Uamuzi wa kuanzisha Baraza Kuu kwa Sanaa na Ustawi wa Fasihi uliidhinishwa kwa mujibu wa Sheria Namba 4 kwa mwaka 1956
Liwe taasisi huru linaloambatanishwa kwa Baraza la Mawaziri , lenye jukumu la kuratibu na kuunganisha juhudi za mashirika ya serikali yanayofanya kazi katika nyanja za sanaa na fasihi.
Miaka miwili baadaye, Baraza lilikuwa na uwezo wa
kudhamini sayansi za kijamii.Kwa karibu robo ya karne, Baraza Kuu la Sanaa, fasihi
na Sayansi za Kijamaa liliendelea kuchukua jukumu lake katika maisha ya
kitamaduni na kitafakari nchini Misri.
Mnamo 1980 ilibadilishwa kwa "Baraza Kuu la Utamaduni
"kwa kutolewa na sheria namba 150
kwa mwaka 1980.Baraza Kuu la Utamaduni liliongozwa na Waziri wa Utamaduni. Na
katibu mkuu kwa Baraza kuu la Utamaduni ana jukumu kuendesha sera yake na anasimamia utekelezaji
wake, na jambo lile halikuwa kubadilisha jina tu bali ilibadilika katika jukumu
na malengo. Basi kwamba Baraza Kuu la
Utamaduni limekuwa akili inayopanga kwa ajili ya sera ya kitamaduni nchini
Misri kupitia kamati zake zifikazo
kamati ishirini na nane, ambazo ni pamoja na kikundi cha wasomi na wabunifu kutoka vizazi na mienendo
tofauti.
Mnamo miaka ya hivi karibuni, Baraza Kuu la Utamaduni
limeshuhudia kuongezeka kwa shughuli zake. Ambapo limekuwa kituo cha kitamaduni
na mawazo kwa kiwango cha kimisri na kiarabu na ngome ya kuijua kupitia mikutano na semina zilizopangwa na
kuhudhuriwa na kikundi cha wasomi na watafakari waarabu, ambayo ikawa inafaa
kwa mwingiliano wa kitamaduni kwa kiwango cha Kiarabu pamoja na Ushiriki wa
watafiti wengine mashuhuri katika taasisi za kimasomo ulimwenguni mashariki na magharibi katika shughuli za
Baraza.
Jengo la kisasa la Baraza Kuu la Utamaduni liko katika ukumbi
wa Opera., Jengo hilo linaangalia mto wa
Nile kutoka upande wa magharibi wa barabara ya Um Kulthoum. Na kutoka upande wa
mashariki huangalia Ukumbi wa nyumba ya
kimisri ya Opera .
Jengo hilo lina maktaba kuu inayoweza kuchukua watu 50 na kazi kuu ya
maktaba katika jengo jipya la Baraza kuwa maktaba kwa vitabu vya zamani ambapo
inajumuisha kikundi cha masomo, kamusi na vitabu vya zamani muhimu katika
nyanja zote za elimu ,pamoja na kikundi cha vitabu vya zamani, na ambazo hakuna
maktaba moja nchini Misri inayozijumuisha.
Maktaba pia ina machapisho ya Baraza , Kituo cha kitaifa kwa
Ufasiri , mfululizo wa kitabu cha
kwanza, semina na mikutano inayofanyikwa kwa Baraza.
Jukumu la Baraza Kuu kwa Utamaduni:
Baraza Kuu la Utamaduni linachangia mafanikio mengi katika
ngazi ya kitamaduni na kimawazo, kitaifa , kikanda na kimataifa. Na miongoni mwa Mafanikio haya ni:
Baraza limepanga mikutano na semina nyingi za kitaifa,
kikanda na kimataifa, ambapo limejadili masuala mengi ya mawazo, utamaduni,
sanaa na fasihi . , kama vile ilivyokuwa eneo la mawasiliano ya kiakili kati ya
wafikiri na wabuni wamisri, waarabu na wazungu katika miaka iliyopita.na
miongoni mwa mikutano hii ya kimataifa ni mkutano wa Amaz Donkol , mkutano wa
riwaya ya kimisri- kimorocco . Mkutano wa mwanamke mwarabu na Ubunifu, Mkutano wa Masuala ya Ufasiri na
Mingiliano ya kitamaduni , pia Baraza lilisherehekea kumbukumbu ya alama za
kitamaduni, mawazo, waumbaji na wafikiri kupitia semina tofauti, Na maadhimisho
ya Baraza yaliongezeka hadi alama kadhaa za mawazo ya kimataifa na sanaa na
maandiko, ya zamani na ya kisasa, kama vile:Federico Garcia Lorca - Sophoances
- Bertold Brecht - Alexander Pushkin - Ibn Rushd - Refaah Al Tahtawi - Abdul
Rahman Al Rafie - Jamal Al Deen Al Afghani - Mohammed Abdo - Zaki Naguib Mahmoud
- Salah Abdel Sabour - Berm Eltunsi -
Umm lilting -Naguib Rihani - Abi Hayyan Tawhidi - Taha Hussein - Tawfiq
al-Hakim - Mahmoud Said, pia Baraza limetoa kundi la nakala kadhaa, ambazo
zimetayarishwa na kamati tofauti za Baraza kama jarida la njia za muziki, jarida la falsafa, jarida la kitabu na kuchapisha, jarida la Ufasiri.
Katika kiwango cha Tuzo za nchi : Serikali iliunga mkono
jukumu la Baraza katika kukuza ubunifu na kuthaminiwa kwa wasomi na watalam kwa
kurudisha idadi ya tuzo za nchi kwa kutathmini uhamasishaji, ambazo hupewa kwa
Baraza Kuu la Utamaduni katika matawi ya sanaa, fasihi na sayansi za kijamii kulingana
na kuteuliwa kwa taasisi kadhaa za
kisayansi na kiutamaduni. Na gharama za tuzo zile ziliongezeka kufikia paundi
laki mbili kwa tuzo za kutathmini .
Tangu mwaka wa 2003,
Baraza limeanza kutoa barua mpya inayoitwa "Machapisho ya hivi
karibuni" ambayo ina orodha ya machapisho ya hivi karibuni ya Baraza
iliyotolewa wakati wa robo mwaka , nayo ni habari mfululizo ya kila miezi
mitatu.
Shughuli za Baraza zimepokea msaada na uungaji mkono wa nchi
. na Baraza lilishuhudia maendeleo wazi katika shughuli zake mnamo miaka ya hivi karibuni. , na limekuwa
kituo cha utoaji wa kiutamaduni na kielimu katika ngazi za kitaifa, kikanda na
kimataifa, ambapo maisha ya Baraza yalikaa zaidi ya miaka arobaini na tano, na lilikusanya
wataalam wa sanaa, fasihi na sayansi za
kijamii, na likaanza shughuli zake ambazo ziliamriwa katika sheria ya
kuanzishwa kwa mipaka mipana zaidi iwezekanavyo, na kupitishwa kutoka miradi
isipokuwa ikiwezekana kuingia kwenye shughuli za taasisi ya kiserikali au
shirika la umma.
Malengo ya Baraza Kuu kwa Utamaduni:
Ni kurahisisha njia za kiutamaduni kwa watu na kuziunganisha
na maadili ya kiroho, kwa kukuza demokrasia ya utamaduni na kuifikia katika
sekta pana zaidi ya watu , pamoja na likikuza
vipaji katika nyanja tofauti za utamaduni, sanaa na fasihi, kufufua urithi wa
zamani na kuwajulisha raia kwa tija za maarifa ya kibinadamu, na kuthibitisha
maadili ya jamii ya kidini, kiroho na
maadili.
Inatafutia kuratibu juhudi za kiserikali na za kijamii
katika nyanja za sanaa na fasihi. Kwa hivyo Baraza hilo lilikuwa la kwanza kwa
aina yake kwa uwanja wa Kiarabu, lililosababisha kuhamasisha nchi nyingi za Kiarabu
kuifuata Misri na kuunda Mabaraza kama yale.
Comments