Waziri wa michezo yuko kwenye mkutano wa vyombo vya habari kwa kutangaza maelezo ya kura ya kombe la dunia la mikono 2021

Shukrani na heshima kwa Rais Abd El-Fatah El-Sisi kwa kutolewa msaada wote na mwongozo ili kutokeza tukio zuri linalofaa nafasi ya kimtaifa ya Misri .

Kusisitiza  uangalifu wa Waziri Mkuu anayeongoza kamati ya juu kwa michuano na Uanachama wa mawaziri 18 .

Hatua kali za tahadhari kuanzia mapokezi ya wageni ,sherehe za kura na matukio ya michuano mpaka kuondoka .

Eneo la Piramidi lakaribisha sherehe za kura ya kombe la dunia la mpira wa mikono mnamo Septemba 5 ijayo , Januari 13 mpaka 31 kwa uzinduzi wa michuano. 

  Matumaini mema yote kwa mahudhurio mema kwa vipengele vyote vya mchezo ,wahusika na timu  duniani kote .

Waziri huyo, Dokta Ashraf Sobhy ,siku ya Jumanne , Septemba mosi, 2020 alifanya mkutano wa uandishi wa habari kwa kutangaza maelezo ya sherehe ya kura kwa michuano ya dunia kwa mpira wa mikono,inayopangwa kuifanyika nchini Misri Januari 2021 katika toleo lake la 27 ,kwa mahudhurio ya Mhandisi Hesham Nasr Mwenyekiti wa kamati iandaayo ,Kocha Hussien Labib Mkurgunzi wa michuano ,Tarek Eldeep Naibu wa Mkurgunzi wa michuano ,Dokta Ahmed Elshiekh Mwenyekiti wa kamati ya mawasiliano ya serkali ,wakuu wote wa kamati za kiufundi zinazoandaa michuano ,na wahusika wa kampuni mbili za Tiketi yangu na Presentation .


Dokta Ashraf Sobhy alitoa shukurani na heshima kwa Rais Abd El-Fatah El-Sisi kwa kutolewa msaada na mwongozo ili kutokeza kombe la mikono kwa sura nzuri inayofaa nafasi ya kimtaifa na kihistoria ya Misri ,pia alitoa shukurani kwa nchi ya Waziri Mkuu  anayeongoza kamati ya juu iandaayo  michuano na Uanachama wa mawaziri 18 juu ya uangalifu wake mkubwa kwa maelezo yote ya tukio .


Waziri huyo alionesha ,vitu vipya vya mwisho vinavyohusiana  na kumalizika kwa majengo yote yanayohusiana na kumbi zinazokaribisha michuano ambapo kiwango cha kumalizika kwake kimepita 88% kwa thamani ya  paundi za kimisri za bilioni 3,2 na jambo hili linasisitiza kiwango cha miradi ya kimchezo inayotekelezwa katika enzi ya Rais  El-Sisi na vitu vyake vya mwisho ni majengo yaliyoboreshwa katika mashindano ya mataifa ya Afrika 2019 yaliyovutia ulimwengu wote kwa maandalizi yake .

Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza dhraura ya kutekeleza hatua na taratibu za kinga na tahadhari na kufuata daima na kamati ya kimtaibabu na kamati iandaayo kuanzia mapokezi ya ujumbe wa timu ,ujumbe unaooandamana na wageni kupitia sherehe ya kura kwa kombe la dunia la mikono mnamo Septemba 5 huko eneo la Piramidi ,kuhifadhi Usalama na Afya wakati wa hali za kisasa zilizosababishwa na Janga la Corona.


Waziri huyo alionesha kundi la hatua za kulinda ambalo imeamuliwa kuzifuatilia katika michuano na la muhimu zaidi ni kupima  joto ,kuvaa maski ,kuepuka msongamano ,kuepuka watu ,kutumia vitu vya kusafisha mikono pamoja na hatua za kutenda na visa vinavyoweza kugundulika wakati wa kombe la dunia kupitia ushirkiano na Wizara ya Afya iliyoonesha Ushirikiano wote kamili na msaada wote ili kutolewa nafasi za kimatibabu kwa kila mtu anaingia Misri na kuchukua hatua zote pamoja na hospitali kuanza Uwanja wa ndege ,kupanda mabasi ,safari na mazoezi katika kumbi pia mikutano ya vyombo vya habari ,akiashiria jambo hili linasisitiza nchi inakamilika njia ya mafanikio na kutoa sura nzuri kwa Dunia ,Waziri aliita dharura ya ushirikiano wa wote wa jamii kwa ajili ya kuhakikisha mafanikio mazuri kwa michuano na kuandaa kwake kwa kiwango bora zaidi .


Kuhusu orodha za mahudhurio ya mashabiki kwa michuano Sobhy alisema :" Wakati wa kisasa tumejadili jambo hili , pengine mashabiki watapatikana kwa 100 % ,au kiasi cha 2 kwa 1 inamaanisha kuna kiti bure kati ya  viti viwili vinavyojaa."


Sobhy alisema :" Michuano ya kombe la dunia kwa mikono 2021 ni michuano ya kwanza inayoandaliwa kwa ushiriki wa timu 32 ,isipokuwa toleo lililopita limefanyika katika nchi mbili na linalokuja litaandaa katika nchi tatu ,jambo linalotuweka katika changamoto mpya ,tunaweza chini ya uongozi wa Rais Abd El-Fatah El-Sisi kushindana  na kuhakisha miujiza jinsi ilivyotokea katika michuano ya mataifa ya kiafrika 2019."


Waziri huyo aliongeza :"Siri ya kuhakikisha mafanikio ya michuano imo ndani ya  ushirikiano wa wote kutoka taasisi za nchi na Mashabiki wa Misri na Shirikisho la kimataifa na kimisri kwa mikono."


Kwa upande wake ,Mhandisi Hesham Nasr Mwenyekiti wa shirikisho la mikono ,alisifu jukumu kubwa kwa Waziri wa michezo kwa hatua zote za kila wakati ili kumaliza kazi zote kwa mujibu wa jedwali za wakati zinazotangaza hapo awali  zilizokabiliwa pamoja na Shirikisho la kimataifa kwa mikono chini ya uongozi wa Dokta Hassan Mustafa  aliyeashiria  juhudi kubwa zinazotolewa na Misri  katika kuandaa kwa michuano kupitia kumbi ambazo shughuli zake zote za majengo zitamalizikwa hivi karibuni , zinazozingatiwa mahali pakubwa kwa michezo yote sio mikono tu .


Kwa upande wake Huseen Labib Mkurgunzi wa michuano alisisitiza imeshamalizika kutoka ishara inayohusiana na michuano na imeshatengenzwa katika  nchi moja  ya Ulaya ,itagunduliwa  katika sherehe ya kura Jumamosi ijayo .

Michuano hufanyika mnamo kipindi cha 13_31 Januari 2021 ,litakuwa toleo la kwanza linalojumuisha timu 32 badala ya 24 , mashindano yake yanafanyikwa kwenye kumbi 4 nazo ni : ukumbi wa Uwanja wa Kairo ,Ukumbi wa mji mpya wa kiutawala ,Ukumbi wa 6 Oktoba na Ukumbi wa Borg Alarab .

Comments