Mohamed Faik ni mwananchi mmisri.
Amezaliwa tarehe 28, mwezi wa kumi na moja, mwaka 1929 mjini
Mansoura(Mkoa wa El-Dakahlia). Alisomea kitivo cha Biashara, kisha alipata kozi
kadhaa zinazohusisha ulinzi wa angani nchini Uingereza mwaka 1951.
Maisha yake ya kikazi :
■ Alipewa jukumu la katibu mkuu
wa Shirika la Kiarabu linaloshughulika na kutetea haki za binadamu kuanzia
mwaka 1986 hadi mwaka 2008, naye ni mmoja wa wanachama wa baraza la wadhamini
wa shirika hilo kuanzia mwaka 2008 mpaka sasa.
■ Mkuu
wa baraza la waaminifu wa gazeti la El-Arabi.
■
Alikuwa mkuu wa ofisi ya Rais wa zamani wa Misri Bw. Jamal Abdel Nasser inayoshughulikia mambo ya kiafrika kisha
alipandishwa cheo, akawa mshauri wa Rais anayeshugulikia mambo ya Afrika na
Asia.
■
Alikuwa waziri wa vyombo vya habari wa
Misri kuanzia mwaka 1966 hadi mwaka 1970.
■
Aliteuliwa ili kushughulikia nafasi ya waziri wa mambo ya nje mwaka 1970.
■
Alikuwa makamu wa mwenyekiti wa kamati ya Misri ya mshikamano wa Afrika na wa
Asia pia.
■ Ni
mkuu na mmliki wa shirika la Uchapishaji la El-Arabi lililojengwa mnamo mwaka
1981.
■
Anaongoza baraza la kitaifa la haki za binadamu kuanzia tarehe 22, mwezi wa
Agosti, mwaka 2013 hadi sasa.
Maelezo ya jumla kuhusu Mohamed Faik :
Mohamed Faik ni mwanasiasa maarfu wa kitaifa ambapo
alipoteza umri wake akiutetea uhuru nchini Misri na nje ya Misri pia. Mwanasiasa huyo alikuwa na jukumu la
kukuza harakati za ukombozi za kimataifa, pia alikuwa kama ishara ya harakati
hizo barani Afrika ambapo alikuwa kama mkono wa Rais Jamal Abd El-Nasser barani
humo. Aidha, alifanya kazi bega kwa bega
na Rais wa zamani wa Misri Jamal Abd
El-Nasser, pamoja na hayo alipewa majukumu kadhaa ya kisiasa na ya kiwizara
kwenye kipindi cha utawala wa Rais Jamal Abd El-Nasser. Alikuwa mshauri wa
mambo ya kiafrika na baadye alipandishwa cheo, akawa mshauri wa mambo ya
kiafrika na kiasia. Alichangia kwa kiasi kikubwa katika mapambano ya ukombozi
na alilaani vikali suala la ubaguzi wa rangi barani humo. Pia alifanya urafiki
na viongozi wa harakati ya ukombozi wa kitaifa ulimwenguni na viongozi wa
harakati ya kutoungana na pande zozote kama Nelson Mandela, Kwami Nkroma,
Andira Ghndi, Pandaranika, Videl Kastro, Arnsto Guivara. Mara nyingi mahojiano
yake yameathirika na wale viongozi kwa upande wa uundaji wa mtazamo wa kina kwa
harakati ya ukombozi wa kitaifa ulimwenguni.
Aliendelea na majukumu yake kama waziri wa vyombo vya
habari katika kipindi cha utawala wa
Rais Anwar El-Sadat, lakini alijiuzulu mwaka 1971 baada ya kulalamika juu ya
mielekeo ya kisiasa ya Rais Anwar El-Sadat inayohusiana na kufuta madhara ya
uchokozi wa Israel mwaka 1971. Jambo ambalo lilimweka kifungoni na kumlazimisha
apoteze muda wa miaka 10 ya umri wake kifungoni ambapo alituhumiwa na tuhuma za
bandia tu kama {jaribio la kuipindua/kuiangusha serikali}.
Alipata umaarufu mkubwa kutokana na misimamo yake
iliyodhihirisha ujasiri wake ambapo wakati wa uchokozi wa nchi tatu
{Uingereza-Ufaransa-Uyahudi} dhidi ya Misri mnamo mwaka 1956, alivaa nguo za
wavuvi na kujipenyeza mwenyewe kati ya upinzani wa kiraia dhidi ya majeshi ya
Uingereza mjini Port-Said. Na mnamo mwaka 1976 alipinga uamuzi wa Rais Anwar
El-Sadat unaompa Mohamed Faik uhuru wake kamili kwa sharti moja tu, sharti
lililokuwa ni kumwomba Rais Anwar El-Sadat amsamehe kwa kosa lake hilo
alilolitenda, lakini Mohamed Faik alikataa kufanya hivyo, kwa sababu yeye
mwenyewe hakufanya kosa lolote ili kuomba msamaha, akaishi miaka mitano mingine
kifungoni. Na baada ya miezi michache tu tangu kuachwa huru, alikamatwa tena
akiwa pamoja zaidi ya viongozi wengine 1500, lakini mara hii viongozi hao wote
pamoja na Mohamed Faik hawakuachwa huru ila baada ya Rais Anwar El-Sadat
kuuwawa mwaka 1981 wakati wa maadhimisho ya ushindi wa majeshi ya Misri dhidi
ya Israel kwenye vita ya Oktoba.
Umri wake haukupotezwa bure kifungoni ambapo aliandika kitabu cha Abd El-Nasser na mapinduzi ya kiafrika kwenye kipindi cha kifungo chake.
Mafanikio yake yaliyo muhimu zaidi
- Aliunda programu ya kimuziki kwenye redio.
- Aliunda programu za kielimu kwenye kituo cha
televisheni pamoja na kituo cha uandishi
wa habari.
- Mwenye wazo la kuunda cheo cha Mzungumzaji Rasmi kwa mara
ya kwanza nchini Misri.
- Kazi zake zilikuwa nyingi sana, kwa mfano {utafiti kuhusu
Afrika na haki za binadamu, tafiti kuhusu Rais Jamal Abdel Nasser na utafiti
kuhusu mapinduzi ya kiafrika}.
Comments