Mchezaji wa mweleka wa Kimisri wa Olimpiki
Mwenye idadi kubwa zaidi ya medali, muhimu zaidi ni medali
ya kidhahabu kwa juhudi yake mjini Athene, na ambayo umaarufu wake umekua baada
ya ufuzu wake kwa medali hiyo kwa kiasi kikubwa.
Kuzaliwa :
Karam Gaber amezaliwa siku ya kwanza, mwezi wa Septemba,
mwaka wa elfu moja mia tisa sabini na tisa katika mtaa wa Almansheya, mjini
Aleskandaria , ambapo amehitimu kutoka taasisi ya kifundi ya kibiashara.
Njia yake :
Karam Gaber ameanza kazi yake na mchezo wa mweleka na umri
wake hauzidi miaka kumi na saba katika kituo cha vijana cha Alobour, na
ameshiriki katika michuano ya kwanza katika maisha yake mwaka wa elfu moja mia
tisa themanini na tisa, michuano hiyo imekuwa kwa vijana inafuatia mkoa wa
Aleskandaria, na uzito wake umekuwa kilogramu 26 katika wakati huo, baadaye
amekwenda kituo cha vijana cha Alnasr ili kufanya mazoezi ya michezo hiyo,
ambapo katika wakati huu ameshinda kwa michuano zote za kijamhuri amezozishirikia.
Karam Gaber ameendelea katika kituo cha vijana cha Alnasr
kwa muda wa miaka tano, kabla ya kwenda kwake kwa klabu ya Olimpiki, ambayo ni
mojawapo ya klabu kubwa zaidi za Kimisri, kupitia klabu ya Olimpiki amefika
ulimwenguni kutokana na mtaalamu wa marehemu wa Armenia ( yehia kazaryan ),
ambaye amekufa mwaka wa elfu mbili na mbili, ambapo kocha wa Armenia amemunga
kwa timu ya kitaifa, mwaka wa elfu moja mia tisa tisini na tano, na amefanya
kumzoeza kwa uangalifu wa kipekee, na amemfanya na uzito wa kifunda, kisha
amemsukuma kwa ngazi ya kimataifa ili mchezaji anaanzia kushinda kwa medali na
michuano tangu mwaka wa elfu moja mia tisa tisini na saba.
Mashindano :
Gaber amekuwa na ufundi nzito katika mchezo wa mweleka tangu
ujana wake na amehakikisha michuano zote za Kimisri katika makundi tofauti ya
kiumri, na ujuzi wake umeongezeka baada kujiunga kwake kwa timu ya kitaifa,
ambapo baada ya kipindi kifupi ameweza kushinda kwa medali ya kidhahabu kwa
michuano ya vijana wa kiarabu nchini Syria katika uzito wa kilogramu 96, mwaka
wa elfu moja mia tisa tisini na saba.
Na katika mwaka huo huo amehakikisha mafanikio mengi ikiwa
ni pamoja na medali ya kidhahabu ya michuano ya kimataifa ya Beirut katika
uzito wa kilogramu 96, medali ya shaba ya mashindano ya michezo ya bahari
nyeupe ya Kati nchini Italia katika uzito wa kilogramu 85 na medali ya shaba ya
michuano ya dunia kwa vijana nchini Finland katika uzito wa kilogramu 96, pia
Gaber ameshinda medali ya kidhahabu ya michuano ya Afrika mjini Cairo katika
uzito wa kilogramu 97 mwaka wa elfu moja mia tisa tisini na nane, katika mwaka
huo huo ameshinda medali ya shaba ya michuano ya dunia kwa vijana mjini Cairo
katika uzito wa kilogramu 96, medali ya shaba ya michuano ya tuzo kuu kwa
mchezaji wa mweleka ( Ibrahim Mustafa) katika uzito wa kilogramu 97 na medali
ya kidhahabu ya mashindano ya (Fahmy Amry) nchini Uturuki katika uzito wa
kilogramu 97.
Katika mwaka wa elfu moja mia tisa tisini na tisa ameshinda
kwa medali ya kidhahabu ya mashindano ya michezo ya Kiafrika katika mji mkuu wa
Afrika Kusini, (Johannesburg) katika uzito wa kilogramu 97.
Na katika mwaka wa elfu mbili ameshinda kwa medali ya
kifedha kwa michuano ya tuzo kuu (Ibrahim Mustafa) katika uzito wa kilogramu
97, katika mwaka huo huo ameshinda kwa medali ya kidhahabu ya michuano ya
Kiafrika nchini Tunisia katika uzito wa kilogramu 97.
Na amepatia medali ya kidhahabu ya michuano ya dunia kwa
mabara katika uzito wa kilogramu 97, tuzo ya bora zaidi, mwaka wa elfu mbili na
moja, katika mwaka huo huo amepatia medali ya kidhahabu ya michuano ya
Uhispania ya kimataifa na kombe la mchezaji wa mweleka bora zaidi katika uzito
wa kilogramu 97, na medali ya kidhahabu ya michuano ya kimataifa ya Austria na
kombe la mchezaji wa mweleka bora zaidi katika uzito wa kilogramu 97, pia
medali ya kidhahabu ya michuano ya tuzo kuu (Ibrahim Mustafa) katika uzito wa
kilogramu 97.
Mwaka wa elfu mbili na moja umekuwa mwaka wa ongezeko la
umaarufu wa mchezaji wa mweleka wa Kimisri (Karam Gaber), ambapo ameshinda kwa
medali ya kidhahabu katika michuano ya kiarabu iliyofanyika nchini Syria katika
uzito wa kilogramu 97 na medali ya kidhahabu ya mashindano ya michezo ya bahari
nyeupe ya Kati nchini Tunisia katika uzito wa kilogramu 97.
Gaber amehakikisha michuano ya pili mfululizo katika
mashindano ya kiarabu baada ya kufuzu kwake kwa medali ya kidhahabu katika
michuano iliyofanyika nchini Qatar katika uzito wa kilogramu 96, mwaka wa elfu
mbili na mbili, katika mwaka huo huo ameshinda kwa medali ya kidhahabu ya
michuano ya Kiafrika iliyofanyika mjini Kairo katika uzito wa kilogramu 96, na
medali ya kidhahabu ya michuano ya dunia kwa mabara na kombe la mchezaji wa
mweleka bora zaidi katika uzito wa kilogramu 96 kwa mwaka wa pili mfululizo.
Pia amepatia medali ya dhahabu ya kombe la dunia kwa watu
wazima na medali ya kidhahabu ya michuano ya tuzo kuu (Ibrahim Mustafa) katika
uzito wa kilogramu 96 kwa mwaka wa pili mfululizo pia.
Gaber ameshinda kwa medali ya kidhahabu ya michuano ya
(David sholtz) nchini Marekani, mwaka wa elfu mbili na tatu, pia ameshinda kwa
medali ya kifedha katika michuano ya dunia ya arobaini na nane iliyofanyika
nchini Ufaransa na ameshinda kwa medali ya kidhahabu katika uzito wa kilogramu
96 katika michuano ya ( ptlasensky) nchini Poland mnamo wa kipindi kutoka siku
ya 22 hadi siku ya 24, mwezi wa Agosti, mwaka wa elfu mbili na tatu.
Pia amepatia medali ya kidhahabu katika mashindano ya
michezo ya Kiafrika iliyofanyika mjini Abuja, nchini Nigeria mnamo wa kipindi
kutoka siku 2 hadi siku ya 15, mwezi wa Oktoba, mwaka wa elfu mbili na tatu
katika uzito wa kilogramu 96, na kupitia michuano hiyo amefikia mashindano ya
michezo ya Olimpiki mjini Athene.
Pia amefuzu kwa medali ya kidhahabu katika mashindano ya
michezo ya Olimpiki mjini Athene, mwaka wa elfu mbili na nne katika uzito wa
kilogramu 96.
Comments