Hany Azer

Amehotop wa Misri

 Mhandisi mmisri aliyebeba ndoto na matumaini yake toka Tanta kisha aliyaweka katika safari yake kuelekea Ujerumani: ili kujiweka nafsi yake katika Jukwaa la kimataifa, kama mhandisi mmoja mzuri wa Wahandisi wa Handaki ulimwenguni, na jina la Hany Azer lilikuwa kama alama maarufu sana katika sekta ya Handaki, kabla ya kupata lakabu ya Amehotop wa Mafarao toka wazungu.


 Na  Leo , Mjuzi  wa kimataifa wa sekta ya Handaki Hany Azer anasherehekea kwa kipindi kipya cha mafanikio yake, baada ya uamuzi wa serikali ya kijerumani kumpeleka Nishani ya Ubora ya cheo cha kwanza kumheshima kwa mafanikio yake yaliyofanyikwa huko Ujerumani, kwa kuwepo Balozi Nabila Makram Abd Elshaheed " Waziri wa nchi kwa Uhamiaji na masuala ya wamisri" kwa washiriki katika sherehe ya kuheshima. 


  katika mistari ifuatayo taarifa muhimu zinazohusu mjuzi wa kimataifa wa Handaki Mhandisi Hany Azer: 


 Jina lake : Hany Helmy Azer.  amezaliwa katika mwaka wa 1948 huko Tanta naye ana miaka 71 , alipata kiasi cha 87.5% katika shule ya Sekondari , alihitimu masomo yake toka Kitivo cha Uhandisi Chuo Kikuu cha Ain Shams mwaka wa 1973. aliathiri sana kwa mhusika wa Baba Shenuda " Baba wa Aleskandaria na Askofu wa Kundi la Kimorkosi' " aliyeaga dunia" wakati ambapo alikuwa Askofu .  alisafiri kwa mji wa " POKHOM' huko Ujerumani baada ya Hitimo yake ili kujifunza Uhandisi.  


 alifanya kazi kama Muuzaji wa Magazeti huko Ujerumani. na "Mngoja " ili kuweza kuishi mnamo kipindi cha Elimu yake , alisimamia kujenga kituo cha Treni za Berlin.                                                                                                                  alichangia katika kuunda Handaki ya Reli za chini ya Ardhi  " Dorotomond" mwaka wa 1979.


katika mwaka wa 1994 aliongoza kundi la kujenga Handaki ya " Tergarten" chini ya Berlin.


 Wajerumani wanamwita kwa jina la " Amehotop wa Mafarao .


alikuwa Mhandisi mkubwa zaidi kwa kituo kikubwa zaidi cha Treni huko Ulaya ' Lerter Banhoof" huko Berlin.   


 alichaguliwa miongoni mwa wahusika 50 maarufu zaidi nchini Ujerumani, baaya ya ujenzi wake kwa kituo cha Reli za chini ya Ardhi Berlin mwaka wa 2006, kilichopata wakati huo tuzo la " Kituo cha Dunia "  .  


alishiriki katika makumi ya miradi huko Ujerumani , na jina lake lilihusiana kwa Handaki kadhaa na miradi kuzunguka Ulimwengu, na alikuwa Mtaalamu maarufu zaidi wa Handaki ulimwenguni.


alipata Nishani ya Jamhuri  ya kijerumani, kutokana na Mshauri mjerumani Anjela Merkel mnamo 26 toka mwezi wa 5 mwaka wa 2006, wakati wa Ufunguzi wa kituo cha Berlin kwa Treni kwa juhudi zake na kuhudumia mchi ya kijerumani.


Rais aliyepita Hosny Mubark alimheshima nchini Misri katika tarehe ya kwanza mwezi wa 10 mwaka wa 2006.


 alichaguliwa mwanachama wa Baraza la Wataalamu wa Misri, na Rais Abd Elfatah Elsisi alimpa jukumu la kufuatia Miradi inayofanyika nchini Misri  khasa Mradi wa kitaifa kwa Mabarabara.  


 Rais Mheshemiwa kwa Taasisi ya " Misri inaweza".

Comments