Msichana wa dhahabu wa Misri ambaye hubadilisha ndoto yake kuwa kweli
" Kesho siku zitapita, mtakuwa hapa kunisaidia".
Ndoto kutoka kwa Mayar Sherif aliyoshiriki na familia
yake wakati akiangalia moja ya nakala za mashindano ya Tenisi ya Roland Garros.
Mayar alipata rekodi kadhaa katika historia ya Tenisi ya
wanawake wa Misri, kuwa Mmisri wa kwanza kushinda mashindano makubwa "
Grad Slam " na pia Mmisri wa kwanza kufikia raundi kuu katika mashindano
ya Roland Garros.
Mwanzo wa ndoto :
Mayar Sherif amezaliwa mnamo Mei 1996 _ miaka 24 _ na
akaanz safari yake ya Tenisi tangu utoto wake akiwa na umri wa miaka mitano.
Mayar alicheza Tenisi kama dadake mkubwa Rana, na dada
zake Dalia na Rawan, pia hucheza mchezo huo.
Mayar alikuwa ana shauku kubwa sana na mchezo huo na hamu
yake ya kushiriki kitaalam ikawa kama mashujaa unaowaona kwenye Runinga.
" Nakumbuka nilipokuwa na umri wa miaka 13 wakati
niliruka kwa furaha kuona Roger Federer ametwaa taji la mashindano",
alisema Mayar.
" Ninajaribu kufikia mafanikio yatakayodumu kwa
miaka mingi", ameongeza.
Mayar alianza safari yake na mchezo kuelekea kufikia
ndoto zake, polepole taaluma mbalimbali na klabu.
Mayar alifanya vizuri hatua ya wachipukizi na
akafikia viwango vya ulimwengu katika
hatua hiyo, kabla ya kuondoka kwenye mashindano kwa muda.
Kizuizi kipya :
Mayar aliacha kushiriki mashindano ya vijana wachipukizi baada
ya kumaliza shule kabla ya kujiunga na chuo kikuu cha Berden huko California,
Marekani.
Katika kipindi hicho, Mayar alijiunga na timu ya Tenisi
katika chuo kikuu chake na alishiriki kwenye mashindano mengi ya chuo kikuu na
akapata rekodi mashuhuri katika kiwango cha mtu binafsi na maradufu.
Mayar alikuwa akitembelea Misri wakati huo na kushiriki
katika mashindano kadhaa kama yale yaliyofanyika huko Sharm El-Sheikh ili awe
katika Uainishaji wa ulimwengu.
Mnamo 2017, Mayar alimshinda mwenye kiwango cha kwanza
katika mashindano makubwa zaidi ya chuo kikuu katika sehemu ya Magharibi huko
Marekani.
Mnamo 2018, Mayar alimaliza masomo yake ya chuo kikuu na
kuhitimu shahada ya dawa ya michezo, haswa katika majeraha ya Tenisi.
2019 ndio Hatua ya mabadiliko:
Mayar alihitimu kutoka chuo kikuu, kuanza tena hatua za
kugeuza ndoto yake kuwa kweli na kucheza katika kiwango cha taaluma.
Mayar hakuanza katika mashindano makubwa na hakika
ameweza kuwa katika Uainishaji wa Dunia akafikia kati ya wachezaji 300 wa hali
ya juu ulimwenguni.
Mabadiliko makubwa yalikuwa mnamo Agosti wakati
aliposhiriki kwenye michezo ya Afrika
huko Morocco, na Mayar alipata medali ya dhahabu kwenye mashindano kwa viwango
vya mtu binafsi na maradufu.
Mayar alifikia michezo ya olimpiki huko Tokyo kama Mmisri
wa kwanza kushiriki kwenye Olimpiki katika kiwango cha Tenisi, lakini kwa
sharti tu kwamba iliorodheshwa kati ya wachezaji 300 bora ulimwenguni kabla ya
uzinduzi wa mashindano na wakati huo ulikuwa namba 212.
Mayar alijulikana kati ya wafuasi wa Misri baada ya
kufikia Olimpiki, na kila mtu akisubiri atakachowasilisha wakati wa kipindi
kijacho.
Ndoto hiyo iligeuka kuwa ukweli :
Ndoto ya Mayar ilitimiza kupitia ushirikiano katika moja
ya mashindano makuu " Grand Slam " wakati akishiriki mashindano wazi ya Australi Januari jana.
Mayar alicheza mbele ya mmarekani Anne Lee katika duru ya
kwanza katika harakati ya kuandika historia na kutimiza ndoto ya kufikia duru
kuu.
Kama inavyotarajiwa, Mayar aliondolewa kutoka raundi ya
awali, lakini kwa hasara iliyokuwa karibu na seti mbili 3-6 , 5-7 .
Ndoto ya Mayar iligeuka kuwa kweli wakati huo
aliposhiriki mashindano ya Roland Garros, alizungumza na familia yake kwamba
siku moja atakuwa hapa na watakuja kumsaidia kama mabingwa hawa.
Mayar alifikia raundi kuu, akicheza na kicheki Karolina
Pliskova aliyeorodheshwa nafasi ya nne Ulimwenguni na nafasi ya pili kwenye
mashindano, na ilitarajiwa kwamba shujaa wetu wa Misri atapoteza kwa urahisi,
lakini hiyo haikutokea.
Mayar alicheza vizuri mno na akashinda seti ya kwanza 7-6
kabla ya kupoteza kwa 2-6 ya pili na katika seti ya kuamua, Mayar alipoteza
chupuchupu 4-6 kuhitimu msichana wa dhahabu wa Misri akiwa na fahari mbele ya
ulimwengu.
Sifa pana :
Mayar Sherif amesifiwa sana kwa mafanikio yake mazuri
huko Roland Garros ndani na kimataifa.
Hata Pliskova alimsifia
baada ya mechi, " ulikuwa mchezo mgumu sana na nadhani nilicheza
vizuri naye ni mpinzani mgumu sana".
Gazeti la Uingereza, The Guardian, lilisifiwa kwa kile
alichowasilisha wakati wa mechi na akasema, " Mayar Sherif pamoja na
mtindo wake wa kucheza vibao vya mbele, harakati zake nzuri na busara yake
ziliifanya mechi yake ni ngumu sana kwa Pliskova na alikataa kujisalimisha. Tutaona
zaidi kutoka kwake Mayar mnamo miaka ijayo na itakuwa nzuri ikiwa atahimiza
wachezaji zaidi wa Misri na waafrika kumfuatilia.
Kwa habari ya jarida la Ufaransa L'Equipe, ilisema :
" Mayar Sherif, Mmisri alishika namba 172 Ulimwenguni na mchezaji wa
kwanza kutoka nchi yake kushiriki mashindano makubwa ya Tenisi, ilifanya mambo
kuwa magumu kabisa kwa Belskova katika mechi iliyoendelea kwa saa mbili na robo
".
Kuhusu tovuti rasmi ya Shirikisho la tenisi, ilisema :
" Sherif alicheza mechi isiyosahaulika na akamtaabisha Belskova katika
seti ya kwanza, lakini hiyo haitoshi kumkasirisha zaidi mcheki ".
Mafanikio ya Mayar
yamesifiwa kutoka kwa mabingwa wa Misri katika michezo tofauti, mbele yao
Mohammed Salah, nyota wa Liverpool na timu ya kitaifa ya Misri, aliyeonesha
kwenye tovuti ya Instagram maoni yake ya mechi ya kihistoria ya bingwa wa
Misri.
Pia, Nyota wa Boga Ali Faraj na Nour El-Sherbiny, ambao
hapo awali waliongoza kiwango cha ulimwengu, walisifu mafanikio ya Mayar na
kutazama kwao mechi hiyo licha ya ushiriki wao leo kwenye mashindano makubwa ya
Boga ya kimataifa.
Nini baadaye:
Je ! Matamanio ya Mayar yanaacha baada ya mafanikio hayo
? Kwa kweli, hiyo siyo inayotarajiwa na bingwa mmisri au hata wafuasi
walioshikamana na kiwango chake na kupatia mshangao wao.
" Daima nilifuata orodha ya wachezaji 100 bora
ulimwenguni, nilijiuliza ni kwa nini hatukuwa hapa ?", Mayar alisema.
" Natembea hatua kwa hatua kuelekea ndoto zangu na
natamani kufikia orodha hiyo siku moja. ", aliendelea.
Tamaa kubwa ya Mayar sasa ni kuelekea orodha ya wachezaji
100 bora ulimwenguni, Mayar aliyeshika kiwango cha 172 alikuwa na kiwango bora
zaidi Agosti iliyopita alipofika kiwango cha 170.
Tamaa ya pili inayotarajiwa ni ushiriki zaidi wa Mayar
katika mashindano makubwa Grand Slam na kufikia mafanikio zaidi.
kufikia Mayar Sherif
Olimpiki ya Tokyo,halimaanishi tu kupata medali ya Olimpiki, bali
mafanikio zaidi katika mashindano hayo.
Comments