kuzaliwa na ukuaji wake
Tariq Selim alizaliwa katika mtaa wa Dokki mnamo Julai 15,1937 mwana wa Mohammed Selim na kaka mdogo wa Saleh Selim Rais wa kumi wa klabu ya Al-Ahly.
Alijiunga na timu ya mpira wa miguu katika klabu ya Al-Ahly
baada ya aligunduliwa na Hessein Kamel skauti maarufu halafu aliinuka katika
timu za wachipukizi hadi kufikia timu ya kwanza mwaka 1954,kulingana na maagizo
ya kocha Mokhtar Al-Tech.
Safari yake :
Marehemu alishiriki katika mechi yake ya kwanza kwa timu ya
kwanza dhidi ya timu ya Suez kwenye
uwanja wa Suez, na alifunga mabao mawili katika mechi hii, na klabu ya Al-Ahly
ilishinda 4/0.
Na pia alishiriki
katika kuhakikisha mashindano 12 kwa
klabu ya Al-Ahly, miongoni mwao ni
mashindano 7 ya ligi na mashindano matano ya kombe la Misri na pia
ilishinda mashindano mawili na timu ya kitaifa, nayo ni kombe la Mataifa ya
Afrika mwaka 1959, na mashindano ya Jamhuri ya kiarabu mwaka 1961/1962.
Alicheza kwenye
kiwango cha kimataifa kuanzia 1956 hadi 1963 ampabo alishiriki katika
mashindano ya mataifa ya Afrika 1909,na 1963, na ligi ya Roma ya Olimpiki mnamo 1960 na mashindano ya
Mediterania na kombe la Dunia la jeshi.
Alitangaza kustaafu kwake mwaka 1965, baada ya miaka 17 kwa
shati la klabu ya Al-Ahly na kuelekea kufanya Kazi katika idara ya klabu ya
Al-Ahly, halafu alirudia kwa Kazi yake ya asili
Kama mwanahewa , akawa mwanahewa mkubwa wakati wa Kazi yake katika
kampuni ya kitaifa ya usafiri wa Anga.
Katika ugonjwa wake, alikuwa na hamu ya kuwepo katika mazoezi
ya timu ya mpira wa miguu ili kuwasaidia wachezaji katika nyakati ngumu.
Na miongoni mwa misemo yake maarufu ni:
"Niko tayari kufanya Kazi Kama mlinzi kwenye lango la
klabu ya Al-Ahly kwani huduma ya klabu ya Al-Ahly ni heshima kwangu,
Al-Ahly sio klabu ya michezo kwangu, lakini ni nyumba yangu,
na hakuna mtu mmoja anayependa
kutoa siri ya nyumba yake
nje".
Kifo chake :
Tariq Selim alifariki Dunia
Julai 16, 2016 akiwa na umri wa miaka
79 baada ya shida kubwa na ugonjwa, akiacha historia iliyojaa kutoa,
uaminifu na ukweli katika upendo wa
klabu ya Al-Ahly kutuacha mwili wake, lakini kanuni yake na tabia yake zitabaki
milele, ili kujifunza kutoka kwake vizazi wa kisasa na watakaokuja.
Comments