Ni bingwa wa dunia wa zamani wa Boga ( skowashi )
Darwish alizaliwa mnamo Agosti 29, 1981, na akaanza kucheza Boga ( skowashi ) katika umri mdogo, ili kufanikiwa kwenye mchezo huo na kuandika jina lake miongoni mwa wakubwa wake.
Karim Darwish alishika nafasi ya juu ya Boga( skowashi ) kwa wanaume mnamo Januari 2009, alihifadhi nafasi yake katika orodha ya kumi bora kwa miaka 12 mfululizo, na kuhifadhi nafasi yake katika orodha ya tano bora kwa miaka minane mfululizo.
Karim Darwish alishinda michuano 25 ya kitaalamu, muhimu Zaidi kati yao ni
michuano ya Saudi, Kuwait, Qatar na Marekani, na pia michuano ya vijana ya
dunia na michuano ya dunia kwa vyuo vikuu.
Kuhusu mwanzo wake na Boga Darwish anasema “mwanzo wangu na
mchezo nilikuwa na umri kwa miaka saba mnamo 1987 kama mchezaji wa karate, na
kaka yangu mkubwa alikuwa kucheza Boga
“nilienda kwa mazoezi naye, na kumwona mara mbili na nilipenda mchezo huo. Nilienda kufanya mazoezi kama majaribio, kocha Mohamed Eid alinipenda na akaamua kuniunga katika shule ya Boga ( skowashi ) kwenye Klabu ya Maadi, hadi sasa naona kuwa yeye na kakangu mkubwa walikuwa na jukumu kubwa katika safari yangu.”
Mara tu nilipocheza Boga ( skowashi ), mchezo ukawa ndani ya damu yangu. Sikuweza kufikiria kuishi bila ya kucheza Boga( skowashi ). Hiyo ilikuwa motisha kubwa kwa familia yangu kunitia moyo kuendelea kucheza mchezo huo, ingawa wakati huo haukuwa na umaarufu mkubwa kama wakati wa kisasa ."
Manmo 2001 Karim Darwish aliingia orodha ya ishrini bora
katika uainishaji, mnamo 2003 alikuwa kati ya 10 bora duniani, kisha mnamo 2004
akafika tano bora duniani na akaendelea miongoni mwa kumi bora hadi kujiuzulu
kwake.
Karim Darwish aliamua kujiuzulu akiwa na umribwa 33 baada ya
safari iliyojaa michuano katika mwaka 2014, lakini haendi mbali na mchezo.
Karim Darwish alioa bingwa wa zamani wa Boga ( skowashi ) Inji Khairallah, na kisha akaelekea kazi ya idara ya Boga ( skowashi ), ambapo anachukua nafasi kwenye sekta ya Boga katika klabu ya Wadi Degla.
Comments