Eneo la kijiografia
Mji wa Ismailia unazingatiwa kuwa ni miongoni mwa miji ya mfereji. Nao ni mji mkuu wa mkoa wa Ismailia. Idadi ya wakaazi wa miji na mitaa yake inakadiriwa kwa watu milioni. Mji huu umejengwa kwenye ukanda wa magharibi wa ziwa la mamba ambao unazingatiwa kuwa ni moja ya sehemu za mhimili wa mfereji wa Suweiz ili uwe kituo cha mamlaka ya mfereji wa Suweiz mnamo zama ya sultani Ismail.
Baada ya ongezeko la wakaazi katika nyakati za hivi karibuni, mji ule umeyashuhudia mabadiliko kadhaa miongoni mwayo; kuanzisha barabara ya chini ya ardhi ya Jamal Abdi EL-Naasir katika kituo cha mji , ukiongezea na "MJI WA EL-MUSTAKBAL" ili kukidhi ongezeko la wakaazi na mji huu upo barabara ya kairo ya Ismailia jangwani. VileVile mkoa huo ulianza kufanya upya na kujenga madaraja mapya juu ya mfereji wa Ismailia. Aidhaa mkoa huo unapambanuka kwa bustani nyingi na matembeleo ya kimaumbile.
Historia kwa ufupi
Uanzishaji wa mji huo unarejea katika zama za kabla ya familia. Mitume, Ibrahim, Yussf, Yakobo na Musa walipita katika ardhi yake. Ulipata heshima kubwa ya kutembelewa na familia takatifu. Uislamu uliingia humo ukiambatana na ufunguzi wa kiarabu chini ya uongozi wa Amru bin Aasiy. Ulianzishwa rasmi katika zama ya Said Pasha tarehe 27 Aprili 1862. Kila mwaka, unasherehekea sikukuu yake ya kitaifa tarehe 25 Januari kuendeleza kumbukumbu ya ari ya majeshi yake dhidi ya majeshi ya kiingereza mwaka 1952.
Matembeleo ya kimaumbile na ya kiutalii
Mji huo unatoka katika kingo mbili za mfereji wa Suweiz na maziwa yenye maji chumvi Pamoja na ziwa la mamba. Kwa kuangalia hali yake ya hewa ya wastani kwa muda wa mwaka mzima , licha ya kuwa ni karibu na mikoa ya kairo, Kaliyubiyah na Sharkiyah unayatumia maeneo ya mapumziko ya majira ya joto na ya baridi.
VileVile una makusudio mengi ya kiutalii ya kihistoria yanatuhisisha utukufu wa ustaarabu wa kimisri pamoja na yanatukumbusha shindi zilizo tukuka. VileVile alama zake za kihistoria zinazoonekana kama mchoro mzuri wa uzuri unaotoa fursa kwa watalii kuyaishi pamoja na safari ya kihistoria katika ardhi yake. Na miongoni mwa matembeleo haya ni :-
Makaburi ya Commonwealth
Makaburi haya yanaenea sana katika maeneo mbali mbali nchini Misri. VileVile yanawavutia watalii wengi wanaokuja ili kutembelea jamaa zao.
Kumbusho la mabaki ya kale
Linazingatiwa kuwa ni miongoni mwa makumbusho ya kale zaidi yaliyojengwa na wahandisi waliofanya kazi katika mamlaka ya mfereji wa Suweiz mwaka 1911.
Kumbusho la DELSEBS
Uanzishaji wake unarejea katika kipindi cha uchimbaji wa mfereji wa Suweiz mwaka 1859. Lilikuwa makazi ya kuishi mhandisi wa kifaransa Ferdinad Delesebs. VileVile linajumuisha vyombo vyake na viambata vyake vya michoro ya kiuhandisi.
Kumbusho la polisi
Linapatikana usimamizi wa usalama wa Ismailia. Linajumuisha silaha mbali mbali zilizotumiwa na majeshi ya kimisri ili kupiga vita majeshi ya kiingereza katika mwezi wa Januari 1952.
Mlima wa KAFRYA na AI-SAIDI
Upo kijijini Abu Khalifa. Na kijiji hiki kinazingatiwa kuwa ni miongoni mwa maeneo ya kizamani muhimu sana yanayorejea katika zama ya kiyunani na ya kirumi.
Mlima wa EL-SAHABA na EL-AZBA
Upo kusini mwa Abu Suir umbali wa takribani kilomita mbili. Unajumuisha mabaki ya kale yanarejea katika zama ya kiyunani na ya kirumi.
Mlima wa ABU SAIFI
Unapatikana umbali wa takribani kilomita tano kutoka mashariki mwa Qantara. Unajumuisha vipande vitatu vya mabaki ya kale vinarejea katika zama ya kiyunani na ya kirumi.
Mlima wa EL-HABR
Upo umbali wa takribani kilomita 75 kutoka mashariki mwa Qantara. Unajumuisha ngome tatu za kizamani zinarejea katika zama za mwisho za kifarao na wabatalima na waromani.
Comments