Tarek Yahya

Ni nyota wa zamani sana wa timu ya Al-Zamalek na timu ya taifa ya Misri

Amezaliwa tarehe 10, Septemba, mwaka 1961, bawa la kushoto kwa ngome nyeupe "Al-Zamalek", ametia safari yake katika ligi ya kimisri mnamo umri wa miaka 19 kwa kujiunga kwake kwa timu mojawapo ya timu za Kafr Al-Sheikh ambapo amezaliwa na amecheza mbele ya Al-Zamalek na amechukua nafasi hii kwa kuonesha kiwangi kizuri kabisa.

 

   Pia Yahya amefunga mabao mawili katika wavu wa Al-Zamalek na baadae ameenda kwa ngome nyeupe pamoja na wachezaji wasiozidi umri wa 21 "timu ya vijana", kisha amejiunga kwa tumu ya kwanza na amecheza mechi yake ya kwanza mbele ya Al-Mansoura katika michuano ya kombe la Misri ambapo Al-Zamalek imeshinda kwa mabao manne safi.

 

   Mechi ya Al-Zamalek mbele ya Isko katika 1982 inazingatiwa mechi yake maarufu zaidi pamoja na Al-Zamalek ambapo Al-Zamalek imeshinda kwa mabao sita, miongoni mwaoYahya amefunga mabao matatu. Vilevile amejulikana kwa uhodari wake mbele ya Al-Ahly, ambapo amefunya nyavu za Al-Ahly katika mechi iliyoishia  sare  chanya kwa mabao mawili kwa kila timu, naye aliyepoteza furaha ya Al-Ahly baada ya kuhakikisha ushindi mnamo Ramadhani dhidi ya Al-Ahly baada ya siku fulani kutoka ushindi wake kwa ligi.

 

   Pia ameshinda  michuano ya ligi katika miaka ya 1984, 1988, 1992 na kombe la Afrika katika 1984 na 1986. Vilevile, amefunga bao la ushindi ndani ya nyavu za  Al-Itahad kwenye fainali ya kombe la Misri mwaka 1988, na kwenye mwaka huu huu, Al-Zamalek imeshinda michuano ya "Afro asian".

 

   Pia ameshiriki katika kupata kwa timu ya taifa ya Misrikwa kombe la mataifa ya Afrika katika 1986 mjini Kairo, na alikuwa mfungaji wa pili kwa kiasi cha magoli 67, miongoni mwake ni magoli 51 katika michuano ya ligi, naye ameshika kiwango cha nane kwenye orodha ya wafungaji wa timu katika michuano ya ligi. Pia amefunga magoli sita katika kombe la Misri na amefunga magoli kumi katika michuano ya kiafrika.

 

   Naye amefanya kazi kama kocha msaidizi pamoja na timu za Al-Kanaa, Al-Sharkia na Al-Zamalek kutoka mwaka wa 1999 mpaka 2003 kisha akawa Meneja kwa kwa timu kama Nabaroh, Tanta na Al-Masria Etisalat kutoka mwaka wa 2003 hadi 2008 na baadae akawa kocha msaidizi kwenye timu ya Al-Zamalek mwaka wa 2008.

 

   Vilevile amefanya kazi kama Meneja wa timu za Asmant Al-Suez, Al-Intag Al-Harbi naMasr Al-Makassa kutoma 2008 hadi 2012, na amechukua uongozi wa timu ya Hagr Al-Saudi katika 2012, Masr Al-Makassa 2013, Al-Masri, Talae Al-Geish  Al-Sharkiya, Betrouget, na Smouha, pia akawa Meneja wa Al-Zamalek kwa kipindi cha muda mdogo kabla ya "Mecho" wa Serbia  amechukua uongozi wa ngome nyeupe.

Comments