Waziri wa Michezo akutana na Kamati iandaayo kwa Kombe la dunia la Mpira wa Mikono 2021
- 2020-08-25 12:10:50
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, amekutana asubuhi ya leo na Kamati iandaayo kwa Mashindano ya kombe la dunia kwa Mpira wa Mikono, na yaliyopangwa kukaribishwa na Misri mnamo mwanzoni mwa mwaka ujao 2021,
kwa mahudhurio ya Rais wa Shirikisho la kimisri kwa Mpira wa Mikono Hisham Nasr, na Hussen Labib, Mkurugenzi wa Kamati iandaayo kwa mashindano, na viongozi kadhaa wa Wizara ya Vijana na Michezo.
Mkutano huo pia ulijadili taratibu za wajitolea wa mashindano kutoka vijana wamisri, zitakazotangazwa mnamo siku zijazo. Mkutano huo pia ulizungumzia maandalizi ya michezo ya kumbi zilizofunikwa, ambazo zitakuwa kwa viwango vya juu zaidi vya kimataifa katika suala hili.
Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza wakati wa mkutano huo kwamba nchi ya Misri, chini ya uongozi wa Rais Abd El Fatah El-Sisi rais wa Jamhuri, iliiweka Misri katika nafasi ya kutofautisha kati ya nchi za ulimwengu kwa sababu ya miundombinu ya kimichezo ya kipekee iliyofanya Misri kuwa kituo cha matukio na mashindano ya dunia , akionyesha kwamba miundombinu hiyo itaongezewa katika siku za usoni Kundi linalojulikana la vituo na kumbi za kimichezo zilizohusiana na kukaribishwa kwa Kombe la Dunia la mikono 2021.
Kuhusu wanaojitolea, Sobhy alisisitiza kwamba Misri imekuwa na vijana wanaoweza kuchukua jukumu na kufanya kazi za kujitolea katika mashindano ya kimichezo kwa ustadi na kiwango cha juu, kilichoonyeshwa katika mashindano mengi ya Kidunia , ya kibara na ya kimataifa yaliyoandaliwa na Misri mnamo kipindi kilichopita.
Imetajwa kuwa Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, hufanya mkutano wa kila wiki pamoja na kamati iandaayo kwa mashindano hayo kuangalia taratibu zote na maandalizi ya mashindano hayo na kurahisisha vikwazo vyote.
Comments