Rais wa kamati kuu ya matibabu aeleza maandalizi ya kiafya kwa kukaribisha Misri, 2021

Daktari Hazem Khamis –Rais wa kamati kuu ya matibabu kwa Shirikisho la kimataifa kwa mpira wa mikono- ameeleza maandalizi magumu kwa toleo la 27 la mashindano ya dunia ya mpira ya mikono kwa wanaume- Misri, 2021.

 Hayo ni mashindano ya kwanza ya kimataifa ya Pamoja kwa wanaume yanayofanyika baada ya mlipuko wa virusi vya Corona.


Khamis alizungumza na tovuti rasmi ya Misri, 2021, akisema: “ kukaribisha mashindano sio chanagamoto za kawaida; kwani nchi nyingi labda hazitakubali kupanga mashindano makubwa kama hayo katika wakati huu, na katika hali isiyoshuhudiwa hapo awali Duniani."


Akakamilisha:" Misri ikiwakilishwa na Rais wa kamati kuu iandaayo  mashindano –Mheshimiwa Waziri Mkuu ,Dokta Moustafa Madbuly , wajumbe wa kamati kuu inayojumuisha aghlabu ya mawaziri wa Misri, inajua jinsi ya kupanga mashindano hayo yatakayoshuhudia ushiriki wa timu 32 kwa mara ya kwanza.”


Akaongeza: “ ajali zimeamua kuwa kamati ya matibabu katika Shirikisho la kimataifa kwa mpira wa mikono inayohusiana na mashindano haya itabeba taratibu hizi. Tunapaswa kuthibitisha kwa ulimwengu, na kuutuliza kuwa maandalizi ya kimatibabu -nchini Misri- ni kwenye kiwango cha juu kulingana na viwango vya shirika la afya duniani (WHO).”


Akaoneysha: “tangu tulipounda kamati, tumefikiria jinsi ya kulinda kila mtu ana uhusiano na mashindano kutoka hatari za kuambukizwa, kwa hivyo tulijumuisha viongozi wa Wizara ya Afya ya kimisri, na wanaosimamisha maandalizi , pamoja na wasimamizi wa hospitali ya Wadi Al Nil –mtoaji wa kiafya kwa mashindano-, na kadhalika kamati ya matibabu katika Wizara ya vijana na michezo ya Misri; kwani jambo muhimu Zaidi ni kuhifadhi ujumbe wote huo kutoka Corona.”


Akaonesha: “tangu mwanzo wa mkutano wetu na Daktari Hala Zaid –Waziri wa Afya-, Dokta Ashraf Sobhy –Waziri wa vijana na michezo-, na kamati iandaayo, tumeweka sentensi tatu kuu, Hakuna maonyesho, Hakuna uzembe, Hakuna upendeleo.”


Maandalizi ya kimatibabu yanayotarajiwa kutekelezwa.


Akaeleza: “maandalizi yatakayofanyiwa sio kutoka uvumbuzi wetu, bali yanakuwa maandalizi ya kimataifa. Kila mtu ataingia Misri kwa kushirikana na mashindano, atafanya uchambuzi wa PCR matokeo yake ni hasi kabla ya kufikia Misri kwa masaa 48, na tangu kupanda ndege kwa kufikia uwanja wa ndege wa Kairo, atafanya maandalizi ya kimatibabu katika ndega au uwanja wa ndege, au katika basi za timu zinazowabeba kwenye hoteli. Maandalizi yataanza kutoka dakika ya kwanza hadi dakika ya mwisho wakati timu zinapopatikana nchini Misri.”


Akaendelea: “lengo letu kutumia nadharia ya bubuni. Kila mtu atashughulisha na wachezaji, watawala, makocha, wasaidizi au wafanayakazi wa matibabu, watasimama katika mahali pao, kufanya uchambuzi PCR kila masaa 72, ni hilo ni jambo linalotumika kwa kila mtu atakayeshiriki katika mashindano. Maeneo fulani yamehususishwa katika hoteli kwa timu, na kadhalika maeneo fulani kwa kutengwa ikiwa kuna maambukizi.

 Moja kwa moja timu ya matibabu itashughulikiwa, ili kudhamini kuhifadhia maandalizi haya.”


Akasisitiza: “kwenye Kumbi, wote watavaa vifuniko vya kujikinga "Barakoa" isipokuwa wachezaji ndani ya uwanja wa michezo wakati wa mashindano na matayarisho.”


Akasisitiza: “ wote lazima wajue kuwa  hakuna ukosefu wowote wa mfumo wa  kimatibabu ; kwani macho ya ulimwengu yanakusudia mashindano na Misri, na jambo hilo litakuwa wazi kwa hadharani kuanzia  sherehe ya kura, Septemba 5.”


Matayarisho ya sherehe ya kura.


Kuhusu sherehe ya kura, huko eneo la piramidi za Giza, Khamis amesema: “ujumbe unaokuja kutoka nje, utakaa katika hoteli karibu na eneo la tukio. Pale tutafanya mkutano wa habari kwa kuonesha kazi za kamati ya matibabu, ili wote wanatulia kuhusu maandalizi.”


Akaonesha: “ watu 200 tu watahudhuria sherehe ya kura. Tumewagawanya kwa vikundi tofauti kati ya watu muhimu, waalikwa, na wanahabari, kila kikundi kina mwingilio fulani  ili kutekleza dhana ya kutenga  watu.”


Akasisitiza: “tumeweka maandalizi magumu kuhusu kuingia na kutoka, hasa wakati wa kutoka; kwani watu huwa kusahau maandalizi baada ya mwisho wa tukio, pia tutahakikisha kuwa wote watahudhuria tukio, wakivaa vifuniko vya kujikinga"Barakoa" isipokuwa mtu azungumzaye kwenye jukwaa, wakati wa atakuwa pale tu.”


Matayarisho ya kukaribisha watazamaji.


Khamis ameelekea kueleza maandalizi ya kukaribisha watazamaji katika kumbi nne zinazokaribisha mashindano, akasema: “uratibu umefanywa na kamati ya matibabu katika Wizara ya vijana na michezo, Shirikisho la kimisri la mpira wa mikono, kamati yake ya matibabu , na viongozi wote wa wizara ya afya wanaokuwa katika kamati. Kila wiki mbili, tunakutana kupitia mkutano wa video pamoja na Shirikisho la mataifa la mpira wa mikono, wajumbe wa shirika la afya duniani, na pia wajumbe wa Shirikisho la Ulaya la mpira wa mikono, pamoja na wasimamizi wenye ufanisi na maarufu Zaidi wa maandalizi ya kimatibabu katika uwanja za mpira za kiulaya.”



Akasisitiza: “ idadi za watazamaji hazitazidi kutoka 25% hadi 30% kutoka eneo la kila ukumbi, pamoja na umbali kwa mita 2 baina ya kila shabiki na mwingine. Tutapitia nafasi hizi kwa kadri ya hali itakayokuwa bora. Wote watavaa vifuniko vya kujikinga, na kutopatikana vyakula au vinywaji. Maandalizi ya kutotangamana yatafanywa wakati wa kuingia na kutoka kwa ukumbi, kulingana na maelekezo ya kimataifa.”


Akaeleza: “sisi tuna mkataba pamoja na hospitali mbili karibu na kila ukumbi, kwa umbali wa dakika 28 wa kuandesha gari la ambulansi kwa kufikia ukumbi. Tuna vifaa vyote ndani  ya kumbi, magari ya ambulansi 12 yana vifaa, na vifaa vyote vya kisasa, ikiwa ni pamoja na vifaa vya mshtuko wa umeme, pia tumeandaa wahusika wa matibabu ili wawe ndani ya viwanja.


Khamis ameshatimiza: “bila shaka, watu wa Misri wanasaidia mashindano, na jinsi ya kwanza ya kusaidia ni kufuata maandalizi ya kukinga yanayotolewa na Wizara ya Afya  mara kwa mara, pia kamati ya matibabu inayohusiana na mashindano. Misri kwa uongozi wake wa kisiasa, na raia wake inastahili kuwa katika hali bora zaidi.”

Comments