" Utaifa wa kiafrika bila ya Umoja wa kiafrika wa kweli utakuwa bure, mwenye hatari, na wakati hautauulizwa"
Ile ni kauli ya rais mtanzania "Julius Nyerere" kama ilipatikana kwenye kitabu cha" Robert Emerson- kwa Umoja wa kiafrika", katika mwaka wa 2009.
"Julius Kambrake Nyerere "mwenye lakabu ya baba wa Taifa", alizaliwa katika mwezi wa Machi(3), mwaka wa 1922, kutokana na kabila la "Zanki", kwenye kijiji cha"Butyama", kutokana na familia ya kabila linalofanya kazi ya Ufugaji, na baba yake ni kiongozi wake, alikufa mwezi wa Oktoba(10), mwaka wa 1999, pia yeye ni baba kwa wavulana watano na wasichana wawili, alijulikana kwa Uaminifu na Uongozi, aliitwa kwa" Mwalimu", na "Mwanafunzi wa nchi yake na Mwalimu wake. "
Alifanya kazi ya kufundisha baaya ya kupata daraja la masomo ya juu toka Uingereza, kisha aliunda chama cha "TANU" kwa lengo la Uhuru wa Amani kutokana na siasa ya Ukoloni -inayoshangilia Uongozi wa kimakabila- unaowakilisha katika siasa ya Ubaguzi na Utenganisho, na katika mwaka wa 1961 alikuwa waziri mkuu wa Tanganika baada ya kupata Uhuru wake, na baada ya miaka miwili, Zanzibar ilipata uhuru wake pia, na katika 1964 Umoja wake pamoja na Tanganika ulitangazwa chini ya Jina la nchi ya Tanzania, na Nyerere alikuwa rais wake, kisha aliacha Urais mwaka wa 1985.
Yeye ni mmoja wa wakubwa wanaoita Umoja wa kiafrika, na mmoja miongoni mwa viongozi wa harakati ya uhuru wake kutoka Ukoloni katika miaka ya 60 na 70, ni mmoja wa waanzishi Taasisi la umoja wa kiafrika - Umoja wa kiafrika hivi sasa- nao ulioundwa baada ya mwaka mmoja wa mapendekezo ya ( mkutano wa Adis Ababa) mnamo mwezi wa Mei(5), mwaka wa 1962,ambapo alipozungumzia Akisema" tunauamini Umoja wa kiafrika sawa ni Imani kwa Afrika lenyewe."
Inatajwa kwa Uongozi wake uliendelea kwa vipindi vinne vya Urais, mnamo vyake alipata Uungaji mikono, Upendo, na Usaidizi kutokana na nchi yake, khasa matabaka ya nchi, na hayo kwa sababu ya kuwa na mtindo wa "Ujamaa ", na kwa maoni yake, Ujamaa ni mchanganyiko wa" Ujamaa wa kiutendaji" na "Utani wa kiafrika", pia katika mwaka wa 1992, aliruhusu kufanya mabadiliko kwenye Katiba nchini mwake;ili ziwe na nafasi ya kupata mifumo ya kisiasa na yenye vyama mbalimbali, na mnamo 1967, Tanzania iliingia katika Muungano wa nchi tatu za mashariki ya Afrika ulioitwa ( Umoja wa mashariki ya Afrika), na aliifanya lugha ya Kiswahili lugha rasmi ya nchi zake, na kupitia hayo, aliweza kuondoa na kupunguza tofauti katika makabila ya mashariki na katikati ya Afrika.
Alikuwa msomi, anayejali Fasihi ya Ulimwengu, alifasiri kwa lugha ya Kiswahili ( Mfanyabiashara wa Bunduki), (Julius Kaisar) kwa Shekespeer, pia ana vitabu vingi navyo ni kama: Uhuru na Umoja 1967, Uhuru na Ujamaa 1968, Uhuru na Maendeleo 1973. Linalosisitiza juu ya Imani yake kubwa kwa Ujamaa wa kiafrika na kwamba Elimu iwe kwa wote, nayo ni njia ya kuikomboa nchi.
Alikuwa na Urafiki adhimu sana pamoja na rais mmisri aliyekufa" Gamal Abd Elnaser ", kulingana na mradi wake nchini Tanzania unaofanana na mradi wa "Nasser " nchini Miari ambapo wote walibeba nembo ya "Ujamaa" na wao waliangalia mielekeo ya pamoja inayohusu masuala ya bara la Afrika na Masuala ya kitaifa, na mnamo mwaka wa 1964 bwana "Salem Ahmed Salem" aliainishwa kama Balozi wa kwanza kwa Tanzania nchini Misri, wakati wa Umoja kati ya Tanganika na Zanzibar.
Na bwana Nasser katika hotuba zake nchini Misri, alimsifu Nyerere kwamba ( yeye ni mwanafunzi wa nchi yake na mwalimu wake, naye ni mmoja wa waafrika adhimu mnamo zama zake), na mnamo ziara yake kwa Bunge aliisisitiza tena akasema:Nyerere ni kiongozi mgumu, shujaa, na mwaminifu, siyo kwa Tanzania tu wala kwa Afrika bali kwa Utu mzima", na inatajwa kwamba rais Nyerere alihuzunika sana kwa kifo cha rais mmisri Abd Elnaser, akasema:Kifo cha Abd Elnaser ni msiba mkubwa na hasara kubwa sana kwa Ulimwengu mzima, hata maadui wake watamhuzunika, yeye alikuwa mwanamume adhimu, baadaye alilia, na inayotajwa kwamba, ilikuwa mara ya kwanza ya kulia kwa Nyerere na ilionekana kwa watu.
Comments