Waziri wa usafiri wa Anga ampokea Waziri wa Vijana na Mwenyekiti wa shirikisho la kimataifa la mpira wa mikono
- 2020-08-25 12:08:16
kujadili maandalizi ya Kombe la Dunia la mpira wa mikono
Mwanahewa Mohamed Manar Waziri wa Usafiri wa Anga wa kiraia, alipokea Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo na Dokta Hassan Mustafa, mwenyekiti wa Shirikisho la kimataifa la mpira wa mikono ofisini mwake katika makao makuu ya Wizara ya Usafiri wa Anga wa kiraia kujadili maandalizi maalum ya kukaribisha Jamuhuri ya kiarabu ya Misri kwa michuano ya kombe la dunia la Mpira wa mikono 2021, kwa mahudhurio ya mwanahewa Amr Abu Al-Ain, mwenyekiti mkuu wa uongozi la shirika la Kimisri kwa usafiri wa Anga na msaidizi wake mwanahewa Hassan Munir.
Mkutano huo ulijumuisha kujadili njia za uratibu za pamoja kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na Wizara ya Usafiri wa Anga ya Kiraia ili kuandaa michuano vizuri kwa kushirikiana na Shirikisho la kimataifa la mpira wa mikono na wizara zote zinazohusika kwa ajili ya mafanikio ya mashindano hayo na kutoka kwake kwa sura ya heshima inayofaa nafasi ya Misri ulimwenguni, ambapo maelezo yote yanayohusiana na timu, wajumbe wa michezo na wajumbe wanaoshiriki katika michuano yalijadiliwa, yakiwapa ruhusa maalum, tarehe za kuwasili na kusafiri, na pia ushiriki wa Kampuni ya kitaifa ya Misri kwa usafiri wa anga (Egypt Air) kama mchukuaji rasmi wa michuano hiyo .
Kwa upande wake, Waziri wa Usafiri wa Anga alisisitiza kwamba Wizara ya usafiri wa Anga ya kiraia na mashirika yake yote na kampuni zake zote zinazohusika zinashiriki katika kuandaa mashindano ya michezo yanayokaribishwa na Misri na kufanya juu chini ili kutoa njia zote za msaada kwa wageni wa Misri, akisisitiza juu ya utayari wa viwanja vya ndege vya Misri kupokea timu zote na wajumbe wa michezo na kuchukua Hatua zote za tahadhari ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona kwa kushirikiana na mamlaka zinazohusika na usimamizi wa karantini.Manar ameongeza kuwa ruhusa zote maalum zitatolewa kwa wageni wa Misri na uundaji wa vikundi vya wafanyikazi kwa kiwango cha juu cha ustadi na kiufundi kufanya kazi kumaliza haraka taratibu za ufikiaji na kusafiri kwa njia rahisi na usalama zaidi.
Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza kwamba kuna ushirikiano na mashirika mbalimbali na wizara mbalimbali kuandaa michuano kwa njia inayofaa pamoja na kuchukua hatua zote za tahadhari na kinga muhimu ili kudumisha afya na amani ya timu zote na mashabiki .
Na Sobhy alisifu dhamira ya Wizara ya Usafiri wa Anga kusaidia mashindano ya michezo na kutoa msaada na utunzaji wao, akiashiria kuwa uundaji wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa michuano hiyo unathibitisha uwezo wake wa kuandaa michuano mikubwa ya michezo kwa sababu ya viongozi wa Misri wenye uzoefu wa hali ya juu katika matukio muhimu kama hayo .
Akisifu jukumu kubwa la kitaifa lililochukuliwa na Dokta, Hassan Mustafa, mwenyekiti wa shirikisho la kimataifa la mpira wa mikono, na kujali kwake kufuata na uratibu na wizara, jambo linaloongeza umuhimu wa mfumo wa mpira wa mikono wa Kimisri na huweka daima kwenye majukwaa ya kimataifa ya kushinda.
Comments