Dokta Ahmed Zewail ni mtaalam wa kemia na mwanasayansi mmisri
Aliyepewa Tuzo ya Nobel
katika Kemia mnamo 1999 kwa kuunda mfumo wa kupiga picha wenye upesi mkubwa
sana kupitia kutumia laser unaoweza
kugundua harakati za masi wakati zinatokea na zinapojumuika pamoja. Na kiasi cha wakati kinachotumika kwa jambo
hilo ni Femto sekunde nacho ni sehemu moja
toka dola milioni sehemu ya sekunde moja
, kimechangiakutambua magonjwa mengi haraka, pia ana vyeti vingi vya kubuni vifaa vingi vya kisayansi.
Malezi na elimu
yake
Ahmed Hassan
Zewail alizaliwa mnamo 1946 huko Damanhour, alielekea pamoja na familia yake
kwenye mji wa Desouk mkoa wa Kafr El Sheikh, ambapo aliishi na alipata elimu
yake ya kimsingi.
Alijiunga na
Kitivo cha Sayansi, Chuo Kikuu cha Aleskandaria baada ya kupata shule ya sekondari na kupata
Shahada ya Sayansi kwa cheti cha heshima
mnamo 1967 katika utaalam wa Kemia, na alifanya kazi kama mhadhiri katika
kitivo , baadaye akapata cheti cha uzamili katika uwanja wa sayansi ya Mwangaza.
- Alifanya kazi
kama mtafiti katika Chuo Kikuu cha California (1974-1976) na kisha akahamia
Chuo Kikuu cha Caltech, nacho ni kimoja cha
vyuo vikuu vikubwa vya sayansi huko Marekani.
- alielekea
katika nafasi za masomo ndani ya Chuo Kikuu cha "Caltech" hadi kuwa
profesa wa uwanja wa Kemia, ambayo ndiyo nafasi ya juu zaidi ya kisayansi huko Marekani,
akikuja kufuatia mwanasayansi wa Marekani "Linus Pauling," aliyeipata
tuzo ya Nobel mara mbili, ya kwanza katika Kemia na ya pili katika Amani.
- Alifanya kazi kama profesa mgeni katika vyuo
vikuu zaidi ya 10 ulimwenguni pamoja na Chuo Kikuu cha Marekani huko Kairo.
- alitoa Mamia ya mihadhara ya kisayansi
ulimwenguni kote, na jina lake lilitolewa katika orodha ya heshima huko Marekani
, inayojumuisha wahusika muhimu zaidi waliochangia katika ustawi wa kimarekani,
na alipewa jina Na 18 kati ya watu 29 mashuhuri kama wanasayansi muhimu wa
laser huko Marekani (orodha hii
inajumuisha Einstein, Na Graham Bell).
Tuzo na Heshima
Dokta Ahmed
Zewail amepokea sifa , tuzo, na nishani nyingi za kimataifa kwa utafiti wake wa
upainia katika sayansi ya laser na femto, ambapo ameshinda tuzo za kimataifa
31, pamoja na:
Tuzo ya Max
Planck, nayo ni ya kwanza nchini Ujerumani.
Tuzo ya
"Walsh" ya kimarekani .
• Tuzo ya Harion How ya kimarekani .
• Tuzo ya
Kimataifa ya mfalme Faisal katika Sayansi.
Tuzo ya Hoekst ya
Ujerumani .
• Alichaguliwa
kama mshiriki wa Chuo cha Sayansi na Sanaa cha Marekani.
• amepewa medali ya Chuo cha Sayansi na Sanaa ya
Uholanzi.
Tuzo ya Ubora kwa
jina la Leonardo da Vinci.
• alipata uzamivu
wa heshima kutoka Chuo Kikuu cha Oxford,
Uingereza, Chuo Kikuu cha Marekani huko Kairo na Chuo Kikuu cha Aleskandaria.
Tuzo ya Alexander
von Humbolden kutoka Ujerumani Magharibi nayo ni tuzo kubwa zaidi ya kisayansi huko.
Tuzo ya Buck na
Tine kutoka New York.
Tuzo ya Mfalme
Faisal katika Sayansi na Fizikia mnamo 1989.
• Tuzo katika
Kemia mnamo 1993.
• Tuzo ya
Benjamin Franklin mnamo 1998 kwa kazi yake katika utafiti wa athari za kemikali
kwa wakati mdogo sana (Femto-Second) inayoitwa femtochemistry.
Tuzo ya Nobel kwa
Kemia kwa mafanikio yake katika uwanja huo huo mnamo 1999.
• Imechaguliwa na
Chuo cha Pontifical, kuwa mshiriki na kupokea nishani yake ya kidhahabu mnamo
2000
• Tuzo ya Wizara
ya Nishati ya Marekani ya kila mwaka katika
Kemia.
Tuzo ya Kars
kutoka Chuo Kikuu cha Zurich, katika kemia na Tabia, nayo ni tuzo kubwa zaidi ya kisayansi ya
Uswizi.
• Alichaguliwa
kwa hiari mwanachama wa Chuo cha Sayansi cha Marekani.
• jina lake
liliwekwa kwenye orodha ya heshima huko Marekani.
• Misri ilimheshima,
ambapo alipokea tuzo kadhaa za kimisri, pamoja na nishani kuu ya daraja ya
kwanza kutoka Rais Hosni Mubarak mnamo 1995, na Mkufu Mkuu wa Nile, nishani ya
juu kabisa ya kimisri, na jina lake likaitwa katika mitaa na viwanja kadhaa, na
Mamlaka ya Posta ilitoa stampu mbili
kwajina na sura yake, na jina lake lilitolewa kwa Sebule ya Opera.
• Mnamo Aprili
2009, Nyumba nyeupe” White House” ilitangaza uteuzi wa Dokta Ahmed Zewail yuko
kwenye Bodi ya Washauri ya Rais wa Marekani ya Sayansi na Teknolojia, inayojumuisha
wanasayansi 20 wanajulikana katika nyanja kadhaa.
Maandishi yake
Dokta Ahmed
Zewail alitunga vitabu viwili navyo ni :
- Kitabu cha
safari kupitia wakati .. njia kuelekea Noble.
- kitabu cha Enzi ya sayansi: Iliyotolewa mnamo
2005, na mnamo mwaka mmoja ilichapishwa matoleo 5, ambapo toleo lake la kwanza lilimalizika wakati wa masaa mawili ya kuchapishwa kwake.
Kifo chake
Aliaga dunia mnamo 2/8/2016 na alipendekeza azike huko
Misri.
Comments