Mahmoud Al-Khatib au "Bebo" ni mpenzi wa wamisri

Yeye ni mmoja wa wachezaji bora zaidi na maarufu wa mpira wa miguu waliojulishwa kwa viwanja vya Kimisri katika historia zake zote.

Alicheza kwa klabu ya soka ya Al-Ahly na  timu ya Misri.hivi  sasa yeye ndiye rais wa klabu ya kimisri Al Ahly tangu Desemba 1, 2017.

 

Mahmoud Ibrahim Ibrahim Al-Khatib alizaliwa kwenye mji wa Sinbillawin katika mkoa wa Dakahlia Oktoba 30, 1954.

 

mwenendo wake wa kitaaluma ..

 

Al-Khatib alianza safari na soka kupitia lango la  klabu ya Al-Nasr.Alipokuwa na umri wa miaka 15, alikuwa maarufu katika uwanja wa mpira wa miguu hasa wakati wa ushiriki wake katika ligi ya shule pamoja na shule ya kimichezo.

 

wakurugenzi wa klabu ya Al-Nasr walikubali kuhamisha Al-Khatib kwa Al-Ahly mnamo alikuwa karibu sana kotoka  kusaini  kwa Ismaili. Wakati huu Al-Khatib alikuwa na umri wa miaka 16. Mechi ya kwanza ya al-Ahli dhidi ya  timu ya klabu ya klabu yake ya zamani  ya ELNASR  ,naye alikuwa chini ya  umri wa miaka 18.

Safari yake pamoja na klabu ya Al Ahly kama mchezaji:

 

- Mahmoud Al-Khatib alipanda timu ya kwanza katika klabu ya Al-Ahly na alicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya klabu ya plastiki mnamo Oktoba 15, 1972. Katika mechi hiyo alifunga goli lake la kwanza na baada ya goli la plastiki yaliyoingia magoli mengi katika ligi mpaka alipofikia siku ya kustaafu kwa magoli 108 katika michuano ya ligi aliyafunga katika michezo 199 mnamo miaka 17 ya mfululizo wa kucheza.

Safari yake na timu ya kimataifa:

 

El- Khatib alicheza kwa mara ya kwanza na Misri mwaka wa 1974 na kushirikiana na mafarao katika michezo ya Olimpiki ya 1980 na 1984. Katika toleo la Los Angeles, alifunga goli zuri zaidi katika mechi ya Misri iliyoishinda kwa 4-1 juu ya kosta Rika, ambayo ilitoa Misri tiketi ya usafiri kwa duru ya pili kwa mara ya kwanza tangu Tokyo mwaka 1964.

Kuondoa ..

 

Alistaafu kimataifa mwaka 1986, baada ya kuongoza timu ya kimataifa kushinda michuano iliyoandaliwa na Misri.

Na ndani .. Mechi ya Al Hilal ya kisudan katika fainali ya ligi ya Mabingwa Ijumaa mnamo 15 Desemba 1987,kama

Mechi ya mwisho ya El-Khatib ili kuagana na "mashabiki wa Bebo"  na kutangaza kustaafu kwake kucheza kwa kudumu.

Hatua zake za kiidara pamoja na Klabu ya Al Ahly...

Ilikuwa hatua ya kiidara yenye mafanikio makubwa, ambapo alitaratibu katika shughuli za Idara kwenye Klabu ya Al Ahly, na alikuwa na cheo cha Mwanachama wa uongozi wa klabu ya AlAhly, kabla ya kupata cheo cha Naibu wa Rais  wa Ngome nyekundu.

 

Mnamo tarehe ya kwanza, mwezi wa 12 mwaka wa 2017,alichaguliwa Rais wa Klabu ya AlAhly baada ya Mhandisi Mahmoud Taher.

 

Tuzo na Lakabu...

Mnamo miaka ya kucheza kwake pamoja na mashetani wekundu, Elkhatib alipata lakabu 10 kwa Ligi, na makombe matano ya kimisri. Pia yeye aliainisha historia katika mashindano  ya kibara wakati ambapo alifunga magoli 37 katika mechi 49, nayo ni idadi ajabu lisilopitwa hadi sasa toka yeyote, na baada ya zaidi ya miaka 30 toka kustaafu kwa Bibo, AlAhly ilipepea michuano ya kombe la Afrika kwa klabu (Ligi ya Mabingwa wa Afrika hivi sasa)  1982,1987, na kombe  kuu la kiafrika mnamo miaka ya 1984,1985,1986.

 

Alipata lakabu ya "Mfungaji bora wa kwanza wa AlAhly" misimu minane toka 1973 hadi 1981 hakuna mwengine kama yeye ila Gamal Abd Elhamid katika msimu wa 1978 na 1979 kwa magoli saba kwa kila mmoja.

 

Alipata lakabu ya "Mfungaji wa ligi mara mbili "

Ya kwanza ilikuwa katika msimu wa 1977,1978 kwa magoli 11 na aliikariri katika msimu wa 1980,1981 kwa magoli hayo hayo.

 

Aliingia klabu ya MIA alipopambana na Teke aliyoiweka katika wavu wa Saleh Mahmoud "Golikipa wa ELKROM " lililosababisha ushindi wa ALAHLY kwa magoli matatu kwa goli moja,  na baadaye alifunga goli lake la 101 katika wavu wa ELZAMALEK.

 

Alipata tuzo la mchezaji bora barani Afrika kwa mwaka 1983.

Na kulingana na yaliyotajwa toka "Frans Football" katika tarehe ya 3 mwezi wa Januari mwaka wa 1984 kwa mnasaba wa idadi iliyotolewa kwa tuzo, Mjumbe wa Gazeti toka Kairo alisema kwamba : nasisitiza kwa wote  kwamba ni ngumu kwa Kairo au kwa Misri nzima kupata mchezaji wa Soka mwenye kipaji na mhusika kama Mahmoud Elkhatib".

 

Katika mwaka wa 1987 alichaguliwa kwa Shirikisho la kitaifa la Soka ili kupata tuzo la kucheza kuzuri ulimwenguni, ambapo Elkhatib alicheza zaidi ya mechi 450 za kirafiki na kirasmi, sawa na timu ya Misri au klabu ya ElAHLY naye hakupata ila mwonyo mmoja.

Comments