"samaki wa kidhahabu wa Misri "
Mmisri wa kwanza anayepata rekodi ya kimataifa ya kuogelea
Farida Hesham Othman anayejulikana kwa jina la Farida
Othman, bingwa wa kuogelea wa kimataifa, mchezaji wa timu ya kitaifa ya Kimisri
na klabu ya Aljazera, ni msichana Mmisri amecheza kuogelea tangu utoto wake,
baba yake amekuwa daktari anapenda michezo kwa ujumla na anacheza mchezo wa
(water bolo) na huu ni mchezo wa mpira wa maji.
Kaka yake Ahmed Othman amekuwa anaelekea klabu ya Aljazera
ili kucheza kwa kuogelea kwa kifua, licha ya kukataa kwa baba yake kwa kujiunga
kwake katika timu ya klabu na kufanya mazoezi ya riadha kwa sababu ya udogo wa
umri wake lakini amekubali mwishoni, mama yake ni daktari wa meno (Randa
Al-Salawy) anamsaidia baba katika kuunga mkono kwa Farida juu ya michezo kupitia
kujali kwa ratiba ya mazoezi na ufuatiliaji wa kila wakati kwa kwenda kwa mtoto
na kurudi kwake kutoka klabu, baada ya kujaribu kwake kwa mchezo wa Ballet ya
maji, Farida ameamua kuzingatia kuogelea ambako anapenda, kuanzia hapa
ameangaza na ameonyesha talent yake kwa ulimwengu.
Farida amezaliwa mjini Indianapolis, nchini Marekani siku ya
18, mwezi wa Januari, mwaka wa 1995, yaani katika wakati wa kisasa anakuwa
mwenye umri wa miaka 25, ameishi nchini Misri kwa wazazi daktari wamisri
wamehitimu kutoka chuo kikuu cha Indiana mjini Indianapolis pia, mji mkuu wa
wilaya ya Indiana ya kimarekani, wao ni Randa Alsalawy na Hesham Othman, Farida
anamiliki kitambulisho cha Kimisri hadi sasa.
Farida ameanza kuogelea na kujihusisha katika riadha hiyo
tangu amekuwa mwenye umri wa miaka 4 katika klabu ya Aljazera pamoja na kaka yake
Ahmed, kisha ameacha kuogelea kwa muda maalum ili kucheza kwa Ballet ya maji.
Amerejea tena kwa kucheza riadha ya kuogelea na amekuwa
katika umri wa miaka 11, ameanza kuingia katika mashindano ameiwakilishi Misri
na anasafiri ili kufanya mazoezi na ushindani nje ya Misri kupitia klabu,
Farida alipofikia awamu ya shule ya
msingi amesoma katika shule ya Oasis ya
kifaransa mjini Kairo kisha amehamia
shule nyingine na hii ni shule ya lycee ya kifaransa inayofuata ubalozi
wa Ufaransa mjini Kairo.
Amejiunga chuo kikuu cha Marekani mjini Kairo na anataalam katika sehemu ya masomo ya
vyombo vya habari, hivi karibuni amesafiri ili kusoma uchumi katika wilaya ya
California ya kimarekani.
Mnamo mwaka wa 2006 talenta ya Farida katika kuogelea
imeanzia kuonekana, ambapo ameingia kwenye shindano lake la kwanza na hilo ni
mbio ya mita 50, mita 100 na amepatia nafasi ya pili katika kuogelea huru na
kipepeo, na amepita mita 200, na ameshinda kombe la michuano ya kimichezo kama
mwogeleaji bora zaidi wa michuano hiyo, alipokuwa mwenye umri wa miaka 12
ameshindana katika shindano linalojulikana kwa (Ban Arab) katika msimu wake wa
11, mwaka wa 2007, linalofanyika nchini Misri wakati huo, kama mwogeleaji mdogo
zaidi wa shindano la mita 50 na mita 100 ya kuogelea huru na kipepeo.
Katika shindano hilo, Farida amevunja rekodi katika mbio ya
mita 50 na amepatia nafasi ya tano, ambapo muda wa kuogelea kwake umekuwa
sekunde 28,95.
Na amefikia nafasi ya 6 ya kuogelea kipepeo kwa mbio ya mita
100.
Ameshiriki katika shindano la kimataifa la kuogelea
(shindelfingen) na anashinda nafasi ya pili, ambayo kupitia nafasi hiyo
anapatia kombe la michuano kama mshindani bora zaidi.
Alipokuwa na miak13
Farida amesafiri Marekani ili kukaa katika kambi la msimu wa joto ili kufanya
mazoezi miongoni mwa timu inayojulikana kwa (pear time) mjini Perekly wilaya ya
California ya kimarekani, wakati wa kipindi hicho ameshiriki katika michezo ya
Olimpiki ya vijana na amekuwa kutoka nafasi za 10 za awali katika timu yake ya
kuogelea.
Ameendelea shindano lake mnamo mwaka wa 2009 na amekuwa
mwenye umri wa miaka 14, na amecheza shindano la Muungano wa kimataifa wa
kuogelea, linalofanyika mjini Roma nchini Italia, na ameshinda nafasi ya 66
katika mbio ya mita 50 ya kuogelea huru kwa muda wa sekunde 26,77, katika mbio
ya mita 50 ya kipepeo ameshinda nafasi ya 50, ambapo muda wake wa kuogelea
umekuwa sekunde 27,78 na hivyo amekawa mwogeleaji wa haraka zaidi ulimwenguni
katika umri huo.
Katika mbio ya mita 100 ya kuogelea huru amehakikisha nafasi
ya 87 kwa muda wa sekunde 59,45.
Na katika kuogelea kipepeo amekuwa katika nafasi ya 64 na
amepita mbio kwa muda wa 1,03,21.
Katika mwaka huo huo, Frida ameshiriki katika shindano la
Afrika kwa vijana katika msimu wake wa 8 lililofanyika huko Mureshios nayo ni visiwa vinavyomo ndani
ya bahari ya Hindi, na ameshinda nafasi ya kwanza katika mbio ya kuogelea huru
ya mita 50 kwa muda wa sekunde 26.36, katika mbio ya kipepeo ya mita 50
amevunja rekodi kwa muda wa sekunde 27.60.
Farida ameshinda medali ya kidhahabu ya mbio ya mita 50 kwa
sababu ya kuogelea kwake katika muda wa kipekee umefika sekunde 31.04, na
ameshinda medali ya kifedha ya mbio ya mita 100 ya kuogelea huru kwa muda wa
sekunde 1.03.06, katika shindano lake la kibinafsi la mbio ya mita 100 amepatia
nafasi ya tatu, na kama mshiriki na mwogeleaji miongoni mwa timu ya Kimisri
amepata nafasi ya pili.
Ameshiriki katika shindano la Muungano wa kimataifa kwa kuogelea lililofanyika nchini Peru, mwaka wa
2011, Farida akawa bingwa wa ulimwengu wa vijana na amepatia nafasi ya tatu
katika mbio ya mita 50 ya kuogelea kipepeo, na amefikia muda wa kipekee wa
sekunde 26.69, pia amepatia medali ya kidhahabu na ameifanya Misri kuchukua
nafasi ya 11 katika orodha ya medali na hii ni nafasi kubwa zaidi ambayo
inafikiwa na nchi yoyote ya kiarabu au ya Kiafrika.
Farida hakutosha na hiyo, lakini amejiunga kwa klabu ya
washindi wa medali na ambayo hakuna mwogeleaji mmisri yeyote anayejiunga ndani
yake, mnamo mwezi wa Desemba, mwaka wa 2011 amecheza mashindano ya lakabu ya
mataifa ya kiarabu nchini Qatar.
mwaka wa 2012 katika kikao cha michezo ya msimu wa joto
kilichofanyika mjini London na Marekani, Amechaguliwa katika shindano la mita
50 la kuogelea huru pamoja na mwenzake Shehab Younes ili kuiwakilisha Misri, na
amekwisha kuogelea kwake kwa muda wa sekunde 26.34 na ameshinda nafasi ya 41
kwa masilahi ya Misri.
Mwaka wa 2013, Farida amefuzu kwa nafasi ya 24 ya mbio ya
mita 100 ya kuogelea kipepeo kwa muda sekunde 59.85 katika shindano la michezo
ya maji lililofanyika mjini Barcelona nchini Uhispania.
Siku ya tano amehakikisha nafasi ya 40 katika mbio ya mita
100 ya kuogelea huru kwa muda wa sekunde 59.85, pia katika siku ya sita
amepatia nafasi ya 11 katika mbio ya mita 50 ya kuogelea kipepeo kwa muda wa
sekunde 26.17, na amefikia fainali na ameshinda nafasi ya 7 katika shindano la
mita 50 ya kuogelea kipepeo kwa muda wa sekunde 26.17 katika mwezi wa Agosti,
mwaka wa 2013, na hiyo ni nafasi kubwa zaidi ambayo inafikiwa na Misri katika
historia ya mbio za kuogelea.
Farida amehakikisha mafanikio makubwa kama msichana mmisri na mwogeleaji mnamo mwaka wa 2015
katika shindano la Muungano wa kimataifa wa kuogelea kwa mara ya pili, na
ameshinda medali ya kidhahabu ya mbio huru, pia amepatia nafasi ya tatu katika
mbio ya mita 100 ya kuogelea huru, na amepatia medali ya kidhahabu ya
mashindano ya michezo ya Kiafrika yaliyofanyika mjini mkuu wa Congo,
Brazzaville, ambapo ameshindana katika mbio ya mita 50 kwa muda wa sekunde
25.12.
Mwaka wa 2016 Farida amepatia nafasi ya kwanza na medali ya
kidhahabu ya shindano la michuano ya chuo kikuu cha Marekani, ambapo amefika
kwa muda wa sekunde 21.32 na amehakikisha
Kuwa mshindani wa pili bora zaidi
duniani katika mbio ya mita 50 ya kuogelea huru.
Katika mwaka wa 2017, mwogeleaji mmisri Farida Othman
amehakikisha michuano yake ya kwanza (NCAA) pamoja na chuo kikuu chake cha
Marekani katika mbio ya mita 100 ya kipepeo, na ameshinda lakabu ya michuano
kwa mara ya kwanza, hiyo baada ya kushinda kwake kwa medali ya kidhahabu ya
mashindano ya 2017, na akawa mwogeleaji wa tatu mwepesi zaidi katika historia
ya mashindano, baada ya kushinda kwake kwa lakabu kwa muda wa sekunde 50.05,
kwa utofauti ya sehemu 4 kutoka sekunde kutoka mwenye nafasi ya pili.
Kwa namba hiyo, mwoga Mmisri ameweza pia kuchukua nafasi ya
7 kati ya wepesi zaidi katika historia ya mashindano ya kuogelea katika
michuano ya kimarekani, ambapo (Kelly worel) anachukua nafasi ya kwanza kwa
muda wa sekunde 49.43, na (Natalie Koglen) mwogeleaji wa pili mwepesi zaidi ya
mbio kipepeo kwa muda wa sekunde 50.01.
Farida Othman amehakikisha medali ya shaba ya michuano ya
dunia, mwaka wa 2017 iliyofanyika nchini Hungary kwa muda wa sekunde 25.39.
Ama katika mwaka wa 2018 mwogeleaji mmisri Farida Othman
amepatia medali tatu wakati wa kikao cha michezo ya bahari ya Kati kilichofanyika
nchini Uhispania, akihakikisha kwa hiyo mafanikio makubwa kwa riadha ya
Kimisri.
Farida Othman wakati wa kikao amehakikisha medali ya
kidhahabu ya mbio ya mita 50 ya kipepeo, na medali ya kifedha katika mbio ya
mita 100 ya kipepeo.
Mwogeleaji mmisri Farida Othman amefanikiwa kurudisha
mafanikio ya Rania Elwany ambaye ni bingwa wa kuogelea wa Kimisri kwa kushinda
kwake medali mbili za kidhahabu na medali ya kifedha katika mashindano ya kikao
cha michezo ya bahari ya Kati.
Katika kikao cha bahari ya Kati, mwaka wa 1997 mjini pari
nchini Italia, Rania Elwany amehakikisha medali mbili za kidhahabu za mbio za
mita 50 huru na mita 100 huru, huku ameshinda medali ya kifedha ya mita 200
huru.
Farida Othman amerudisha mafanikio kwa kuhakikisha medali mbili za kidhahabu za mita 50 huru na mita 50 ya kipepeo, pia ameshinda medali ya kifedha ya mita 100 ya kipepeo katika mashindano ya kikao cha michezo ya bahari ya Kati mjini Tarragona nchini Uhispania.
Na mnamo 2019 Farida Othman alishinda Medali ya shaba katika michuano ya dunia inayofanyika huko Korea Kusini.
Pia alishinda nafasi ya kwanza na medali ya kidhahabu katika mbio ya mita 50 kwa kipepeo mnamo muda wa sekunde 20 na sehemu 64 kutoka kwake, katika kikao cha michezo ya kiafrika huko Morocco naye alihakikisha rekodi mpya ya kiafrika ilisajiliwa kwa jina lake.
Pia alipata medali ya
kidhahabu katika mbio ya mita 100
kwa kipepeo baada ya kuhakikisha muda mpya katika kikao cha michezo ya
kiafrika, unaokadiriwa sekunde 58.79 tu. Alishinda medali ya kifedha ya mbio
huru ya mita 100 mnamo muda wa sekunde
55 na sehemu 62 kutoka kwake katika kikao hicho hicho.
Comments