Kisa cha mpira wa mikono wa Misri katika kombe la Dunia

Ni siku 100 hadi kuzindua mashindano ya mpira wa mkono kwa wanaume ya 27 nchini Misri 2021, imekuwa muhimu zaidi kuangalia na kujua visa na historia ya mchezo wa mpira wa mkono.

Ni kitu muhimu kinachobaki katika mchezo wowote ni historia  na katika mashindano ya Dunia ya mpira wa mkono, pengine jambo la muhimu zaidi ni kombe la dunia ambayo timu za kitaifa 32 zinagombeana kwa kuchukuwa kombe na timu moja tu italichukua kombe. 


Lakini, licha ya timu yoyote itakayochukua  kombe la mashindano hayo, bado juu ya kombe hilo kuna mkono mmisri.


Kombe jipya lililoandaliwa na Shirikisho la kimataifa la mchezo limeundwa na msanii  kutoka Ufaransa ametengeneza kombe hilo ni mkono wa mwanamume  mmisri; Kocha Alaa Elsayed Mkurugenzi wa timu za kitaifa katika Shirikisho la Misri kwa mpira wa mkono.


Alaa Elsayed ni miongoni mwa wachezaji wa mpira wa mkono wa kimisri wenye umuhimu mkubwa, vilevile ni mwanachama wa  kamati ya uundaji na mashindano katika Shirikisho la kimataifa la mpira wa mikono, na Mkuu wa kiundi la ukaguzi.


Misri inaandika Historia yake kwa kushika kila upande, kwa kuandaa tukio kubwa wakati wa mlipuko wa Janga kubwa la Corona na kukaribisha kwa mara ya kwanza  timu 31, kwa hivyo mkono wake utapatikana juu ya kombe.


Kwa hivyo timu yoyote itashinda kombe katika mashindano hayo au mashindano yajayo, basi mkono wa kimisri utakuwa daima juu ya kombe.


Comments