Mahmoud El_Aadl aelezea maandalizi ya kamati ya matabibu kwa ajili ya kupokea mashindano ya dunia ya mpira wa mikono

Dokta Mahmoud El_Aadl , mwanachama wa bara la uongozi wa shirikisho la kimisri la mpira wa mikono pia ni mwenyekiti wa kamati ya matibabu kwenye mashindano ya kombe la dunia 2021

, ameelezea mpango wa kamati ya matibabu kupitia kombe la dunia la mpira wa mikono linalofanyika Misri Januari ijayo.



El_Aadl amesema kuwa kuna mpango uliopangwa na kamati ya matibabu , katika mazingira  ambayo ulimwengu unaiishi kwa kueneza kwa Covid19 . Na haki za timu za kitaifa zinazoshirki katika mashindano kuwa na amani juu ya jumbe zake zikiwa za wachezaji au vyombo vya kiufundi au wanahabari , na tunatakiwa tuwe mfano mzuri wa kupanga mashindano ya dunia . 


El_Aadl alisisitiza kuwa kamati ya matibabu inataka kuchukua hatua za kiafya na kutoa huduma tofauti za matibabu ,  hususan  ni mhusika wa kugundua virusi vya Corona , na itakuwa chini ya usimamizi wa kamati maalum kutoka kwa shirikisho la mpira wa mikono la kimataifa , kwa hiyo kamati ikaamua kuwepo kwa kituo cha matibabu katika kila sekta uwanjani unaopokea mashindano , kwa ajili ya mashabiki , isipokuwa shirikisho la mpira wa mikono la kimataifa lilikubali kuwepo kwa mashabiki  kwenye mashindano . 


Kamati ilikubali kuanzisha vyumba vya matibabu kwa wachezaji na vingine kwa wanahabari , na vyumba cha wageni muhimu , ndani ya kila ukumbi kutoka kumbi nne husika  , mpango wa kamati hausimamishwi hapa lakini ilikubali kuwepo kwa magari 8 kwa huduma za afya kwa wachezaji , jumbe , wanahabari na mashabiki , pamoja na kuwepo kwa magari ya huduma za afya yanayoambatana mabasi ya timu za kitaifa zinazoshiriki kwenye mashindano . 


Misri inapokea mashindano hayo katika kumbe nne : uwanja wa Kairo ,mji mkuu wa utawala, uwanja mpya wa 6 Octoba na Borg Al_Arab . 


Na kuhusu maandalizi ya kamati kupokea mashabiki , alizingatia kufuata timu zote zinazoshiriki kwenye mashindano tangu waingie uwanja wa ndege wa Kairo , na itaoneshwa matokeo yote ya PCR kwa timu 32 zinazoshiriki , pia kupima joto kwa mashabiki watakaohudhuria mechi , matibabu ya kukinga yatasafisha daima mahali pa kukaa kwa mashabiki . 


Akiendelea kuwa : kamati itaanzisha kliniki kamili ndani ya hoteli zitakazopokea jumbe za kizungu kwenye mashindano , vilevile kufanya utakaso kamili kwa hoteli na vyumba vya wachezaji .


Comments