Nyumba ya Opera ya Misri, au tasisi Kuu ya Kituo cha Utamaduni cha Taifa, Opera ya kwanza katika Mashariki ya Kati na bara la Afrika
ilizinduliwa katika mwaka 1988. Iko katika jengo lake jipya, ambalo lilijengwa kama hazina ruzuku kutoka serikali ya Kijapani kwa mwenzake wa Misri katika eneo la kisiwa hi huko Kairo , Nyumba ilijengwa katika mtindo wa Kiislamu.
Nyumba kubwa ya kitamaduni iliyofunguliwa mnamo Oktoba 10, 1988, ni mbadala kwa Nyumba ya Opera ya Khediwe iliyojengwa na Khedive Ismail mwaka wa 1869 na kuchomwa moto tarehe 28 Oktoba 1971 baada ya kuwa na mnara la kitamaduni kwa miaka 102.
Tareeh ya ujenzi wa nyumba ya kale ya opera inarejea kipindi cha mafanikio yaliyoshuhudiwa na Khedive Ismail katika nyanja zote. Khedive Ismail aliamuru ujenzi wa Nyumba ya Opera ya Khedive katika Mtaa ya Azbekiya huko kati kati ya mji Kairo katika mnasaba wa ufunguzi wa Mfereji wa Suez , ambapo aliamua kuuitia idadi kubwa ya wafalme wa Ulaya. Opera ilijengwa katika miezi sita tu , ambapo wahandisi wawili wa Italia Avoscan na Ross waliweka ramani yake. Khedive Ismael alitaka kuwa opera ya Misri ishuhudi ufunguzi wa Nyumba ya Opera ya Khedive, ni opera ya Aida .Muziki wake uliwekwa na mwanamuziki wa Kiitaliano Verdi ,Lakini mazingira yaliwazuia kuutolewa kwenye ufunguzi wa sherehe, basi Opera ya Rigoletto ilitangulia wakati wa ufunguzi rasmi , ambao ulihudhuriwa na Khedive Ismail, malikia Eugenie, mke wa Napoleon III, Mfalme wa Austria na mwana wa mfalme wa Prussia.
Nyumba ya Opera ya Khedive, iliyochomwa asubuhi mnamo Oktoba 28, 1971, Inaweza kubeba hadi watu 850, kuna mahali mahsusi kwa watu muhimu sana (VIP) Nyumba hiyo ilikuwa na utukufu ya kifahari.
ujenzi
taasisi la Ushirikiano wa Kimataifa la Kijapani (JICA) liratibitisha na Wizara ya Utamaduni wa Misri huko Kairo, zilikubaliwa kuwa ramani itafanana na majengo yaliyo kariburamani ilikuwa na sifa za ramani za kisasa za Kiislamu .
Eneo la ujenzi linajumuisha mita za mraba 22,772, wakati jengo yenyewe iko kwenye eneo la mita za mraba 13855, na urefu wa juu wa mita 42.
Katika mwezi wa Machi 1985, ramani iliyochukua mwaka na nusu ilikamilika na fadhili ilikuwa kwa juhudi za mikono ya Misri kwa kushirikiana na kampuni ya Kajima kwa ajili ya kukamilika Mjengo mkubwa katika siku 31 Machi, 1988, baada ya miezi 34 tangu mwanzo wa kazi ili kuwa alama za karibuni za kitamaduni za Kairo.
Mnamo Oktoba 1988, nyumba hiyo ilifunguliwa mbele ya Rais wa zamani Hosni Mubarak, Na Amiri Tomohito Auf Mikasa, ndugu mdogo wa Mfalme wa Japani . Japani pia walishiriki kwa mara ya kwanza katika Misri, ulimwengu wa Kiarabu na Afrika katika ufunguzi wa jengo hili la kitamaduni , kwa Utendaji wa bendi ya Kabuki, ambayo inajumuisha wanachama hamsini, Pamoja na wasanii wa cheo cha juu katika uwanja wa muziki, opera na bale. hivyo jengo hili kubwa lilipatikana tena.ili Misri iwe nchi ya kwanza katika eneo kujenga nyumba ya opera mara mbili katika muongo mmoja.
Opera ya sasa ina maonyesho 3: kubwalina viti 1200 , ndogo lina viti 500, wazi lina viti 600, opera hiyo ilikuwa na jukumu muhimu sana katika kuimarisha harakati ya sanaa katika Misri. Ambapo inajumuisha:
Bendi la bale la kairo , simfoni, bendi ya Taifa ya Muziki wa Kiarabu na timu ya ngoma ya kisasa ya ukumbusho .
Opera hutoa saluni za kitamaduni, maonyesho ya sanaa na sherehe ya muziki.Jumatano, Aprili 25, sherehe ya kwanza ya Opera ya Misri ilifanyika katika Kituo cha Utamaduni cha mfalme Fahad huko Riyad chini ya ulilinzi wa Waziri wa Utamaduni wa Saudi na Misri .
Matawi ya Nyumba ya Opera :
Nyumba ya Opera ya Alexandria.
Nyumba ya Opera ya Damanhour.
Nyumba ya Opera ya Luxor.
Nyumba ya Opera ya Mansoura
Comments