Dokta Samira Mousa

Samira Mousa mwanasayansi wa Chembe wa kwanza mmisri na profesa wa kwanza katika chuo kikuu cha Kairo .

 Lakabu yake ilikuwa “miss kori alsharq”ikahusiana na fizikia wa kipolishi “mari kori”na profesa wake mmoja katika chuo kikuu cha Bedford katika ripoti yake ya kisayansi kwa chuo kikuu cha Kairo,alisema kuwa majaribio ya Samira Mousa yalibadilika uso wa Utu .

Ukuaji wake na Masomo yake :

Samira Mousa amezaliwa tarehe 3 mechi 1917 kijijini mwa Snebo Alkubra kituo cha Zefti mkoa wa Algharbia nchini Misri,Samira alijifunza kusoma na kuandika na tangu utoto wake ameshughulika kwa kusoma magazeti ya kila siku na Mwenyezi Mungu alimpa kumbukumbu ya picha ambayo ilimwezesh kuhifadhi kitu chochote haraka alipoiona ,jambo lililomsaidia katika mafanikio yake ya kielimu.

Samira Mousa amejiunga shule ya msingi (Senbo)na amehifadhi badhi ya qurani na ameshughulika kwa kusoma magazeti ,kisha babake amesafiri ili kufanya kazi mjini Kairo ,na Samira amejiunga na shule ya msingi ya “Qasr Al-Shawq”na kisha shule maalumu  ya wasichana ya sekondari “AL-Ashraf”.

 

Samira Mousa alichagua kitivo cha Sayansi katika chuo kikuu cha Kairo na wakati huu Dokta Mostafa Mosharfa alikuwa Mkuu wa chuo kikuu.Samira Mousa alipokea shahada ya Kwanza ya Sayansi .alikuwa wa kwanza lakini hakuteuliwa kama Profesa wa chuo kikuu ila baada ya kuungwa mkono na professa wake Dokta Mousata Mosharafa ambaye alitetea uteuzi wake dhidi ya maprofesa wageni na akaweka kujiuzulu kwake katika ofisi ya mkurugenzi wa chuo kikuu ikiwa hakuchaguliwa kama profesa katika kitivo,hata wameangalia na kujibu kwa ombi lake na aliainishwa profesa wa kwanza katika chuo kikuu cha Kairo

Samira amepokea cheti cha Uzamili  kwa daraja bora katika maudhui ambayo kichwa chake ni “Mawasiliano ya Mafuta kwa Gesi”.

kupata kwake kwa Uzamivu       

Samira Mousa amesafiri kwa London na amepata cheti cha Uzamili  katika maudhui  ya Mawasiliano ya Mafuta kwa Gesi.Kisha amesafiri pamoja na ujumbe kwa Uingereza ambapo alisoma mionzi ya nyuklia na alipata cheti cha Uzamivu katika X-ray na athari zake juu ya vifaa mbalimbali.ameweza kumaliza ujumbe wake katika miaka miwili tu na ametumia mwaka wa tatu katika tafiti mfululizo na kupitia zile alifikia  mlingano muhimu unaomwezesha kusagasaga  Maadini rahisi kama shaba ili kutengenza bomu la Chembe kwa vifaa rahisi

Amekuwa mwanamke mwarabu wa kwanza aliyepata cheti cha Uzamivu .pia,amepatia ufadhili  wa " Fullbright"  ili kusoma Chembe katika  chuo kikuu cha Calofinia,na ameweza kupatia matukio katika nyanja za tafiti za Chembe zilizoshangaza jamii za kisayansi huko Amerika na Ulaya,kwa sababu hii ameruhusiwa kutembelea maabara ya siri ya Chembe huko Amerika,alizingatiwa mmisri wa  pekee aliyeruhusiwa kufanya hivyo na alipata mapendekezo kadhaa ili kuendelea pale Amerika na kupata Utaifa wa Marekani  lakini yeye alikataa na amependa kurudia Misri ili kuendelea ujumbe wake wa kisayansi.

Aliitwa kwa  “miss kory wa Misri” na kuanzia kujenga  shirika la nishati ya Chembe mwaka1948 kama aliandaa mkutano  wa “Chembe kwa Amani”.

Samira Mousa amesafiri kwenye Marekani ili kusoma katika chuo kikuu cha “Okerdig ”mjini “Tinisi ”.

 

Dokta Samira alikuwa akikubali  mwaliko wa kusafiri kwenda Amerika 1952.ambapo alipatiwa nafasi ya kufanya tafiti katika maabara ya chuo kikuu cha Sant Lois mjini mesory nchini Amerika.alipokea mapendekezo  ili kukaa pale lakini yeye alikataa.na kabla ya kurudi kwake kwa siku kadhaa  alikubali mwaliko wa kutembelea mabaraa ya kinyuklia  katika wilaya ya California mnamo mwezi wa Agosti 15. ambapo akienda njia ya  california yenye vikwazo vingi ,ghafla gari kubwa  likaonekana kuingia kwenye gari lake na kulipeleka kwa bonde lenye kina , dereva aliruka na kutotoka  tena kamwe .Uchunguzi ulionesha kwamba  alikuwa na jina la utani,na usimamizi wa Mtambo haukupeleka mtu yoyote.

 

Michango yake ya kisayansi:

Altumaini kwamba Chembe  kutumika vizuri  kwa ajili ya mwandamu na kuingia katika uwanja wa matibabu ambapo  anasema “matumani yangu ni kutibu Saratani kwa Chembe ,kama aspirini”.

Tafiti zilizofikiwa na  Dokta Samira  hazinukuu,  ingawa alikuwa na matumaini ya Misri na ulimwengu wa kiarabu kupata nafasi kati ya maendeleo makubwa haya ya kisayansi,wakati ambapo yeye aliamini kuwa kuongeza kwa umiliki wa silahi za nyuklia huchangia kuhakikisha Amani.Hizi zilirudiwa kwa wito wa umuhimu wa silaha za nyuklia,nakuendelea katika uwanja wa kisayansi mwenye maendeleo haya.

Samira Mousa Alianzisha shirika la nashati ya Chembe ,na alipanga mkutano wa Chembe  kwa ajili ya Amani ambao ulikaribishwa kwa kitivo cha sayansi na idadi kubwa ya wanasayansi wa Ulimwengu .

 

Samira Mousa alikuwa mwanachama wa kamati  maalumu nyingi za kisayansi zinazoongozwa na “kamati ya nishati na ulinzi wa bomu la Chembe ”,iliyoundwa kwa wizara ya Afya ya kimisri .

Misri haisahau binti yake mkubwa,ambapo ilimheshimu wakati Rais Mouhamed Anwar El-Sadat alimpa Nishani ya sayansi na sanaa ya kwanza mwaka 1981,na alipewa jina lake juu ya shule moja ya  wizara ya elimu kijijini mwake .pia,kuanzisha jumba la utamaduni kwa jina lake katika kijiji chake mwaka1998.


Comments