Port Said alichaguliwa kujiunga na safu ya
timu ya kitaifa iliyocheza mechi mbili
dhidi ya Palestina katika raundi za kufikia Kombe la Dunia huko Italia mnamo
1934, mechi ya kwanza ilifanyika huko Kairo mnamo Machi 16,1934, ambapo timu ya Misri ilishinda kwa mabao saba dhidi
ya bao moja. Mechi ambayo Abd El Rahman
Fawzy hakucheza, lakini katika mechi ya marudio , iliyofanyika katika Palestina
mnamo tarehe 16 Aprili 1934, alifanika kufunga bao na mechi ilimalizika kwa
ushindi wa Misri kwa mabao manne dhidi ya bao moja.
Mnamo Mei 1934, timu ilishiriki Kombe la Dunia lililofanyika
nchini Italia, na Abd ElRahman Fawzi alishiriki kwenye mechi ya pekee ya timu
hiyo dhidi ya Hungary, Abd ElRahman alifanikiwa kufunga mabao mawili mfululizo
katika nusu ya kwanza ya mchezo katika mechi hii, nusu iliyomalizika kwa sare
na mabao mawili kwa kila timu, lakini Hungary ilimaliza mechi hiyo katika
kipindi chake cha pili kwa kushinda mabao manne kwa mabao mawili, Abd El Rahman
Fawzi alichaguliwa kama mrengo bora wa kushoto kwenye michuano, na Abd El
Rahman Fawzi atakuwa mchezaji wa kwanza wa Misri, mwarabu na mwafrika kufunga
mabao mawili kwenye Kombe la Dunia.
Baada ya kurudi kutoka Italia, Mohamed Haydar Pasha, Rais wa
klabu ya Zamalek wakati huo, alizidisha shinikizo lake kumjumuisha Abd El
Rahman Fawzi katika safu ya Zamalek, iliyohakikishwa mnamo 1935, na aliendelea
kucheza pamoja na Zamalek hadi 1947.
Baada ya kujiuzulu alielekea mazoezi, ambapo alifundisha
timu ya kitaifa ya Misri, na pia alishiriki katika kufundisha Zamalek na
kugundua wachezaji kadhaa wa kizazi cha hamsini huko Zamalek, kama Alaa
Al-Hamuli, Sherif Al-Far na Issam Bahig, na alikuwa wa kwanza kufikia
Al-Mahalla kwa Ligi Kuu wakati wa katikati ya miaka hamsini, kama alifundisha
timu ya kitaifa ya Saudi, na mnamo 1973, alichukua usimamizi wa kiufundi wa
timu ya Zamalek.
Abdelrahman Fawzy aliendelea na safari ya kutoa kwake kwa
mpira wa miguu wa Misri, hadi alipokufa mnamo tarehe 16 Oktoba 1988 akiwa na
miaka 77, akiacha historia ambayo wote wanahisi fahari kwake.
Comments