Kiongozi wa Mapinduzi
"Miongoni mwa tuliyoyafanya, Historia itakumbuka njia
ya kubadilisha mapambano yenye silaha kwa mapinduzi ya kimaendeleo,
yaliyochangia kujenga jamii mpya; basi kwamba Vita vya Ukombozi tulivyoshikilia
havikuwa kwa ajili ya kubadilisha dhuluma ya kireno kwa dhuluma ya kisumbiji,
au dhuluma ya kiulaya kwa dhuluma ya kiafrika, wala hata dhuluma ya kizungu kwa
dhuluma ya kitaifa, basi Umoja na Ushindi ni lengo moja."
( Kutokana na hotuba ya kiongozi msumbiji Samora Mashel
mbele ya nchi yake.)
"Samora Musis Machel", mwenye lakabu ya rais
Samora", alizaliwa tarehe ya 29,mwezi wa Septemba (9), mwaka wa
1933,kwenye kijiji ndani ya Kata ya Ghaza, kusini mwa Musumbiji, alikufa tarehe
ya 19, mwezi wa Oktoba (10), mwaka wa 1986, kutokana na familia fukara
inayofanya kazi ya Kilimo. Na ili kuweza kuendelea katika Elimu yake, alifanya
kazi mchana kama Muuguzi wa Hospitali moja ya Musumbiji, ili kuweza kusoma
usiku katika shule moja, mpaka alihama nchi zake, na alijiunga Mapambano ya
kitaifa. Alijulikana kwa Askari mgumu, Msemaji mwenye Ushawishi,basi yeye ni
mtu wa kijeshi na mtu wa Mapinduzi na Ujamaa dhidi ya Ubaguzi na Ukabila, kama
yeye ana lakabu nyingi, miongoni mwao ni ( Kiongozi wa Mapinduzi).
Kabla ya kuwa rais wa kwanza wa jamhuri huru ya Musumbiji
mwaka wa 1975, - baada ya Uvamizi wa kireno ulioendelea hivi karne nne na nusu
-, alijiunga kama mwanaharakati katika kando ya Ukombozi ya kimusumbiji kwa
Uhuru kutokana na Ureno, na inayojulikana kwa Jina la ( Alferlimo),
iliyopelekwa kwa Misri na Algeria ili kupata mafunzo ya kijeshi, na baadaye
alikuwa rais na kiongozi wake mwaka wa 1969, pamoja na msaada wake kwa harakati
za Ukombozi barani, khasa harakati za Ukombozi katika kusini mwa Afrika na
Zembabwe. Basi akida yake ngumu ilikuwa kama Imani kubwa kwamba Musumbiji
haitapata Uhuru wake wa kweli ila baada ya kuwakomboa wanyonge - siyo katika
bara jeusi tu, bali nje yake pia - na kwa ajili ya itikadi yake hii, Musumbiji
ilikuwa kimbilio yenye Amani kwa harakati zote za Ukombozi.
Anazingatiwa mwanzishi mmoja wa Taasisi ya Umoja wa kiafrika
-Umoja wa kiafrika hivi sasa-, ulioundwa baada ya mwaka mmoja wa mapendekezo ya
( mkutano wa Adis Ababa) , mwezi wa Mei(5), mwaka wa 1962, na Adis Ababa
ulichaguliwa kama kituo cha Taasisi hii mnamo 1963, kupitia kutia saini mkataba
wake mkuu.
Pia inatajwa kwamba yeye alifanya marekebisho mengi kwa
ajili ya kurudisha Usalama wa kitaifa kwa nchi zake, basi aliangalia Afya,
Elimu, na alifanya maendeleo katika taasisi za kielimu na hospitali. Na
kulingana na harakati za Nasser nchini Misri, Samora alizitaifisha ardhi zote
za taifa na Rasilimali za nchi; lililomfanya kuwana umaarufu mkubwa wa nchi
yake, pia lilisababisha kumheshimu toka nchi yake baada ya kifo chake, kupitia
kuunda masanamu kadhaa kwake katika medani zote, na kuyabeba mabango tofauti
yenye kauli kama:(Samora hajafa, bali yumo moyoni mwetu), na kutoa Jina lake
kwa mabarabara na taasisi nyingi. Inatajwa pia kwamba yeye alipata Tuzo na
Nishani kadhaa, nazo ni kama: Tuzo ya (Lenin) kwa Amani, Nishani ya Msalaba
adhimu kutokana na cheo cha kustahiki kwa jamhuri ya kiitalia, na Nishani ya
Khose Marti.
Mnamo Agano la rais mmisri aliyekufa "Gamal Abd Elnaser
", Misri ilizikaribisha harakati za Ukombozi za kimusumbiji hata kabla ya
kuungana kwa Jina la (Ferlimo), pia ilifungua ofisi ya Umoja wa kidemokrasia wa
kitaifa kwa Musumbiji, na kushughulika ndani yake Makada wake wa vyombo vya
habari na siasa. Na Misri ilichukua jukumu la kuwawezesha, kuwafundisha, na
kutoa njia zote za msaada wa kisiasa na kisanaa mpaka Musumbiji ilipata uhuru
wake, Misri ilikuwa ya kwanza ya kuitambulisha. Na Misri imefungua Ubalozi
kwake kwenye mji mkuu ( Maputu); basi ulikuwa Ubalozi wa kwanza wa kiarabu
nchini Musumbiji, na baadaye imetia saini mikataba tofauti pamoja, nayo ni
kama: mkataba wa Ushirikiano kati ya sanduku la kimisri na Ushirikiano wa
kiufundi pamoja na Afrika na Musumbiji mwaka wa 1985.
Comments