Waziri wa Michezo ayaangalia mafanikio ya kuanzisha ukumbi wa Borg El - Arab kuandaa kombe la dunia la Mpira wa Mikono

Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa Vijana na Michezo alitembelea mradi wa kuanzisha ukumbi wa kufunika , Borg El - Arab , Mkoa wa Aleskandaria ,

unaojengwa kwenye ukubwa wa ekari 12.5 , unaanzishwa kulingana na vigezo vya kimataifa ambapo unapaswa kupokea mashindano ya kombe la dunia la mpira wa mikono kwa wanaume yanayofanyika Misri Januari ijayo . 


Ameangalia vipimo vya utendaji vya kumalizia misingi ya ujenzi wa ukumbi huko Borg El Arab unaofikia asilimia 95 ya kumalizia kazi zinazotakiwa , akatembelea ukumbi mkuu wa kufunika na viwanja vya akiba, vyumba vya wachezaji na vyombo vya kifani na kiidara ,  mahali pa kamati iandaayo , kituo cha vyombo vya habari , klabu ya kimatibabu na ukumbi wa mikutano . 


Dokta Ashraf Sobhy akasifu kiwango cha ajabu cha ukumbi huko Borg El- Arab na kumalizia kazi za ujenzi kulingana na miadi zinazotarajiwa uunganishwe na kumbi nyingine zinazopaswa kupokea Ligi La Kombe La Dunia La Mpira wa Mikono , zinazowakilisha katika ukumbi wa kufunika kwenye "stadi ya Kairo , ukumbi Mji wa 6 Oktoba , ukumbi wa mji mkuu wa uongozi mpya "


Waziri wa Vijana na Michezo aliashiria umuhimu wa uongozi wa kisiasa wa kimisri wa kuendeleza mchezo na kuifanya Misri mbeleni mwa nchi zinazopokea ubingwa wa Michezo wa kimataifa kutokana na uhodari wa nchi wa miundombinu kwa pande za majengo ya Michezo , hoteli , viwanja vya ndege vya kimataifa , kutoa huduma nzuri za mawasiliano , pamoja na usambazaji wa usalama na amani nchini kote , akiashiria kuwa vitu hivyo vyote ni sababu kuu za  mafanikio ya Misri  kuhusu  kupokea ubingwa mkubwa na kubainishwa kwa sura nzuri mbele ya nchi za dunia . 


Waziri akielezea kujali kwa mipango na kamati iandaayo Mondiali ya Mpira wa Mikono , na kukutana na wanachama wa kamati kila wiki ili kujua mapya ya maandalizi ya kilojistiki na kiidara kwa ubingwa , na kujua vyote vya hali ya ujenzi ya kumbi za kufunika zinazopokea Mondiali , akibainisha ufuatiliaji wa Shirikisho la Mpira wa Mikono la Dunia kwa suala hilo kusisitiza utayari wa Misri ili kupokea ubingwa .

Comments