Ndani ya kurasa za historia kuna wahusika wakubwa wasiowezekana kusahauliwa , basi yeye ni (mwalimu) wa bara la Afrika neno lenye maana ya Mwalimwa kwa lugha ya Kiswahili , kwa mujibu wa mchango wake bora katika masuala ya mifumo ya kisiasa za kiafrika na mahusiano ya kiarabu na kiafrika na nchi za bonde la Nile .
Basi
kupitia maandishi yake aliunda shule bora ya kimisri katika masomo ya kiafrika kwa
kipindi kilichozidi kwa miaka Hamsini , na ameweka mtaala kwa shule hii akisema
: tunaishi kaskazini mashariki mwa Afrika na tunazungumzia mengi Afrika, lakini
hatulielewi isipokuwa kwa kuchanganya kati ya masomo na uwanja katika mfumo wa
taaluma ya kitaasisi ,na tukifikia hilo sasa tunalielewa Afrika kwa haki ya
kuelewa " Vizuri" na kujiweka ndani ya moyo na jicho.
Kwa Upande wa
Utu wake , marehumu akitafuotishwa kwa maadili yake bora na tabasamu lake lisiloacha
uso wake, basi kwamba wanafunzi wake walimwita
kwa( mwalimu mwenye tabasamu ya uso na
Mkuu mkubwa) wakati ambapo alitawala vyuo vitatu navyo ni Uchumi na sayansi za kisiasa vyombo vya habari
na tasisi ya mafunzo ya kiafrika, alisifwa kwa sifa ya unyenyekevu mkubwa,
uwezo wake wa kiutawala na umakini kwa maana ya kibinadamu kama mfano wa nadra
usiokariri.
Kwanza :Tawasifu
Dokta Abd Elmalek
Ali Ahmed Odeh alizaliwa katika mkoa wa Dakahilia mwezi wa Machi mwaka wa 1927,
na alipata shahada ya Sayansi ya kisiasa toka kitivo cha Biashara, Chuo kikuu
cha Kairo mwaka wa 1948, na Shahada ya
Uzamili wa Sayansi za kisiasatoka Chuo
kikuu cha Kairo mwaka wa 1951.
Dokta Abd El malek Odeh ameandaa ujumbe wa Uzamivu wa( uzito wa kiisilamu), lakini daktari Abd El
kader Hatem amemwomba ujumbe mwengine ili kuendana mwelekeo mkuu kwa nchi katika umakini kwa masuala ya kiafrika , na
hatua hii ilikuwa kama mwelekeo wa kugeuka ili awe mtaalamu wa kwanza katika
masuala ya kiafrika kwa kupata Uzamivu
wa Falsafa katika Sayansi za kisiasa kutoka chuo kikuu cha Kairo mwaka wa 1956.
katika
muktadha huu daktari Boutrous Ghali "katibu mkuu wa zamani wa umoja wa
mataifa" anasema kwamba nilikutana na daktari Odaa nilipokuwa nikihudhuria
majadiliano yake ya kupata Uzamivu , na alinivutia
kwa majadiliano na majibu kwa maprofesa wake, kwa hivyo wakati wa tunapohitaji
kuteua mwalimu mpya katika sehemu ya Sayansi ya kisiasa katika kitivo cha Biashara
katika chuo kikuu cha Kairo niliwaza jina la daktari Odaa na nikapendelaza achaguliwe
kwa baraza la sehamu kwa ujuzi wake wa
kisayansi na ameteuliwa kama mwalimu wa sayansi ya kisiasa katika chuo kikuu
cha Kairo mwaka wa 1957.
Dokta alipewa
jukumu toka Misri ili kusafiri nchi kadhaa za kiafrika hasa baada ya uhuru wa Guine Konkere mwaka wa 1958
ili kuangalia uzoefu wa kujenga chama
cha kidemokrasia cha Guine, pamoja na maarifa wake kwa harakati za ukombozi wa kitaifa ya kiafrika
kupitia chama chake cha jumuyia ya kiafrika
iliyomsaidia kujenga njia za mawasiliano na vyombo vya habari ya maarifa ya
kiafrika inayopambana ukoloni pia iliyoamini umuhimu wa kurudisha historia kwa Afrika
kutoka mtazamo wa kistaarabu wa kiafrika.
Marehemu alielekea
katika maisha ya kisayansi na alikuwa
profesa msaidizi wa sayansi za kisiasa mwaka wa 1962, profesa wa sayansi za kisiasa kutoka mwaka wa
1968 hadi mwaka wa 1978, alifundisha pia huko Marekani kama profesa Mgeni kwenye chuo kikuu cha jimbo la Indiana katika kipindi
cha 1965-1964, na alifanya kazi kama profesa katika taasisi ya utafiti na mafunzo ya kiafrika chuo kikuu cha Kairo
mwaka wa 1974, kisha alitawala Ukuu wa kitivo cha habari chuo kikuu cha Kairo 1971-1979
na rais wa sehemu ya sayansi za kisiasa chuo kikuu cha Kairo .
Alisafiri Marekani
ili kufanya kazi kama profesa mgeni
katika chuo kikuu cha New York (stoni
brok) Marekani mwaka wa 1979-1978, na aliporudi kutoka Marekani alitawala ukuu
wa kitivo cha habari chuo kikuu cha Kairo 1981-1979, na wakati huo huo Mkuu wa
kitivo cha uchumi na sayansi za kisiasa chuo kikuu cha Kairo 1981-1980 na mkuu
wa taasisi ya utafiti na mafunzo ya kiafrika chuo kikuu cha Kairo 1981 .
Alifundisha
pia nje ya jumhuri ya kimisri kama profesa wa sayansi ya kisiasa na mashauri wa
chuo kikuu cha sanaa kwa masuala ya kitataaluma(jumhuri ya yaman) katika
kipindi cha 1985-1981, aliporudi alikuwa profesa wa wakati wote
"bure" katika kitivo cha uchumi na sayansi za kisiasa chuo kikuu cha Kairo
mwaka wa 1978.
Pili : nafasi za kisayansi :
Alishikia nafasi kadhaa za kisayansi akiwa ni
pamoja na Mwandishi mkuu wa habari ya
gazeti la kimataifa lililochapishwa toka Taasisi ya El Ahram
1980-1956 , ambapo alishirikiana
na Dokta Buotros Ghali katika kuanzisha gazeti la kwanza lilichapishwa mwezi wa
Julai 1965.
Dokta Ali Eldin
Helal "profesa ya sayansi ya kisiasa katika chuo kikuu cha Kairo" alieleza
kwamba Dokta Odaa alishiriki katika kuweka misingi ya kazi katika Gazeti la
siasa ya kimataifa , kuandaa maudhui zake na kuchagua vijana watafiti na kwenye
kurasa zake huchapishwa makumi ya tafiti na ripoti kwa hiyo, siyo ziada kwa kusema kwamba siasa za kimataifa zinarejeshwa kwake na Dokta Buotros Ghali
kwa mwendelezo wake.
Mnamo
mwaka wa 1970 alikuwa mshauri wa waziri wa zamani sana wa vyombo vya habari Bwana( Mohamed Hassanien Heikal)
kisha mkurugenzi wa kituo cha mafunzo ya kisiasa na mikakati katika al-Ahram Kairo
1975-1974,
na alitawala msaidizi wa mwandishi mkuu
wa habari na rais wa idara ya taasisi Al
ahram Kairo 1974-1971 .
Pamoja na kufanya kazi katika nafasi kadhaa za
kimataifa mnamo kipindi cha 1978-1976 alitawala nafasi ya Sekertari mtendaji wa
mfuko wa sanduku la kiarabu kwa msaada wa kiufundi kwa Afrika- katiba kuu ya mkusanyiko wa nchi za kiarabu ,alikuwa mshauri wa masuala
ya taasisi ya kimataifa na kitaifa- wizara wa mambo ya ndani nchini Bahrin 1991-1967 , pia alishiriki katika
kamati maalumu ya utafiti wa mgogoro barani Afrika,
chuo kikuu cha umoja wa mataifa huko Tokyo 1985-1984 ,na pia alitawala nafasi ya makamu wa rais wa chama cha kiafrika kwa sayansi za kisiasa.
Alikuwa
msaidizi kwa kamati ya sayansi ya
kisiasa kwa baraza kuu la utamaduni huko
Kairo 1991-1992, alikuwa pia mwanachama wa mjadala wa utafiti migogoro barani
Afrika ulioandaliwa kwa Umoja wa mataifa na chuo kikuu cha Umoja wa
mataifa huko Tokyo, na alikuwa mwanachama wa mkutano wa kiafrika ulioandaliwa
kwa tasisi ya UNISCO huko Paris ili
kutafiti masuala ya Afrika kwa mustakbali mnamo mwaka wa 1955, na alijiunga na baraza la kimisri kwa
mambo ya nje 1999 .
Tatu:Uanachama wa Jumuyia:
Dokta Odaa amekuwa mwanachama wa vyama kadhaa kwa
ndani na kimataifa na ikijumulisha uanachama wa Jumuia ya kimataifa kwa mafunzo ya vyombo vya habari na mawasiliano (Marekani)
, mwanachama wa taasisi ya kiafrika (Misri ) , taasisi ya kimisri kwa sayansi
ya kisiasa , taasisi ya kimsri wa uchumi na Sheria, taasisi ya kimsri kwa
kanuni ya kimataifa na taasisi ya kiarabu kwa Sayansi za kisiasa .
Nne : sifa na Lakabu zake.
Profesa Abd Elmalek Odda alisifu kwa sifa nyingi nzuri
basi kwamba yeye ni mwalimu mwenye uso wa
tabasamu ambapo alikuwa ametendana na
wanafunzi wake kwa mtindo unaojumuisha Uongozi na huruma ya baba na wanafunzi wake
wanakumbuka msimamo wake katika kuwasaidia wanaojihusisha katika shughuli za
kisiasa katika vyuo vikuu katika kukabili huduma za usalama na ushindi wake kwa
haki za wanafunzi za harakati za uhuru wao wa kueleza maoni yao na misimamo yao
ya kisiasa na katika mfumo huu mwandishi
wa habari "Saeed Elshahat" aliyekuwa Mwanaharakati katika Klabu ya
Mawazo ya Nasserist katika chuo kikuu mwaka 1981 anaeleza kwamba wakati
marehemu alikuwa profesa wa Kitivo cha Uchumi na Sayansi za kisiasa , alimwokoa
kutoka mkono wa Meja wa Usalama wa Nchi aliyemkamata na wanafunzi wengine kwa
sababu wao walikuwa wamesambaza vipeperushi vinawasisimua wanafunzi kwa kukataa
uchaguzi wa Umoja wa wanafunzi katika
Maandamano dhidi ya kuwepo wa Ulinzi wa
chuo kikuu.
Dokta Abd Elmalek Odda amejitetea haki za wanafunzi za
kujieleza maoni yao na alikataa uingiliaji wa Ulinzi wa chuo kikuu katika masuala ya wanafunzi na
ameruhusu haki ya kuandamana na kusambaza vipeperushi , hayo yote yalitokea
mnamo miaka ya Themanini wakati ambapo
yote hayakuruhusiwa na alikuwa amesikiliza kwa shauku kubwa kwa wanafunzi wake
wakati wao walikuwa wamempinga na wamemjadili na yeye alikuwa amejibu na
tabasamu pana kwa upendo na furaha
ambapo ni baba , mwalimu na mtaalamu.
Na sifa ya unyenyekevu inazingatia moja ya sifa muhimu zinazotofautisha mhusika wake ambapo ni mojawapo wachache ambao hakuna
anayepingana na Thamani yao ya kisayansi na tabia zao nzuri za kibinadamu na angalau mnamo kipindi Fulani yeye alikuwa Mkuu wa vitivo vitatu navyo ni kitivo cha uchumi na sayansi za kisiasa ,
kitivo cha habari na taasisi ya mafunzo ya kiafrika katika wakati mmoja lakini
sifa ya unyenyekevu ilikuwa mojawapo sifa muhimu zinazotofautisha mhusika wake .
Profesa Hamdy Abd Elrahman "profesa wa sayansi za
kisiasa katika chuo kikuu cha Kairo"
anasema kwamba Ni nadra na isiyo ya kawaida kwamba tunapata anayekuwa na
unyenyekevu kama huu na wanafunzi na wenzake na yeye hamruhusu mtu yeyote
kubeba mkoba wake lakini yeye anaubeba mwenyewe na ninakumbuka kwamba mimi
nilikuwa naye mjini Khartoum mwanzoni mwa miaka ya tisini ili kuhudhuria
mkutano wa kisayansi kuhusu Ukamilifu barani Afrika ambapo alikuwa hakuketi mbele ya bodi
hata mimi nilihisi haya kwa kukaa kwake
katika safu za mwisho na nimeshangaa
kutoka unyenyekevu wake mkubwa.
Na hivyo ndivyo profesa Mahmoud Abo Elenin "profesa
wa sayansi za kisiasa na mkuu wa zamani wa taasisi ya mafunzo na utafiti ya
kiafrika" amesisitiza kwa msemo wake : sisahau wakati nilikwenda kwa
Maktaba ya kitivo cha Uchumi na nimengoja dakika
kadhaa katika ofisi ya Sekretari kwa shughuli zake na wageni wake ofisini na wakati alikuwa
ametoka ili kuwaaga ، Jicho
lake likanijia na akasema :tangu lini na wewe yupo hapa ? Mimi nimejibu : tangu
dakika kadhaa
Na alisema : sina maprofesa wanaketi nje !! lakini
yeye amemfunza kitu muhimu nimekifanya wakati nilikuwa Mkuu wa taasisi
Hayo ni pamoja na uwezo wake wa mawasiliano ya kijamii
na pande zote iliyomfanya kuwa mwenye
thamani na wa kimo cha kisayansi na kibinadamu ambayo ni nadra kukaririwa ,
ambapo aliweka mgusa na alama zake wazi
katika nyanja ya sayansi za kisiasa kwa ujumla na nyanja ya mafunzo ya kiafrika
hasa na wakati wote alishughulikia kwa masuala na matatizo ya nchi na wanafunzi
wake wameeneza katika taasisi mbalimbali za dola na mashirika , vyuo vikuu ,
vituo vya utafiti , wizara ya mambo ya nje , vyombo vya habari vinavyosemwa ,
vinavyosikiwa na vinavyoonwa , katika Mkusanyiko
wa Nchi za Kiarabu na katika ndani na nje ya misri ambapo alikuwa na wanafunzi
kutoka ndugu waarabu na waafrika na Licha ya tofauti hii , aliweza kuwasiliana
na wote na Kuuliza juu yao na kuwashiriki furaha na huzuni zao.
Na katika muktadha huu , Dokta Mostafa Elfeky anasema
wakati niliomba kusoma katika chuo kikuu
cha London katika mwaka wa 1971
, profesa Abd Elmalek Odda alikuwa amemtuma Kwangu
kumpendekeza kwake na kwa profesa wangu Botros Botros Ghali Kujaza hati
zinazohitajika ili kuandikisha katika kitivo cha mafunzo ya mashariki na
kiafrika na marehemu Alikuwa Mwanazilishi wa Familia ya Nile na ambaye alitupa
kutoka ujuzi wake kile wengine wanakiuma
na wanafunzi wake wanamkaribia kwa njia sio kawaida ambapo Maelfu yalifurika
baba yake na alisambaza ufahamu wa masomo
ya kiafrika na kimataifa katika wakati mmoja, na mimi bado nakumbuka ziara yake
kwangu katika london na mimi ni mwanadiplomasia
katika ubalozi wa kimisri katika asubuhi na mwanafunzi katika chuo kikuu
cha London jioni na jinsi ushauri wake ghali ulivyokuwa kama kitu adhimu sana
katika Hali ngumu zile.
Na marehemu alikuwa amejipambanua kwa Ukali wa
kiteknolojia na kitaaluma na aliwakabidhi
kwa kila mtu aliyefanya kazi naye , kwa hiyo Mfano wa uchambuzi uliotolewa na Dokta
Odda kwa wanafunzi wake ili kufunza ukweli wa kisiasa unajumuisha vipengele
vitatu ambavyo ni historia , ufahamu wake na Mtaala na kufuata sheria zake
,vyombo ambavyo mtafiti anavitumia ili kufikia ukweli na kuchambua zaidi ya
habari na maelezo ambapo alikabiliana na masuala ya sehemu katika kiwango
kidogo na kwa kiwango sawa cha ufanisi katika kushughulikia masuala ya kisiasa
katika kiwango cha ujumla ambavyo kinatoa
uaminifu zaidi kwa uchambuzi wa kisiasa
Kama marehemu anajulikana katika uwezo wake wa
kisayansi na utafiti alikuwa wa kidato cha kwanza, na alithibitisha mafanikio
yaliyopatikana katika nafasi mbali mbali alizozishikilia, alikuwa mkuu wa
maprofesa , ambapo alikuwa mkuu wa Kitivo cha Uchumi na Sayansi za kisiasa ,
Kitivo cha Habari na Taasisi ya Mafunzo ya Afrika, na licha ya uwezo wake bora
wa kiutawala Katika siku ya kukandamiza ukandamizaji wa wasaidizi au uwekaji wa
vikwazo au vikwazo dhidi yao, alikuwa na mwelekeo zaidi wa utawala wa
kibinadamu, ambao ulionekana kama bora kufikia malengo ambayo ukatili na nguvu
haziwezi kufikia.
Kwa hivyo,
ukubwa wa mwanadamu ulikuwa moja ya vifunguo muhimu kwa mhusika wake na labda
alizingatia mawasiliano ya kibinadamu na mahusiano mema ya kibinadamu kama
lango la kuhakikisha kwa mafanikio yoyote ya kisayansi.
Tano: Nishani
na Heshima
Dokta Odda
alipewa Nishani ya Daraja la Kwanza la Sayansi na Sanaa mnamo 1987 kwa kutambua
michango yake ya kielimu katika uwanja wa mafunzo ya Kiafrika. Pia sherehe moja ilifanyika katika baraza kuu
la Utamaduni katika Kairo mwaka wa 2009 wakati wa kuzaliwa kwake kwa miaka ya
Themanini ambapo wataalamu wengu wa Sayansi za kisiasa waliihudhuria , wakati
ambapo Dokta Mustafa El fiky alisema:
"Tunakusalimu, baba wa watoto hao watatu, Dokta wawili Jihad na
Hisham, na wa tatu ni kila mmoja wetu katika wanafunzi wako katika miongo
mitano iliyopita! Ulibarikiwa na mfano wa kutoa, mfano wa udhamini na ishara
ya ubaba, Mwenyezi Mungu aliongeza maisha yako na kukupa vile
vile ulivyotoa nchi na vizazi mfululizo."
Sherehe ya kumheshimu katika Chuo Kikuu cha Kairo
katika ukumbi mkuu wa mikutano wa Taasisi ya Utafiti na Mafunzo ya kiafrika iliyofanyika
mnamo Machi 27, 2013, katika hatua ya Profesa Ibrahim Nasr El-deen, profesa wa
sayansi za kisiasa katika chuo kikuu, kuadhimisha mtaalamu yeyote maishani
mwake, na alihudhuriwa na kikundi cha wanasayansi, mabalozi, wataalamu,
wanadiplomasia na wanaompenda Dokta Abdel Malik Odda kwa kumzingatiwa mkuu
wa masomo ya Kiafrika tangu miaka ya
hamsini, akihudhuriwa na kikundi cha maprofesa wa sayansi ya kisiasa nchini Misri
na ulimwengu wa Kiarabu, kama Dokta Ali
al-Din Hilal, Dokta Saif Al-Din Abdel-Fattah, Dokta Mustafa Alawi, Dokta Kamal
Al-Menoufi, Dokta Helmy Shaarawy, Dokta Ahmed Youssef Al-Qurai, Dokta Ikram
Badr Al-Din, Dokta Mahmoud Abu El-Enein, Dokta Farag Abdel-Fattah , Mabalozi wa Kiafrika,
wataalamu,wanadiplomasia na vyombo vya habari, na umati mkubwa wa wanafunzi wa
mafunzo ya Kiafrika na bara la Afrika, na wengine wengi, ilikuwa sherehe ya
kihistoria kwa maana kamili ya neno hilo katika maisha ya wataalamu wa sayansi za kisiasa.
Sita : sherehe ya ukumbusho
Kitivo cha Uchumi na sayansi za kisiasa katika chuo
kikuu cha Kairo kilipanga Huduma ya ukumbusho ya Dokta Abd Elmalek Odda profesa
wa zamani wa kitivo katika tarehe ya tano mwezi wa kwanza mwaka 2014 na hivyo
kwa kuhudhuria Dokta Hala Elsaeed profesa wa kitivo , Dokta Gaber Nassar mkuu wa chuo kikuu cha Kairo
na marehemu Dokta Botros Botros Ghali Rais wa heshima wa Jumuiya ya Haki za
Binadamu pamoja na idadi kadhaa za washiriki wa Kitivo
Na inafahamika kwamba Dokta Hala Elsaeed profesa wa
kitivo cha Uchumi na sayansi za kisiasa na zamani katika chuo kikuu cha Kairo
Alizindua jina la marehemu kwenye ukumbi wa namba ya 5 kitivoni Kwa kumtambua
na kumkumbuka hasa Dokta Odda alitoa maktaba yake ya zamani inayojumuisha
takriban vitabu elfu kumi na tano kwa kitivo cha uchumi na sayansi za kisiasa
na kutoka upande wake Dokta Gehad Odda ambaye alitoa neno la familia ya Dokta
marehemu Abd Elmalek Odda aliushukuru
usimamizi wa kitivo cha uchumi na sayansi za kisiasa kwa sherehe ya kuheshimiwa
ya baba yake na kumkumbuka
Chama cha wahitimu wa
vyombo vya habari katika kitivo Cha habari katika chuo kikuu cha Kairo
kilipanga sherehe ya ukumbusho ya Dokta Abd Elmalek Odda profesa wa kitivo cha
habari wa zamani , hii hasa wahitimu wa kitivo wanamkumbuka marehemu kwa
kumbukumbu zisizosahauliwa kuhusu mahusiano yake mema yaliyokuwa kati ya wanafunzi na profesa wao wa chuo kikuu na Dokta
Hassan Emad Mekawy na Idadi kadhaa za maprofesa ya kitivo na miongoni mwao : Dokta
Magy Elhalawany , Laila Abd Elmegeed , Ali
Agwaa , familia ya marehemu na maprofesa wa kitivo cha uchumi na sayansi
za kisiasa na taasisi ya mafunzo na utafiti ya kiafrika wameihudhuria
Na hitimisho , Hakuna neno katika lugha linaloweza kumsifu
marehemu profesa Abdel Odda ambapo Alikuwa mfano bora wa Kile kinachopaswa kuwa
na profesa kutoka sifa nzuri na kile
kinachopaswa kuwa profesa wa uzani na
lazima anajishughulikia na masuala yote ya nchi katika daraja la kwanza na kile
kinachopaswa kuwa raia mmisri wa asili
alihusishwa na mizizi yake, basi kumbukumbu kwake kutabaki hai kwa historia
yote na kile ametoa kutoka urithi wa kisayansi na michango ambayo haijawahi
kutekelezwa hasa katika uwanja wa masomo ya kiafrika.
Comments