Kiongozi Mmisri na Mwafrika Gamal Abdel Nasser au (Nasser) aliinua kauli mbiu ya "Inua kichwa chako ewe ndugu yangu . Enzi ya Dhuluma na Utumwa ilimalizika wakati alipoongoza mapinduzi ya Julai 23, 1952, yaliyokuwa hatua muhimu sio tu katika historia ya Misri ya kisasa, bali katika historia ya bara letu la Afrika kwa ujumla, ambapo yalikuwa kama ufunguzi wa mapinduzi na harakati za Ukombozi katika sehemu nyingi za Afrika
Kwa Usimamisi yake na kuunga mkono kwake kwa mapinduzi na
harakati za ukombuzi katika nchi nyingi
za kiafrika,Nasser ametawazwa kwa lakabu ya (Abu Afrika) na amepata kuwasifu kwa mamilioni ya watu hadi
leo..hakuna mji mkuu mmoja wa Kiafrika bila mtaa uliopewa jina lake, na
masanamu yake yametawanyika katika viwanja vingi vikubwa vya Afrika, na sanamu
la mwisho na lenye ukubwa Zaidi lilikuwa huko mjini Johannesburg, Afrika
Kusini, ambayo ilifunuliwa na alama kubwa ya Kiafrika Nelson Mandela mwenyewe
mbele ya wana wa kiongozi mmisri , aliyewaalika kuhudhuria Hafla hii.
Malezi yake
Marehemu Gamal Abdel Nasser alizaliwa huko Aleskandaria kabla ya matukio ya mapinduzi ya 1919
yaliyotikisa Misri, na kusisimua hisia za Wamisri, yakaongeza hisia za
mapinduzi na uzalendo mioyoni mwao, na kupeleka roho ya kupinga dhidi ya
wakoloni. Yeye ana mizizi ya Saeed kutoka kijiji cha Bani Murr mkoani mwa Assiut
wa familia ya kimisri ya kati Kama
mamilioni ya familia za Wamisri.
Maisha yake ya
kijeshi
Na ikiwa tunataka kuzungumzia maisha yake ya kijeshi,yamejaza kwa matukio
tofauti,ambapo Gamal amepata cheti cha shule ya sekondari kutoka shule ya
Alnahda Almasreya huko Kairo (1356 / 1937). alitamani kusoma Sheria, lakini
mwishoni aliamua kuingia chuo kikuu cha
Jeshi, baada ya kukaa miezi michache kusoma sheria,baada ya kuhitimu kutoka
Ktivo cha Jeshi (1357 AH / 1938), alijiunga na kikosi ya 3 ya bunduki,na
amehamia “menkbad”mkoani Asiut,wakati
alimkutana na Anwer Alsadat na Zakaria Mohy Alden.
Mwaka wa 1939 Gamal alihamia Aleskandaria . Na huko
amemkutana na Abdelhakeem Amer, aliyekuwa amehitimu katika kundi lake
linalofuata la chuo kikuu cha jeshi,na katika mwaka wa 1942, alipelekwa kwenye
kambi ya El Alamein,na baad ya kipindi kichache alihamishwa kwenda Sudan pamoja na Amer,aliporudi kutoka Sudan
aliteuliwa kuwa mwalimu katika kitivo cha Jeshi,alijiunga na kitivo cha
Wafanyikazi wa Vita;wakati wa masomo yake, alikutana na wenzake ambao
alianzisha nao “Shirika la Maafisa Huru”.
Na kuhusu Taasisi
hii,
Msingi wake ulianza
kuchukua sura kati ya 1945 na 1947,maafisa wengi, ambao baadaye wakawa Kamati
ya Utendaji ya Maafisa Huru,wanafanya kazi katika vitengo vingi karibu na
Kairo, na walikuwa na uhusiano wenye nguvu na wenzao, walishinda kati yao
wafuasi.
Utaratibu wa kimapinduzi
Vita vya 1948 vilikuwa cheche cha kwanza kilichosababisha
azimio la maafisa juu ya mapinduzi. Wakati huo huo, maafisa huru wengi walikuwa
tayari wakijihusisha katika Vita vya
Palestina. Nasser alikuwa na jukumu kubwa katika kuanzishwa kwa Shirika la
Ukombozi la Palestina mnamo 1964 na Harakati ya Kimataifa isiyo ya Kuagawa.
Baada ya Vita vya Palestina mnamo 1949, wazo la kuanzisha
shirika la mapinduzi la siri katika jeshi lilikomaa wakati ambapo tume ya
uanzishaji uliundwa mwanzoni ulijumuisha wanachama watano tu nao ni ( Gamal Abd Elnasser – Kamal Eldin
Hussen – Hassan Ibrahim- Khaled Mohey Eldin-
Abd Elmenim Abd Elraoof ) Baada
ya hayo hadi kumi, baada ya kuunganishwa na: Anwar Sadat, Abdul Hakim Amer,
Abdul Latif al-Baghdadi, Zakaria Mohieldin, na Gamal Salem. Tharwat Okasha, Ali
Sabri na Youssef Mansour Siddiq walibaki nje ya kamati.
Wakati huo, Gamal Abdel Nasser aliteuliwa kama mwalimu
katika kitivo cha Wafanyakazi wa Vita,
na akapewa daraja la Kabbashi (Kanali), baada ya kupokea diploma ya Wafanyikazi
mnamo 1951 kufuatia kurudi kwake kutoka Vita vya Palestina. Yeye na wenzake
huko Fallujah walinaswa kwa zaidi ya miezi minne, na idadi ya hewa inawapiga
wakati wa kuzungukwa kwa mashambulizi 220.
Nasser alipata uzoefu mrefu wa kijeshi na kisiasa kupitia
kozi nyingi - zilizopatikana nje ya Misri, kama vile "Silaha au Kozi ya
Hatari huko Uingereza" - iliyomruhusu kutambua maisha ya Magharibi na
kuathirika kwa mafanikio yake.
Sio hiyo tu, bali aliathirisha kwa
matukio ya kimataifa na hali halisi ya Waarabu na matukio ya kisiasa,
alifaidika kutokana na taswira ya Vita vya Pili vya Ulimwenguni na mapinduzi ya
Bakr Sidqi Pasha kama mapinduzi ya kijeshi ya kwanza katika ulimwengu wa
Kiarabu nchini Iraqi mnamo 1936, na mapinduzi ya Rashid Ali Al Kilani nchini
Iraqi dhidi ya Kiingereza na serikali iliyo waaminifu kwao mnamo 1941.
Iliyothibitishwa kwa mafuta ya Irani mnamo 1951.
Mapinduzi ya Julai 23, mwaka wa 1952 hayakuwa kwa kuondoa
serikali kama wengine wanavyodai, lakini kama matokeo ya mlolongo wa mapungufu
yaliyowakabili Mfalme Farouk, wa ndani na nje, khasa machafuko katika uhusiano
wake wakati wa Vita vya Pili vya Ulimwengu kati ya nchi za Axis na Washirika,
na utumizi mbaya na ushirika wake na tuhuma za ufisadi na uhusiano mbaya.
Vitu vyote vilikasirisha Maafisa Huru waliokuwa wamemchagua
Mohamed Naguib kama rais wao na baadaye rais wa kwanza kwa Misri;hii ni kwa
sababu ya heshima na kuthamini kwa maafisa wa jeshi, na sifa ya kizalendo , na
pia kuwa katika kiwango cha juu katika jeshi.
lakini baada ya muda isyo mrefu , utawala ulihamishiwa kwa Gamal Abdel Nasser mnamo 14
Novemba 1954, na aliweza kumaliza makubaliano na Uingereza ili kuwaondoa
wanajeshi wake kutoka Misri mnamo 19 Oktoba 1954, baada ya Wamisri na Uingereza
kukubaliana kuipa Sudan uhuru.
Mwaka wa 1958, alianzisha kitengo cha kuungana na Syria,
kilichoitwa nchi mpya ya Jamhuri ya Kiarabu.Lakini, kitengo hiki haikuchukua
muda mrefu.ambapo mapinduzi yalitokea katika eneo la Syria mnamo Septemba 1961
yalisababisha kutangazwa kwa kujitenga, na ndipo makubaliano ya umoja makini na
Iraq na Syria mnamo 1964, lakini kifo cha Rais wa Iraqi Marshal Abdul Salam
Aref mnamo 1966 na vita vya 1967 vilizuia umoja.
Dalili moja yenye umuhimu zaidi kwa msimamo wa mtu huyu ni
kwamba baada ya vita vya 1967, au kile kinachojulikana kama "kurudi
nyuma", Nasser alitoa taarifa kwa raia wakimtaka ajiuzulu, lakini
maandamano yalifanyika katika miji mengi ya Misri, hasa mjini Kairo, ikimtaka
aendelee na kuchukua jukumu katika hali hizi ngumu.
Mafanikio yake
Mojawapo ya mafanikio makubwa ya mtu huyu mkubwa ni idhini
yake ya mahitaji ya Syria ya umoja na Wamisri katika Jamuhuri ya Falme za
Kiarabu, iliyodumu sio zaidi ya miaka mitatu chini ya jina la Jamhuri ya
Kiarabu (1958-1961) kati ya fitina kwa kuiondoa.
Mbali na majibu yake kwa wito wa Iraqi kufanikiwa kwa umoja
na Iraqi na Syria baada ya kudhaniwa na Rais wa Iraqi Marshal Abdul Salam Aref
urais wa Jamhuri ya Iraqi, makubaliano hayo yaliyojulikana kama Aprili 16, 1964
Kwa kuongezea, Nasser alianzisha Shirika lisilo la Kujiunga
na Rais wa Yugoslavia Tito, Sukarno wa Indonesia na Nehru wa India, na
alichangia kuanzishwa kwa Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu mnamo 1969.
Miongoni mwa mafanikio yake mashuhuri ya ndani ilikuwa
utaifishaji wa Mfereji wa Suez, kutaifisha kwa benki za kibinafsi na za nje
zinazofanya kazi nchini Misri, uanzishwaji wa Bwawa kuu juu ya Mto wa Nile,
uanzishwaji wa Ziwa la Nasser, moja ya maziwa makubwa zaidi ya viwandani
ulimwenguni, na hitimisho la makubaliano ya uhamaji na Briteni mnamo 1954,
ambapo askari wa mwisho wa Uingereza alihamishwa. Mfereji wa Suez na Misri zote
ziko tarehe kumi na nane ya Juni 1956.
Vile vile sheria za mabadiliko ya kilimo na uainishaji wa umiliki wa kilimo, wakati ambapo wakulima
wa Misri kwa mara ya kwanza wanamiliki ardhi wanayoifanya kazi na
kuzifanya kazi na kuainisha miliki za wenye Kimwinyi imesalia ekari 200 tu kwa
kuongezea sheria kadhaa kama sheria za Julai
za kiJamaa 1961.
Alichangia pia kuanzishwa kwa Televisheni ya kimisri,
uanzishwaji wa Corniche El Niil (1960), ujenzi wa Uwanja wa michezo wa Kairo
huko Nasr City (uwanja wa zamani wa Nasser), kuanzishwa kwa Mnara wa Kairo,
kuanzishwa kwa gazeti la Jamhuri ya Misri mnamo 1954, na kuanzishwa kwa
Maonyesho ya Kitabu cha Kimataifa cha Kairo.
Nasser amekuwa akitamani kusimama na maskini, na kumfanya
kupanua elimu bure katika ngazi zote, na pia upanuzi thabiti wa utengenezaji na
zaidi ya viwanda 3,600 vilivyoanzishwa.
Misiri pia ilishuhudia mnamo kipindi cha kuanzia miaka ya
sitini hadi mapema kuwarudisha tena kiuchumi na viwandani, baada ya Jimbo
kuanza mwenendo mpya wa kudhibiti vyanzo vya uzalishaji na njia, kupitia upanuzi
wa kutaifisha Benki, kampuni na viwanda vikubwa, na uanzishaji wa miradi
mikubwa ya viwandani. Nasser alijenga shule na hospitali na alitoa fursa za
kazi kwa watu. Na hayo yote pamoja na
uanzishaji wa Bwawa kuu la juu linalozingatiwa mafanikio yake muhimu Zaidi,
wakati ambapo limelinda Misri toka hatari za Mafuriko, pia kuongeza mahali pa
kilimo kwa ekari milioni moja pamoja na
Kuchukua zaidi Umeme katika Misri, ambayo inatoa nishati zinahitajika
kwa mimea na miradi mikubwa ya viwanda.
Jukumu lake barani Afrika
Katika kipindi chote cha enzi yake, Nasser alihakikisha
kuwepo kwa Wamisri barani Afrika kuko wazi na dhahiri. Kulikuwa na ofisi zaidi
ya 52 za kampuni tatu za sekta ya umma zinazofanya kazi katika uwanja wa
biashara ya nje, ambazo ni: kampuni ya Al-Nasr ya kuuza nje na kuagiza, kwa
sehemu kubwa zaidi, Misri ya biashara ya nje, na Misri kwa biashara ya nje.
Matawi haya ya Wamisri yamecheza jukumu muhimu katika kukuza bidhaa za Wamisri
kwenye bara na kuimarisha mahusiano ya
kimisri na Kiafrika.
Jukumu la uigizo lililochukuliwa na Wamisri wakati wa Rais
Gamal Abdel Nasser limesaidia sana katika kuongeza jukumu la Afrika katika
vikao vya kimataifa. Ambapo zaidi ya nchi 51 wakati huo kupata uhuru na
kujiunga na shirika la kimataifa kuongezeka kwa viti 52, wakati Afrika
iliwakilishwa na nchi tisa tu huru mnamo 1960 .. Umoja wa Mataifa ulipitisha
siku maalum iliyoitwa bara la Afrika, (ambapo Mei 25 ya kila mwaka kama siku ya
Afrika).
Mapinduzi ya Kiarabu
Rais Nasser ni mmoja wa viongozi mashuhuri wa umoja wa
Kiarabu na hii ni hisia inayozidi miongoni mwa watu wengi wa Waarabu. Rais
Nasser aliunga mkono sababu ya Palestina na yeye mwenyewe alichangia kwa vita
vya 1948. Alipochukua urais, alichukulia suala la kipaumbele la Palestina kuwa
moja ya vipaumbele vyake kwa sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na kanuni ya
mkakati kwamba kuanzishwa kwa nchi yenye uadui kwenye mpaka wa Misri
kutasababisha uvunjaji wa usalama wa kitaifa wa Misri.
Abdel Nasser alikuwa na jukumu kubwa katika kuunga mkono
mapinduzi ya Algeria na kukumbatia sababu ya ukombozi wa watu wa Algeria katika
vikao vya kimataifa.Alitafuta pia kufanikisha umoja wa Kiarabu. uzoefu wa umoja
kati ya Misri na Syria ulikuwa mnamo Februari 1958 chini ya jina la Jamhuri ya
Kiarabu. alichukua urais baada ya Rais wa Syria Shukri al-Quwatli kuteremka, lakini
ilidumu sio zaidi ya miaka mitatu.
Nasser pia aliunga mkono mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa
na waasi wa jeshi yaliyoongozwa na marshal Abdullah al-Sallal kule Yemen mnamo
1962 dhidi ya ufalme wa maimamu, ambapo Nasser alituma askari wapatao elfu 70
wa Yemen kwenda Yemen kupinga ufalme huo, ulioungwa mkono na Saudi Arabia.
Alisaidia pia Harakati ya Mapinduzi ya Tamoz 1958 nchini Iraq, ikiongozwa na
jeshi la Iraqi, kwa kuungwa mkono na vikosi vya kisiasa vya umoja wa kitaifa
ili kupindua kifalme mnamo tarehe ya 14 Julai 1958.
Jukumu la mwisho wa
Abd El-Nasser lilikuwa kuelekeza mgawanyiko wa hafla ya matukio ya
Septemba Mosi huko Jordan kati ya serikali ya Jordan na mashirika ya Palestina
kwenye Mkutano wa Kairo mnamo Septemba 26 hadi 28,mwaka wa 1970.
Gamal Abdel Nasser aliinua kauli mbiu ya kile
kilichochukuliwa kwa nguvu hakirudishwi bila nguvu baada ya kusitishwa kwa Juni
1967 na kuchukua jukumu zuri katika kurudisha roho ya wanajeshi wa Misri,
ambayo ilipigana vita kali wakati wa vita vya kuvutia ... Hatima haikumpa
Nasser kuona mashujaa wa jeshi la kimisri wakivuka Mfereji wa Suez na
kushangilia pazia Wanavunja mpaka kwenye mstari wa Bar-Barlief na kurudisha ardhi inayopendwa ya Sinai,
pamoja na Heshima ya kimisri na kiarabu.
Mwisho na Maisha ya milele
Licha ya kifo chake mnamo Septemba 28, 1970, jina lake bado
limeandikwa ndani ya mioyo na akili za Wamisri na Waafrika kama ushahidi wa
kuonekana kwa picha zake katika Mapinduzi ya Januari baada ya karibu miaka 41
ya kwenda kwake. Na sera yake iliendelea khasa baada ya kuigiza mhusika wake
katika Senima na Runinga nasi tunataja hizi ;
Nasser miaka 56 mwaka wa 1995 Uagizaji wa nyota "Ahmed Zaki", filamu ya Jamal Abdel Nasser mnamo mwaka 1999 akiigiza
"Khaled El Sawy", mfululizo wa kimapenzi Faris mnamo 2003 kuhusu
maisha ya Youssef Sibai anaigiza nyota "Mohamed Riad", safu ya Nasser
ya mwaka 2008 yenye kichwa "Magdy Kamel".
Katika vitabu vingi, amebakisha kwa milele :
"Mijadiliano ya Nasser wa Riad Sidawi mnamo 1992, Gamal Abdel Nasser mbali
na siasa na Mustafa Badr mnamo 2001, na riwaya ya Mawlana" Sura ya sita
"iliyoitwa na Mohamed El-Aoun mnamo 2010 na Siasa kwa mwandishi Mustafa
Badb mwaka wa 2001..
Thamani yake imekua ndani ya mioyo na dhamiri za watu wote
wa bure wa kikoloni wanaokataa fedheha na unyanyasaji hadi leo..wamisri bado
wanamkumbuka wakati wanaadhimisha kila mwaka Mapinduzi takatifu ya Julai, na
Waafrika bado wanampenda wakati ambapo
jina la Misri hutajwa katika hafla yoyote.
Comments