Uwanja wa uzalishaji wa kivita au "uwanja wa salaam"
nao ni uwanja wenye matumizi mbali mbali. Uwanja huu uko mjini AL- Salaam, Kairo, Misri. Na kwa upande wa magharibi unapakana na barabara ya Bilbisi Jangwani. Na kwa upande wa mashariki unapakana na makaazi ya eneo la AL-Nahda. Na kwa upande wa kusini unapakana na njia ya AL-Nahda au "njia ya shule". Uwanja huo unajumuisha zaidi ya mashabiki 25,000. Umeanzishwa mwaka 2009 kwa ajili ya kuikaribisha michuano ya kundi la pili la kombe la dunia la vijana mwaka 2009.
VileVile ulikuwa ukitumika kwa ajili ya mechi za soka.Umebahatika kupendwa kwa timu zote na waandaaji wa shirikisho la kimataifa la mpira wa miguu (FIFA).
Milango mikuu ya uwanja
Mlango wa kwanza :unapatikana barabara ya Bilbis Jangwani. Unatumika kwa ajili ya kuingia na kutoka VVIP+VIP, mabasi, waamuzi na kamati zinazoandaa.
Mlango wa Nne : unapatikana kusini mwa uwanja huo kwenye njia ya AL-Nahda. Unatumika kwa ajili ya kuingia na kutoka kwa mashabiki wa daraja la kwanza, kamati za uandaaji za kitaifa na watumiaji wa vyumba vya Sky box.
Mlango wa Tano ":mlango huu unatumika kwa ajili ya kuingia mashabiki wa timu wakati wa michuano ya ligi kuu. VileVile unatumika kwa ajili ya kuingia na kutoka kwa mashabiki wa daraja la pili na la tatu wakati wa michuano ya kombe la dunia.
Mlango wa Sita : unapatikana kaskazini mashariki mwa uwanja. Unatumika kwa ajili ya kuingia na kutoka kwa mashabiki wa daraja la pili.
Mlango wa Saba:mlango huu unazingatiwa kuwa ni mlango mkuu. Unapatikana barabara ya Bilbis Jangwani. Unatumika kwa ajili ya kuingia na kutoka kwa mashabiki wa daraja la tatu .
Sehemu ya kutua ndege
Uwanja huo unapambanulika kwa kuwepo sehemu ya kutua ndege inayotumika kwa ajili ya kumkaribisha raisi na wageni wake wakubwa. VileVile inatumika katika kasi ya kuwasafirisha wagonjwa
Maeneo makuu ya uwanja
Eneo la Rais "VVIP".
Eneo la maafisa.
Eneo la mashabiki wa daraja la kwanza.
Eneo la waandishi wa habari.
Eneo la kamati zinazoandaa.
Eneo la Sky box.
Eneo la wachezaji na waamuzi.
Eneo la huduma ya kwanza na upimaji wa madawa ya kuongeza nguvu mwilini.
Eneo la Rais "VVIP".
Eneo la mapokezi ya Rais.
Eneo la maafisa "VIP".
Majukwaa
Majukwaa haya yanajumuisha viti 24034. Na yamebuniwa kwa umbile la yai kwenye pindo dogo katika sehemu ya mkato linampa kila mtazamaji muono mzuri.
Vyumba vya waliokwama
Uwanja huo unajumuisha vyumba 10 vinavyohusiana na waliokwama. Vyumba hivi vinajumuisha mahitaji yote ya waandishi wa habari.
Comments