Umoja wa Afrika

Shirika la Umoja wa Afrika

Mnamo 25 Mei mwaka 1963 huko Adis Ababa nchini Ethiopia , mataifa 32 ya kifrika yaliyopata uhuru wakati huo yalikubaliana kupata Shirika la Umoja wa Afrika, Wajumbe 21 wamejiunga hatua kwa hatua, kufikia jumla ya Nchi 53 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika mnamo 2002. Mnamo 9 Julai mwaka 2011,Sudan Kusini ikawa mshiriki wa 54 wa Umoja wa Afrika. Malengo makuu ya Shirika la Umoja wa Afrika, Kama ilivyoainishwa katika Hati ya shirika la Umoja wa Afrika (OAU), ilikuwa kukuza umoja na mshikamano kati ya Mataifa ya Afrika. Kuratibu na kuzidisha ushirikiano na juhudi za kufikia maisha bora kwa watu waafrika ; kudumisha uhuru na uadilifu wa nchi Wanachama;Kukuza ushirikiano wa kimataifa ndani ya mfumo wa Umoja wa Mataifa, Wanachama wa Jimbo la kisiasa, kidiplomasia, kiuchumi, kielimu, kitamaduni, afya, sera za kijamii na kisayansi Kiufundi na ulinzi.

      Shirika la umoja wa Afrika linafanya shughuli  kwa msingi wa mkataba wake na mkataba wa Kuanzisha (Jumuiya ya / kikundi cha ) Uchumi wa Kiafrika (inayojulikana kama Mkataba wa Abuja) mnamo mwaka 1991. Vyombo vyake vikuu ni Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali, Baraza la Mawaziri na Sekretarieti na Tume ya Upatanishi, Ushirikiano na Usuluhishi. Kamati ya Uchumi na Jamii. Kamati ya Afya ya Kamati ya Elimu, Sayansi na Utamaduni na Ulinzi. Kamati ya upatanishi na usuluhisho ilibadilishwa kwa namna ya  kuzuia migogoro mnamo mwaka 1993.

 

Kuelekea Umoja wa Afrika:
       Mnamo miaka ya tisini, viongozi walijadili hitaji la kurekebisha muundo wa shirika la umoja wa Afrika ili kuonyesha changamoto za ulimwengu unaobadilika. Mnamo mwaka 1999,Wakuu wa Nchi na Serikali ya shirika la umoja wa Afrika walitoa Azimio la “Sirt”  la kutaka kuanzishwa kwa Jumuiya mpya ya Afrika. Maoni ya Muungano yalitegemea shughli ya Shirika la Umoja wa Afrika kupitia kuanzishwa kwa kiini kinachoweza kuharakisha mchakato wa ujumuishaji barani Afrika, Kusaidia na kuwezesha nchi za Kiafrika katika uchumi wa dunia na shughulikia shida nyingi za kijamii, kiuchumi na kisiasa zinazolikabili bara hilo Kwa ujumla, mikutano minne ilifanyika kabla ya uzinduzi rasmi wa Jumuiya ya Afrika:
- Mkutano wa Sirt (1999), uliopitisha Azimio la Sirt na mwito wa kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika.
- Mkutano wa Lomi (2000), uliopitisha Sheria ya Jumuiya ya Umoja wa Afrika.
- Mkutano wa Lusaka (2001), ulioandaa ramani ya barabara ya utekelezaji wa Jumuiya ya Afrika.
- Mkutano wa Durban (2002), uliozindua Jumuiya ya Afrika na ulifanya Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa Nchi na Serikali.

      Idadi kubwa ya miundo ya Shirika la umoja wa Afrika imejumuishwa katika Jumuiya ya Afrika (Umoja wa Afrika), na vile vile, ahadi nyingi za kimsingi za shirika la umoja wa Afrika, maamuzi na mfumo wa mkakati zimeendelea kuunda sera za umoja wa Afrika. Ingawa mwenendo wa shirika la umoja wa Afrika unabaki kuwa na nguvu, Sheria ya Jimbo la Jumuiya ya Afrika na Itifaki ilisababisha idadi kubwa ya muundo mpya. Wote katika kiwango cha vyombo vikubwa au kupitia kikundi cha kamati mpya za kiufundi na ndogo, nyingi zilizotoka tangu 2002 na zingine bado ziko chini ya maendeleo. Lugha chini ya Kifungu cha 11 cha Itifaki ya Sheria ya Jumuiya ya Afrika, Lugha rasmi ya Jumuiya ya(Umoja wa)  Afrika na taasisi zake zote zitakuwa Kiarabu, Kiingereza, Ufaransa, Kireno, Kihispania, Kiswahili na lugha nyingine yoyote ya Kiafrika. Lugha za kufanya kazi za Umoja wa Afrika ni Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa na Kireno.

Alama za Umoja wa Afrika

      Nembo ya Umoja wa Afrika ina mambo manne. Majani ya mtende pande zote za mzunguko kwa ishara ya amani. Mzunguko wa dhahabu inawakilisha utajiri na mustakabali (siku zijazo) nzuri ya Afrika.Ramani ya Afrika bila mipaka kwenye mzunguko wa ndani inamaanisha umoja wa Afrika. Pete ndogo nyekundu zinazoingiliana kwenye msingi wa mfano zinaonyesha mshikamano wa Afrika na damu iliyomwagika kwa ukombozi wa Afrika.

Bendera ya sasa ya umoja wa Afrika  ilipitishwa mnamo Juni 2010 katika Kikao cha 12 cha Kawaida cha mkutano wa wakuu wa nchi. mfumo ni ramani ya bara la Afrika kwa rangi la kijani kibichi juu ya Jua kwa rangi la nyeupe, limezungukwa na mzunguko wa nyota 54 zenye dhahabu na shamba la kijani kibichi. Rangi la kijani ni mfano wa tumaini barani Afrika, nyota zinawakilisha Nchi Wanachama wa Jumuiya ya(umoja wa) Afrika.  

Pili: Vyombo vya Umoja wa Afrika:

1-    (Mkutano wa kilele):

       Mamlaka ya juu zaidi ya Muungano yana Wakuu wa Nchi, Serikali au wakilishi wao, na hukutana angalau mara mbili mnamo mwaka.

      Rais wa nchi au Serikali anaongoza mkutano huo baada ya mashauriano kati ya nchi wanachama kwa kipindi cha mwaka mmoja.Hasa kati ya mikoa mitano ya Afrika (Kaskazini / Kati / Magharibi / Mashariki / Kusini), mada kuu hutambuliwa kwa kila mkutano.

​​​                                                                                                   

2-     Baraza la Utekelezaji (EC):

      Linalokuwa na  mawaziri wa nje au mawaziri wowote walioteuliwa na serikali zao.

      Kwa Kawaida hukutana mara mbili kwa mwaka katika vipindi viwili vya kawaida, hukutana katika vikao si kwa kawaida kwa ombi la Jimbo Mwanachama na kwa idhini ya theluthi mbili ya wanachama.

3-     Kamati ya Wakilishi ya Kudumu (PRC):

       iko na mabalozi au wakilishi wa kudumu waliokubaliwa katika Umoja huo, Inawajibika katika kuandaa kazi ya Halmashauri(baraza la utekelezaji),mwongozo wake,Inaweza kuunda kamati ndogo au vikundi vya kufanya kazi kama inahitajika.

4-    Bunge la Afrika (PAP):

      Sheria ya Katiba ya Jumuiya ya(umoja) Afrika ilianzisha Bunge la -Pan-Afrika kama chombo cha Jumuiya ya Afrika ili kuhakikisha ushiriki kamili kwa watu waafrika katika maendeleo na ujumuishaji wa bara hilo.

5-    Tume ya Umoja wa Afrika (AUC):

       Kuzingatiwa kama Sekretarieti Kuu au Sekretarieti ya Muungano, ina Rais, Makamu wa Rais na Makamishna 8 wanaowajibika kwa masuala yanayohusu amani na usalama na masuala ya kisiasa,Miundombinu, nishati, masuala ya kijamii, rasilimali watu, sayansi na teknolojia, biashara na tasnia, uchumi wa vijijini na kilimo, na masuala ya kiuchumi, kila mmoja wa wajumbe wa Tume anachaguliwa kwa muda wa miaka minne, mbadala mpya mara moja.

      Tume ya sasa ya Tume ya umoja wa Afrika, iliyoongozwa na Rais wa Chadi Moussa Fakih Ahmed, ilichaguliwa wakati wa Mkutano wa Adis Ababa (Januari 2017).Ni shirika la nne kusimamia Tume ya AU tangu kuanzishwa kwake,Dokta Amani Abu-Zeid ni Kamishna wa Miundombinu na Nishati wa Misri.

6-     Kamati za Ufundi maalumu (STCs):

      Kamati kumi nan ne(14), muhimu zaidi kuwa Kamati ya Ulinzi, Usalama na Amani, Kamati ya uhamiaji, wakimbizi na watu waliohamishwa ndani,Kamati ya Masuala ya Fedha, Mipango ya Uchumi na Ushirikiano, Kamati ya uhamiaji, wakimbizi na watu waliohamishwa ndani, Kamati ya Pamoja ya Bara na Uchukuzi na Miundombinu ya Mkoa,Nishati na utalii.

      Lengo la kamati maalumu ni kupunguza idadi ya mikutano ya mawaziri kwa kuunganisha mikutano kadhaa ya mawaziri katika kamati maalumu ya ufundi.

7-    Baraza la Kiuchumi, kijamii na kiutamaduni (ECOSOCC):

      Baraza linalenga kusaidia na kuhimiza mazungumzo na uongozi kati ya watu wa Kiafrika juu ya masuala muhimu kadhaa na kuhakikisha ushiriki mzuri wa watu wa Kiafrika katika utekelezaji na tathmini ya mipango ya umoja wa Afrika. 

8-    Taasisi za Fedha:

      Jumuisha Mfuko wa Fedha wa Afrika,benki ya Uwekezaji ya Afrika (Libya) na Benki Kuu ya Afrika (Nigeria).

9-    Taasisi za haki za binadamu:

Tume ya Afrika juu ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR):

Tume ya Afrika juu ya Haki na Ustawi wa Mtoto

 

10- Baraza la Amani na Usalama (AU-PSC):
      Limeanzishwa  mnamo 2004, maamuzi yake yanafaa kwa Mataifa yote ya Jumuiya ya (umoja wa) Afrika.
      Limeundwa na washiriki kumi na tano(15), kumi(10) waliochaguliwa kwa miaka mbili na watano kwa miaka mitatu, Kwa msingi wa kuzungusha kulingana na kanuni ya uwakilishi wa jiografia ya bara.

11- Taasisi za Sheria: 
Baraza  la Ushauri juu ya Rushwa:
      Lilianzishwa mnamo 2006 chini ya Ibara ya 22 ya “Mkataba wa Jumuiya ya(umoja wa) Afrika dhidi ya Ufisadi”, kwa lengo la kuimarisha, kupitishwa na utekelezaji wa hatua za kupambana na ufisadi (rushwa) katika bara hilo na kushauri serikali juu ya jinsi ya kushughulikia ufisadi katika sheria zao za kitaifa.

Tume ya umoja wa Afrika ya sheria ya kimataifa (AUCIL):


      Tume ya Afrika juu ya sheria ya kimataifa ilianzishwa mnamo Februari 2009 kwa mujibu wa mfumo msingi wa tume ya sheria ya kimataifa ya Jumuiya ya(umoja wa) Afrika kama tume huru ya ushauri iliyopewa ili kufuata maendeleo katika sheria za kimataifa.

 

Orodha ya Marais wa Jumuiya ya Afrika :

Mwenyekiti

Mwisho wa muhula wa  uongozi

Mwanzo wa muhula wa uongozi

Nchi

Abd-El Fatah El-Sisi

-

Februari 2019

Misri

Paul Kagame

Februari 2019

Januari 2018

Rwanda

Alpha Konde

Januari 2018

Januari2017

Guinea

Idriss Deby

Januari 2017

Januari2016

Chad

Robert Mugabe

 

Januari2016

Januari2015

Zimbabwe

Mohamed Wld Abd-El Aziz

Januari2015

Januari 2014

Mauritania

Hailemariam Desalegn

Januari2014

Januari 2013

Ethiopia

Yayi Boni

Januari 2013

Januari 2012

Benin

Teodoro Obiang Nguema Mbasog

Januari 2012

Januari2011

Guinea Kitropiki

Bingu wa Mutharika

Januari2011

Januari2010

Malawi

Muammar Qadhafi

Januari 2010

Februari2009

Libya

Jakaya Kikwete

Januari2009

Januari 2008

Tanzania

John Kufuor

Januari2008

Januari2007

Ghana

Denis Sassou Nguesso

Januari2007 

Januari2006

Congo

Olusegun Obasanjo

Desemba 2005

Julai 2004 

Nigeria

Joaquim Chissano

Julai 2004

Julai 2003

Mozambique

Thabo Mbeki

Julai 2003 

Julai 2002

Afrika Kusini

 

Comments