Saleh Selim

Yeye ni mmoja wa maarufu zaidi katika historia ya klabu ya Al-Ahly na Mpira wa kimisri kwa jumla kwa zaidi ya nusu karne alibaki kati ya kuta za ngome nyekundu kama mchezaji, msimamizi na Rais wa klabu tangu alipojiunga na vijana wa klabu mnamo 1944 hadi kifo chake mnamo Mei 2002.

Kuzaliwa na ukuaji

 

Saleh Selim – aliyejulikana kwa jina la Maestro - alizaliwa mnamo Septemba 11 mwaka 1930,  mtaa wa Dokki.

Kipaji cha Saleh Salim na mpira kilionekana pamoja naye tangu utoto wake, ambapo alijiunga na timu ya Shule ya msingi ya Orman halafu alichaguliwa kama mwanachama wa timu ya shule za sekondari  wakati alikuwa mwanafunzi katika shule ya Saidia kabla ya kujiunga na klabu ya Al-Ahly mnamo 1944, na akafanikiwa haraka kuthibitisha kuwepo kwake na talanta yake hadi  alijiunga na timu ya kwanza na yeye alikuwa na miaka kumi na saba.

 

Njia  yake

 

Alicheza mechi yake ya kwanza na Al-Ahly  kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Al-Masry mnamo 1948. Al-Ahly ilishinda wakati huo 2-1 na Salim alifunga bao la ushindi. Mechi rasmi ya kwanza ilikuwa dhidi ya Yunnan Alexandria katika wiki ya tatu ya mashindano ya Ligi Kuu msimu wa 1948 na Al-Ahly ilishinda 2-0.

 

Tangu kushiriki kwake kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa kwanza wa mashindano ya ligi kuu nchini Misri, Saleh Selim alianza safari yake na umaarufu,  ambapo aliendelea na Al Ahly kwa miaka 19 kwenye viwanja hadi alistaafu kutoka kwenye mchezo huo mwishoni mwa 1966.Mechi yake rasmi  ya mwisho ya kucheza na Al Ahli ilikuwa dhidi ya Al-Tayaran mnamo Novemba 11, 1966.

 

Wakati wa njia yake na Al-Ahli, Saleh Salim alichangia mashindano 19 ya Al-Ahly, miongoni mwao ni ligi kuu 11 na Kombe 8. nyota wa Al-Ahly alifanikiwa kufunga mabao 78 katika mechi za ligi na 14 kwenye Kombe.

 

Saleh alianza njia yake na timu ya Misri mnamo 1950 na alikuwa kocha wa timu hiyo iliyoshinda Kombe la Mataifa ya kiafrika mnamo 1959 katika Kairo, na pia alishiriki na timu ya kitaifa kwenye kikao cha Michezo ya Olimpiki huko Roma mnamo 1960.

 

Saleh Selim anashikilia rekodi ya idadi kubwa zaidi ya mabao yaliyofungwa na mchezaji katika mechi mmoja wakati alifunga mabao saba ndani ya wavu wa klabu ya Ismaili kwenye mzunguko wa kwanza wa msimu wa 1958 na kumaliza mechi wakati huo Al-Ahli ilishinda kwa mabao manane safi.

 

Saleh Salim anabaki kutoka wachezaji wa kwanza ambao walikuwa wataalamu nje ya nchi , ingawa Hussein Hegazy na Mohamed Latif walikuwa na uzoefu mbele yake, lakini ilikuwa kwa masomo ya nje ya nchi, lakini nyota huyo wa zamani wa Al-Ahli alipokea ofa ya kitaalam katika safu ya Klabu ya Austria "Graz" Baada ya kuwa maarufu na kweli Saleh Salim ameamua kupata uzoefu wa utaalam katika Ulaya mnamo 1963, lakini haikudumu zaidi ya miezi minne baada ya kupata ugumu wa kukabiliana na maisha huko Ulaya wakati huo, ingawa alicheza mechi kali na klabu yake na alifunga mabao sita kwenye mechi mmoja wa ligi hadi wakati Mashabiki wa Austria walipomwita Farao mmisri.

 

 

Kustaafu kwake

Baada ya kustaafu kutoka kwa mchezo huo, Saleh Selim hakuondokia soka  mpendwa wake wa kwanza. Baada ya miaka minne ya kustaafu kwake , alichukua nafasi kama mkurugenzi wa soka mnamo 1971 na akafanikiwa kumleta Mkurugenzi wa Ufundi wa Kihungari "Hedikoti " mwenye mafanikio mazuri ya timu Al-Ahli mnamo miaka ya sabini, na hakuendelea sana madarakani baada ya kukataa kwake uingiliaji wa wengine katika majukumu ya ofisi na kisha akageukia kazi ya hiari katika bodi ya wakurugenzi, ambapo alichaguliwa kuwa mwanachama katika baraza mnamo 1972.

 

 

Miaka minne baadaye, mnamo 1976, Saleh Salim aliamua kuingia uchaguzi wa klabu katika kiti cha wakurugenzi dhidi ya Abd El mohsen Murtaji, lakini alipata asilimia 45 ya kura, na uchaguzi wa 1980 ulikuja na Nyota wa Al-Ahly aliiniga uchaguzi tena, lakini alifanikiwa kwa ubora mkubwa wakati huu kuwa mchezaji wa kwanza wa soka alichukua nafasi hii katika historia yote ya michezo ya kimisri,na alifanikiwa kushinda urais wa klabu kwa raundi tano, Amekuwa katika nafasi ya uongozi kwa vilabu vikubwa na kongwe zaidi barani Afrika na ulimwengu wa Kiarabu kwa miaka 20 wakati huo Al-Ahly imeshinda mamia ya mashindano katika michezo tofauti.

 

 

Kifo chake

Saleh Salim alikufa mnamo 6 Mei 2002 baada ya kuteseka na saratani.

Comments