Hassan Mostafa asisitiza kuwepo kwa mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa kwa Kombe la Dunia la mpira wa mikono 2021 huko Misri

Dokta Hassan Mostafa, mwenyekiti wa Shirikisho la kimataifa la mpira wa mikono, alitangaza kuhudhuria kwa Thomas Bach, Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa, kwa Kombe la Dunia Misri 2021.

Hassan Mostafa, mwenyekiti huyo, alimpa Dokta Mustafa Madbouly Waziri Mkuu "kalamu ya kidhahabu" pembezoni mwa ufunguzi wa kura ya Kombe la Dunia la mpira wa mikono 2021 , huko eneo la  Piramidi, akisifu juhudi zake na juhudi za serikali kuandaa sherehe hii na kukaribisha Misri kwa mashindano .


Hassan Mostafa alitoa hotuba yake kwa Kiingereza wakati wa sherehe hiyo, akisema: "Ninafurahi kuwa na nyinyi leo, na kusherehekea kura ya Kombe la Dunia la mpira wa mikono. Natamani ifanikiwe. Natamani mashindano haya yawe taa mwishoni mwa kipindi cha giza. Ningependa kumshukuru Mustafa Madbouly kwa uongozi wake wa kamati na uandaaji wenye kuvutia. Napenda pia kumshukuru Ashraf Sobhy, Waziri wa Michezo. "


Aliendelea: "Janga la Corona bado halijaisha, na hakuna hata mmoja  anayejua ni lini janga hili litaisha, kwa hivyo lazima tuishi na maisha haya mapya, na serikali ya Misri na Shirikisho la Mpira wa Mikono la Kimataifa lilishinda, na lazima nimshukuru Khaled Abd El Aziz,  aliyekuwa Waziri wa Michezo, na nina uhakika kuwa Misri itakuwa nuru itakayoangaza kwa ulimwengu kwa kuzingatia janga hili. "


Aliongeza: "Afya na Usalama ni jambo muhimu zaidi, kwa hivyo tumetoa timu za matibabu kuweka hatua zote muhimu za kiafya, na tutajaribu na kufanya harakati iwezekanavyo kuhakikisha Usalama wa washiriki wote kwenye mashindano, na hafla hii itakuwa kubwa zaidi kwa idadi mnamo wakati wa janga la Corona , na ikiwa tutazungumzia kura ile ile, lazima tutaje." Inahusu bahati nzuri na bahati mbaya. "

 

Na mwanamuziki Omar Khairat aliwafurahisha mahudhurio ya mashindano ya Kombe la Dunia la mpira wa mikono yaliyofanyika huko eneo la Piramidi kwa muziki nzuri sana.

Comments