Abdou Saleh El-Wahsh

Mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu, kocha, Mwenyeketi wa zamani wa timu ya Al-Ahly, meneja wa kiufundi wa timu ya Misri katika miaka ya Themanini, meneja wa kiufundi wa umoja wa kiafrika wa mpira wa miguu na mwalimu wa kimataifa.

 Kuzaliwa

 Abdou Saleh El-Wahsh amezaliwa tarehe ya 9 mwezi wa tano mwaka wa 1929.

 

Maisha yake

Mnamo mwaka 1963 amesafiri kwa Kuwait kama mkaguzi katika wizara ya malezi na elimu na kocha wa timu ya Kuwait kwa miaka mitano na wakati aliporudi alifanya mazoezi kwa  timu ya Alahly kwa miaka miwili.

 

Aliongoza klabu ya Al-ahly kutoka mwaka 1988 hadi mwaka1992.

 

Alijiunga na shirikisho la Afrika kama meneja wa kiufundi. Na kutoka mwaka 1982 uhusiano wake na shirikisho la kimataifa umeanza. Na kutoka mwaka 1985 ameanza Kuweka mipango yote kwa makocha wa Afrika katika shirikisho la kiafrika na ameendelea kwa miaka kumi na tatu na hasa hadi mwaka 1998.

 

Amekuwa Mwenyeketi wa shirikisho la mpira wa miguu wa muda katika mwaka 2000. Alwahsh  Amzingatiwa  kiongozi wa mazoezi ya chuo kikuu katika nyumba ya kiarabu na mmoja wa wataalamu nane katika kamati ya kiufundi ya shirikisho la kimataifa la mpira wa miguu "FIFA".

 

Kifo chake

Abdou Saleh El-Wahsh alikufa tarehe ya 21 mwezi wa tano mwaka wa 2008.

Comments