Msikiti wa kwanza kujengwa barani Afrika.
Ulijengwa mjini Fustat, ulioanzishwa na Waislamu huko Misri baada ya ufunguzi. Iliitwa pia Msikiti wa Fath, Msikiti wa Kale na Taj Al-Jwama. Msikiti wa Amr Ibn Al-Aas iko upande wa mashariki wa Nile urefu wa 31 31 59 Mashariki, na kwa latitude 30 0 37 kaskazini.
Ilikuwa markazi ya serikali na kiini cha wito wa dini ya Kiislamu huko Misri, Amr ibn al-Aass alijenga mskiti hiyo katika 20 H, sawa na 641 AD,kisha kujengwa jiji la Fustat, ambalo ni mji mkuu ya kwanza wa Misri, Amr ibn al-Aas alipochagua msimamo wa msikiti kukielekea juu ya Mto wa Nile, na ngome ya Babiloni .
Eneo la msikiti wakati wa ujenzi lilikuwa ; upana dhiraa 50 na urefu dhiraa 30 na lilikuwa na milango sita, ilisalia hivyo mpaka 53 H / 672 AD ambapo kupanua na kuongezeka eneo lake na Musallam bin Mukhalid Al Ansari na mkuu wa Misri na kujenga minara minne, kisha kuendelea na marekebisho na kupanua mikono ya wale waliomtawala Misri mpaka lilipofika eneo lake ni karibu ishirini na nne dhiraa ya usanifu. Sasa eneo lake ni ; upana mita 120 na urefu mita 110.
Na kutumia matofali ya kujenga kuta za msikiti hakuwa na rangi, bua ya mitende yalitumiwa kwa nguzo na wamba kwa paa, msikiti una milango kadhaa, lakini hakuna mlango katika ukuta wa Qibla, Msikiti wa Amr ibn al-Aas uliojengwa kwa mtindo wa Msikiti wa Mtume Muhammad (S.W.A ) huko Madina kabla ya marekebisho yaliyofanyika; ; ambapo msikiti ulionyesha maadili ya Kiislam bila udohoudoho au uharibifu, lengo la ujenzi wake kulikuwa na nafasi ya kulinda wanaoSali kutoka mambo mbalimbali kama hali ya hewa. Mambo muhimu zaidi yaliyotendeka kwenye msikiti wa Amr ibn al-Aass utendaji wa wajibu wa kidini. Inashikiliwa na halmashauri za mahakama, bodi za hadithi. Ilifanyika vipindi vya elimu, ambavyo vilifikia idadi vyao katika karne ya nne AH (karne ya kumi) vipindi mia moja na kumi , na imeweka baadhi ya vipindi hivi kwa wanawake ,Na kuweka mabaraza haya na mhubiri wa wakati wake Um EL-Khair El- Hijaziyah. Wakati wa vita dhidi ya nchi za Kiislamu kutoka kampeni ya wafuasi wa salibi, hasa katika 564 H .Waziri Shawar aliogopa kampeni ya wafuasi wa salibi dhidi ya mji wa Fustat, aliiweka moto kwani hakuwa na uwezo wa kulinda na kuchomwa mji na kuharibu Msikiti wa Amr ibn al-Aass. Wakati Salah El-Diin alipounganisha Misri na nchi yake, aliamuru kujenga msikiti tena katika 568 H, na msikiti ulijengwa tena na mihrab kubwa, iliyopambwa kwa gololi na kuchonga na miongoni mwa epigrafu Haya ya jina lake (Salah El-Diin ). Mambo haya yalifanya Msikiti wa Amr ibn al-Aass chuo kikuu cha sayansi ya kale kabisa katika Misri ya Kiislamu, ambayo tayari ni Al-Azhar miaka 600 iliyopita.
Comments