Mchezaji mmisri apataye tuzo la kiatu cha dhahabu katika ligi ya Uingereza
"Malkia wa Misri katika klabu ya Stock city"hii imekuwa kichwa cha maudhui ya tovuti ya FIFA,baada ya kufanya mazungumzo na mchezaji wa Soka wa kimisri Sarah Essam,ambaye hucheza katika Uingereza.
Sarah Essam anazingatiwa mchezaji mmisri na mwarabu wa kwanza ameweza kuchezea ligi ya Uingereza kwa wanawake,na ameelekea kucheza huko Stock City, akitoka klabu ya Wadi Degla mnamo wa mwaka 2017.
Na katika siku yake ya kuzaliwa ya 21 tovuti ya FIFA imefanya mazungumzo naye kwa ajili ya kuangalia Ukuaji wake na safari yake katika kucheza Soka hadi kufikia Uingerza.
Sarah ameanza mazungumzo kwa kusema:Nilipokuwa mdogo,nilikuwa kucheza Soka na kakangu,nilikuwa mtoto wa kike wa kipekee aliyecheza na watoto wa kiume,nilipenda Soka hata ingawa nilikuwa mzuri sana katika kucheza mpira wa kikapu,lakini napenda changamoto,kwa hivyo sijasitasita nilichagua kucheza Soka na kuacha michezo mingine yote
Vilevile amesema: nilikabiliwa kwa baadhi ya ukinzani kutoka familia yangu ambayo imeona kucheza Soka hakutakuwa kuzuri kwangu,lakini baada ya kupita wakati nilipata umahari zaidi katika kucheza na wamume hadi nilikuwa mwenye ustadi kuliko wao,imekuwa kitu chenye furaha wakati wa wanaume wamekiri ustadi wangu katika kucheza,hasa ndani ya jamii inayozingatia Soka ni kwa wanaume tu.
Sarah amejiunga timu ya Wadi Degla ili kucheza Soka,na amepanda timu ya kwanza ,halafu amepokea mwito kwa kujiunga timu ya kitaifa ya Misri inayojiandaa kwa mashindano ya kombe la nchi za Afrika 2016,lakini amepata hasira kikubwa kwa sababu ya kutochagua kwake katika orodha ya mwisho ya wachezaji wa mashindano.
Sarah ameendelea:nilihisi kwamba kila kitu kinaenedela vizuri,nilikuwa naenedelea mazoezi yangu kwa kuwa tayari,lakini nilipata hasira kikubwa zaidi nilipojua kwamba sijaingia orodha ya fainali ya timu ya mashindano.
Sara amekata shauri kutokata tamaa na amesafiri na dadake kwa Uingereza mnamo mwaka 2017 ili kutafutia klabu yoyote na kucheza ndani yake na amesema: nilienda kila klabu na kuingia majaribio na klabu kadhaa hadi nilisaini mkataba na Stock city mwaka 2017, katika wakati wangu mzuri zaidi mnamo safari yangu.
Na ameeleza : Nilikuwa najua kwamba itakuwa ngumu, lakini nilikuwa na hamu kubwa ya kisaikolojia na kiakili, nami napaswa kutambua kwamba kuzoea haraka haraka kama hivyo hakutakuwa bila ya misaada ya wenzangu ndani ya timu,nao ni marafiki wa karibu sana tunawasiliana daima ninapokuwa mjini Kairo".
Na kuhusu kuchanganya kati ya kucheza Soka na masomo yake amesema :Nilifanya juhudi kubwa zaidi katika kucheza Soka ,lakini sijaacha masomo katika chuo kikuu,mimi husoma Uhandisi hapa Uingereza, ingwa watu wengi waniambia sitakuwa ngumu kucheza na kusoma lakini nilikata shauri nitakabiliana na shida na nitaendelea kufanya juhudi katika pande zote mbili.
Baada ya kuwa bingwa katika Stock city,amepata tuzo la mchezaji mwarabu bora zaidi kwa mwaka wa 2018,linalofuata shirika la London ya kiarabu,kiasi kwamba amesema: Nina fahari kubwa sana kwa kushindia tuzo,hasa mimi ni mtu mmisri wa kwanza aliyepata tuzo hili,na ustadi wangu umevuta watu na taasisa kadhaa hadi nilishika fursa kutoka BBC ya kutoa maoni katika sherehe ya tuzo kutoka CAF 2018 iliyoshuhudia ushindi wa Mohamed Salah kwa tuzo la mchezaji Mwafrika bora zaidi ,pia nimekuwa miongoni mwa timu iliyo kuzungumzia mechi za kombe la nchi za Afrika nchini Misri 2019.
Na kuhusu kufanana kwa Sara na Mohamed Salah Mchezaji wa Liverpool, Sara amesema: Mimi na Salah tumekwenda Uingereza katika mwaka huu huu,tumesaini na Liverpool na Stock city katika mwezi huu huu.
Na amekamilisha: baada ya taji ya Salah imekuwa mashuri zaidi,mashabiki wa Stock city wameniita"Oh Sarah" malkia mmisri,wamenizingatia toleo la Salah la mke,na hii ni nzuri sana.
Sarah aliyepatia tuzo la mfungaji wa Stock City kwa mwaka 2019 amehitimisha kauli yake akisema: ninatamani nitapata faida kutoka mafanikio haya na majaribio na kuyapeleka kwa wachezaji wa kike nchini Misri,na ninatamni mimi na wenzangu tutaweza kuhakikisha ufanisi wa kushiriki na Misri katika mashindano ya kombe la dunia kwa wanawake,basi kazi kwa kina kwa muda mrefu itatupa Mafanikio.
Comments