Waziri wa Vijana na Michezo na mwenzake wa UAE wafanya kikao cha mazungumzo kuhusu ujasiriamali wa vijana na uchunguzi wa Anga Za Juu

 

Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na Dkt. Sultan bin Saif Al Neyadi, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Masuala ya Vijana wa Falme za Kiarabu, walifanya kikao cha mazungumzo na baadhi ya vijana wa Misri kutoka majimbo mbalimbali kuhusu ujasiriamali wa vijana na uchunguzi wa  Anga Za Juu .


Dkt. Ashraf Sobhy alianza mkutano huo kwa kumkaribisha Waziri na vijana waliohudhuria, akisisitiza umuhimu wa mikutano hii katika kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano wa Kiarabu katika nyanja ya uwezeshaji wa vijana.

Waziri wa Vijana na Michezo pia alisisitiza kwamba vijana ndio viongozi wa siku zijazo, na lazima sote tuwaunge mkono ili kufahamu changamoto za kimataifa na fursa za uvumbuzi na ubunifu. Mkutano huu unawakilisha hatua nyingine kuelekea kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Misri na UAE, na kutoa fursa kwa vijana wetu kufaidika kutokana na uzoefu wa kusisimua kama ule wa Dk. Sultan Al Neyadi."


Kwa upande wake, Dkt. Sultan bin Saif Al Neyadi alizungumza kuhusu uzoefu wake wa upainia kama mwanaanga wa kwanza Mwarabu kufanya safari ndefu kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu, ambapo alipitia changamoto alizokabiliana nazo na jinsi safari yake ilivyokuwa chanzo cha msukumo kwa vijana wa kiarabu.

Alieleza, akisema: “Safari yangu ya  Anga Za Juu  ilikuwa ni uzoefu wa kipekee ambapo ilibeba ndoto na matamanio ya vijana wa UAE na Waarabu hadi kwenye upeo mpya miaka 5 iliyopita tulikuwa watu wa kawaida, lakini tulikuwa na ndoto kubwa na fursa hiyo iliwasilishwa kwetu, na kwa mipango mizuri, tuliweza kufikia hapa tulipo sasa.”

Mwishoni mwa hotuba yake, Dkt. Sultan bin Saif Al Neyadi, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Masuala ya Vijana huko Miliki Za Kiarabu, alikuwa na nia ya kufikisha ujumbe kwa vijana na kusisitiza harakati zao za kutimiza ndoto zao, bila kujali jinsi zinavyoonekana kuwa haiwezekani, na. kuvumilia na kujifunza kitu kipya kila siku.