Dokta Zahi Hawass

Mwanakiolojia ambaye alikuwa zamani waziri wa vitu vya kale, pia alikuwa katibu mkuu wa Baraza Kuu la Vitu vya Kale vya kimisri , na mkurugenzi wa vitu vya kale vya Giza.

  Kwa hivyo, aliitwa “ Mlenzi wa Mafarao”. Pia ana juhudi nyingi wazi katika njia ya ulinzi na kurudisha upya wa vitu vya kale, kuhifadhi urithi wa kitamaduni kimisri  na  kurejesha kile kilichotoka nje kwa njia haramu.

 Uzazi na Malezi,

 Alizaliwa mjini Damietta, kijiji cha Al-Ubeidiya mnamo Mei 28, 1947. Na alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Aleskandria, Kitivo Cha Sanaa. 

Ugunduzi wake wa kiathari,

 Aligundua  mengi muhimu ya kiathari, kama:

- Makaburi ya wajenzi wa piramidi.

- Bonde la masanamu ya kidhahabu.

- Kaburi la Mtawala wa  oasisi na familia yake mnamo umri wa Al-Sawy ( familia 26).

Machapisho yake,

 Ametunga vitabu vingi kwa kiarabu na kiingereza, na pia vilitafsiriwa kwa lugha nyingi, kama :

- Abu Simble….Mahekalu ya Jua wazi.

- Bibi wa ulimwengu  mkale.

- Muujiza wa Piramidi Kuu.

- Bonde la masanamu ya kidhahabu.

- Siri kutoka mchanga.

Pamoja na makala nyingi yaliyochapishwa katka magazeti na majarida ya kimataifa.

Ufundishaji,

 Dokta Zahi Hawass, amefundisha katika vyuo vikuu vingi, na alitoa mihadhara pia katika vyuo vikuu vingi vya ulimwengu, kama :

- Chuo kikuu  cha Los Angeles cha Marekani. 

- Chuo Kikuu cha Marekani mjini Kairo (AUC).


Tuzo na Heshima,

- Nishani ya Sayansi na Sanaa ya daraja la kwanza.

- Tuzo la kiburi la Misri katika uchunguzi wa chama cha waandishi wa kigeni nchini Misri mnamo mwaka 1998.

- Tuzo la ngao ya kidhahabu kutoka Chuo cha Marekani cha Mafanikio, mnamo mwaka 2000.

- Tuzo la Mwanasayansi mmisri wa kipekee kutoka Jumuiya ya Wanasayansi wa Kimisri huko Marekani.

- Na pia aliheshimiwa na Mkoa wa Damietta na chuo kikuu cha Al-Mansoura.

- Na alichaguliwa na gazeti la  The Times la kimarekani, miongoni mwa orodha ya wahusika 100 muhimu zaidi ulimwenguni.

- Pia alipata tuzo la “Emmy”, ambalo ni tuzo kubwa zaidi kwenye kiwango cha ulimwengu, linalopewa na Chuo cha Sanaa za Televisheni na vyombo vya habari huku Marekani. Ambapo, Dokta Zahy Hawas alipata tuzo hilo kwa ushiriki wake katika filamu kuhusu Tut Ankh Amun na Bonde la Wafalme, iliyotolewa kwa kipindi cha CBS, mnamo mwaka 2005.

Comments