Hesham Nasr, mkuu wa shirikisho la mpira wa mikono na mkuu wa kamati iandaayo kwa toleo la 27 la mashindano ya mpira wa mikono duniani kwa wanaume _ Misri 2021,
alionesha maendeleo ya hivi karibuni yanayohusiana na kukaribisha mashindano, yatakayofanyika kati ya 13 na 31 Januari ijayo.
Hesham Nasr alisema katika mazungumzo maalumu kwa tovuti rasmi ya mashindano " tulikubali changamoto tangu mwanzo wa uamuzi wa kukaribisha mashindano yanayoshuhudia kwa mara ya kwanza kushiriki kwa nchi 32 pamoja na changamoto nyingine nayo ni virusi vya Corona lakini tunafanya kazi chini ya kauli mbiu ya (Ndio tunaweza).
Hesham Nasr alieleza kuwa kujiandaa kwa mashindano hugawanyika kwa sehemu 3 , nazo ni : upande wa kimuundo, taratibu na kiufundi.
Nasr aliendelea "sehemu ya kwanza maalum ya majengo, tumekaribia kukamilisha kumbi 3 mpya mjini mwa 6 Oktoba, Borg Al Arab na mji mkuu mpya wa utawala, na tutakuwa na mashindano ya majaribio pamoja na kuboresha ukumbi wa uwanja wa Kairo, hii ni pamoja na kumbi 10 za mazoezi tulijitahidi kuzikaribisha na hoteli ambamo timu zinazoshiriki zinapokaa".
Nasr aliongeza "kuhusu upande wa taratibu tuna kamati za kiwango cha juu na kuwasiliana moja kwa moja na Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo, na kazi yaendelea kwa kasi ili mashindano yatoke nje kwa mkali kama ilivyo kawaida ya Misri katika kuandaa vikao vya kimataifa".
Nasr aliendelea "sehemu ya tatu ya kuandaa, huhusiana na upande wa kifundi ambapo tuna kocha kwa kiwango cha juu cha ufanisi naye mhispania "Roberto Garcia Barondo", na tulifanikiwa kushinda msimbo wa mashindano ya mataifa ya Afrika ambao uliotufikisha Olimpiki ya Tokyo majira ya joto ijayo, na licha ya matatizo kwa sababu ya virusi vya Corona hata hivyo, tumeweka hatua zote za tahadhari; kulinda timu zote pamoja na mipango ya kuandaa timu ya kimisri kwa mashindano kupitia kambi za ndani mpaka ndege kufunguliwa zaidi".
Nasr aliongeza "tuliheshimiwa kupanga mashindano ya dunia kabla ya virusi vya Corona na bila shaka kuibuka kwake kulituchelewesha kidogo lakini tuliazimia kutotuathiri hata kama kazi ni polepole kuliko tunayopenda, lakini tumekaribia kumaliza na inatimia kuwasiliana na shirikisho la kimataifa katika mambo haya yote ikiwa ni madogo au makubwa".
Nasr aliashiria "tunawasiliana na shirikisho la kimataifa pia kuhusu hatua za mahudhurio ya mashabiki na ikiwa nina uhakika kuwa mnamo miezi ijayo, mambo yatakuwa bora na kutakuwa na idadi nzuri ya mashabiki na mambo yatafanyika kwa kawaida".
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Mikono wa Misri alisisitiza kuwa yeye ni "mmoja wa watu wanaoweka malengo yanayoweza kutekelezwa ili nisikosolewe ukienda mbali na tamaa".
Na alisisitiza" tukiendelea kuwepo kati ya timu 8 bora zaidi duniani, hili ni jambo zuri, lakini tamaa yetu kuwepo katika mraba wa dhahabu (fainali) na hili litakuwa mafanikio ya kushangaza".
Na alisisitiza "ulimwengu ni kama kijiji kidogo, wakati janga la Corona likitokea, ulimwengu wote uliathiriwa sio tu Misri na hii ni aina ya Uadilifu. Kuahirishwa kwa olimpiki ya Tokyo kuliathiri timu ya kimisri kwa kweli na hii kwa sababu timu ingekuwa ikicheza kati ya timu 12 bora ulimwenguni.
Na aliendelea "athari hiyo haikuwa kwa sababu ya kuahirishwa kwa olimpiki ya Tokyo tu lakini kukomesha kila kitu, na tunatatua hayo kwa kambi za ndani ili kuboresha kiwango cha mwili na tunaandika kwa nchi zingine ili kupambana Misri na zingine kukaribisha kambi ya nje baada ya kufungua kwa ndege".
Nasr aliashiria kuwa "kuwepo kwa Dokta Hassan Mostafa katika urais wa shirikisho la kimataifa hufanya mambo yawe magumu zaidi kwetu, kwani yeye ni mtu mwenye nguvu sana na aliyejipanga sana, hapendi kuona kosa lolote ili isisemekane kwamba yeye anapendelea Misri".
Aliendelea "wakati wa Janga la Corona alikuwepo nchini Misri na alijaribu kuchunguza kumbi yeyebmwenyewe mnamo kipindi hicho ili kuangalia utayari wake, na akizingatia mafanikio ya mashindano kwa ajili ya mpira wa mikono pia kujisikia fahari ya kuwa mtu mmisri".
Rais wa shirikisho la mikono alieleza furaha yake kwa wazo la kuathiri kwa mashindano juu ya ongezeko la msingi kwa watendaji na mashabiki wa mchezo nchini Misri "idadi ya watendaji inapoongezeka, tunaweza kuchagua ubora wa hali ya juu zaidi, na tulisaini itifaki na wizara ya elimu baada ya mashindano ya dunia ya wachipukizi ili kugundua talanta".
Comments